Zitambue fursa za kiuchumi katika Mkoa wa Njombe

Zitambue fursa za kiuchumi katika Mkoa wa Njombe

Soko kuu
Screenshot_20230304-131724.jpg
 
Around makambako sub town zinakua Sana hizi Zina fanya mji wa makambako uchangamke Sana mfano ilembula ,kipagamo na mtwango hii hapa ni ilembula
thumb_584_1130x480_0_0_auto.jpg
 
Mkoa wa Njombe: Mkoa wa Njombe una Halamashauri 6 ambazo ni Njombe Mjini, Vijijini, Ludewa, Makete, Wangingombe na Makambako.

Wenyeji wa Mkoa wa Njombe 70% ni wabena, ambao wanapatikana Wilaya za Njombe mjini,Vijijini, Makambako, Wangingombe na wakinga-Halamashauri ya Makete na Halamashauri ya Ludewa wapo Wapangwa na wanyasa.

Sifa muhimu za kiuchumi katika Mkoa wa Njombe
  • Ndio Mkoa unaongoza kwa Idadi ndogo ya watu kwa takwimu za awali za sensa ya 2022 Mkoa huo unakadiriwa kuwa na watu 889,946
  • Mkoa wa Njombe ni miongoni mwa Mikoa top 5 iliyo na watu wa vipato vikubwa zaidi kuliko Mikoa mingine.
  • Mkoa wa Njombe-Makambako kuna upepo wa kiwango kikubwa ambao unaweza kuzalisha umeme wa megawati zaidi ya 300
  • Unaongoza kwa uzalishaji wa mbao-Asilimia 60-70 ya mbao zote zinazotumika Tanzania zinatoka katika huo Mkoa-na zinalimwa karibu Halamashauri zote za Mkoa huo.
  • Unaongoza kwa uzalishaji wa zao la viazi mviringo 70% ya viazi vyote Tanzanua vinalimwa huko.
  • Unaongoza katika uzalishaji wa zao LA parachihi Tanzania nzima.
  • Ndio Mkoa unaongoza kwa madini ya Chuma na Makaa ya mawe. Kwa Tanzania akiba kubwa ya madini hayo yapo Mkoa huo na yanapatikana kule Luganga na Mchuchuma Wilayani Ludema.
Sifa nyingine:
  1. Unaongoza kwa wafanyabiashara wakubwa Tanzani a.k.a Wakinga
  2. Ndio Mkoa unaongoza kwa baridi Tanzania nzima hasa Njombe Mjini na Makete
  3. Mkoa wa Njombe ndio Mkoa pekee kwa kipindi cha miaka 5-10 unaongoza kwenye top 3 ya maambukizi ya HIV
  4. Mkoa wa Njombe ina Idadi kubwa ya Wanawake kuliko Wanaume kuliko Mikoa yote Tanzania.
N.B. Kama mtu upo interested kuishi mazingira kama ya Ulaya ulaya yenye baridi na green-Mkoa wa Njombe ndio jibu sahihi. Huko Mbu na nzi ni kama hakuna. Maelezo mengine kuhusu investment opportunities katika Mkoa huo tembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

Chai hujaitaja na fursa ya kilimo cha maua na apples kati ya mengi.
 
Fursa ya kibiashara ukanda wa tambarare makambako Hilo eneo linajumuisha maeneo ya mtwango ,kichiwa ,ikuna ninga ,igongolo na kata zote za makambako tc na wangingombe tc kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022 hili eneo Lina watu zaidi ya laki nne ambapo ni zaidi ya nusu ya watu wote waliopo mkoa wa njombe hili eneo asilimia kubwa lipo busy na biashara asilimia 90 makazi Yao yameungana na kitovu Chao Cha biashara ni makambako hii inafanya centre ya makambako Kuwa busy na biashara na pongezi kwa aliye buni mradi wa kujenga soko la kimataifa makambako maana ni eneo lililopo centre na Lina mwingiliano mkubwa wa watu
IMG-20230416-WA0004.jpg
 
Fursa nyingi, mfano maranda ya mbao unaweza tengeneza mkaa, au briquettes pellet ukaexport. Kuna mianzi ya kutosha unatengeneza bidhaa kibao za mianzi Mfano mkaa, mkaa wa kusafisha bidhaa za viwandani mfano mafuta nk, kutengeneza mbao , karatasi, vipodozi, nk
 
Moja kati ya barabara ngumu na ya kiume tanzania[emoji1787][emoji1787] makambako - njombe - songea - mbinga balaa tupu, hizo kitonga ziwe hata 10 ila hapo ndio mwisho wa matatizo
 
Kon
Moja kati ya barabara ngumu na ya kiume tanzania[emoji1787][emoji1787] makambako - njombe - songea - mbinga balaa tupu, hizo kitonga ziwe hata 10 ila hapo ndio mwisho wa matatizo
Kona Zinaanzia njombe mjini had songea makambako njombe imenyoka
 
Back
Top Bottom