Zitambue fursa za kiuchumi katika Mkoa wa Njombe

Zitambue fursa za kiuchumi katika Mkoa wa Njombe

Mkoa wa hovyo watu wa majungu, uganga, full uchawi sana, wasiotaka wageni wafanikiwe ni wenyewe tu watu wenye roho mbaya na za kwa nini. Huko kuishi mpaka uwe mwenyeji na kufanikiwa kutoka kibiashara uwe mtu wa madawa sana
Hayo ni majungu ya kuchafua mkoa wageni ni wengi Sana wamewekeza mkoa wa njombe na saiz wachina na wakenya wanamiminika kwa wingi mkoa wa njombe una fursa kibao
 
Hao wameomba ekari Zaid ya 1000 wanawekeza viwanda vya parachichi mkoa wa njombe now ni moto
IMG_4060-768x512.jpg
 
Pole mkuu,
Nadhani njombe ndo sehemu rahisi sana kwa wageni kuingia na kuwekeza mkuu. Maana kama ni ardhi ipo na inapatikana, hali ya hewa iko vizuri, usafiri 24/7 na biashara zinafanyika day and night. Uchawi upi unaousema wewe ambao haupo mikoa mingine mkuu?
Nimeishi miaka miwili Mkuu napafahamu vizuri sana sie ndio tulimpokea Mtaka na tukaondoka
 
Inawezekana mimi ndo siijui njombe vizuri, ila nipo njombe mwaka wa saba huu, na nimepita wilaya zote na vijiji vingi nimefanya nao kazi.
Mkuu wewe utakuwa ni mtu wa huko kusini huwezi kugundua ubaya wa mkoa wa Njombe huo mkoa kwa wageni sio mkoa wa kuwekeza
 
Nitajie wageni japo kadhaa tu waliowekeza mkuu, narudia tena kusema tena kwa ujasiri ni kwamba kwa mkoa wa Njombe ni ngumu kutoboa kama sio mwenyeji huko ni watu wana wivu hatari
Wivu gan mzee watu tunaongea tumewekeza njombe na tunaona watu wakimiminika kutoka mikoa mbalimbali wakiwekeza na hadi kutoka mataifa mengi hasa kutoka kenya ndo wamejaa na wachina ingia mtwango kaangalie wachina walivofungua viwanda vya singboard bado wakenye wamepanda parachichi za kutosha na na wamefungua viwanda vya usindikaji na bado kwenye chai jamaa njombe hujaizungukia vizuri ww bado ludewa huko ndo kwenye makaa wanamiminika
 
Back
Top Bottom