Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Mkuu mimi bado nafuatilia.Hii ndo sehemu pekee iyounganisha hizi halmashauri nne za mkoa ndo maana kwa Sasa imezungukwa na makazi kibena
View attachment 2532206![]()
Sasa naona tovuti imeanza kubadilika kidogo ni jambo zuri.
Jaribu kuhakikisha mtu anaeshughulika na hiyo tovuti aenda na wakati na tovuti yasheheni taarifa zote muhimu.
Kwa mfano hakuna taarifa zozote za mwezi Februari jambo ambalo si la afya kidogo.
Tatu, jaribu kuhakikisha tovuti ya mkoa ni dynamic yaani mtu aweze kufungua ukarasa zaidi ya mmoja bila kuathiri mwonekano (visual appeal) na muundo (layout). Tovuti isiwe yasimama (static) kwamba kila karasa ipo katika eneo moja tu na ni hapohapo.
Mwisho, msiogope kuwekeza katika masuala kama websites maana hizi ni dirisha la kwanza kabisa kwa mgeni khasa anotokea masafa ya mbali. Static website yahitaji manual updating lakini dynamic itakupa sehemu mbili yaani "client side scripting" na "server side scripting". Hizi njia zakupa website ambayo ni ya kisasa, yenye kujazwa taarifa kwa "real time" na ipo salama zaidi kwasababu kwenye "client side scripting", Java huweza kutumika.
Huo ni ushauri kwa kifupi sana lakini naamini utashughulikia kwani Halmashauri ya Njombe ina pesa ya kutosha kwa mambo madogo kama kugharamia website.