Zitto aanika siri nyeti za Mbowe! Adai hatakufa kama Chacha Wangwe
Cdm mmezoea kufukuza watu ovyo pindi demokrasia inapokula upande wenu,ona Machali na wenzake walivoondoka cdm,sasa zitto ameamua aweke ujinga wa cdm wazi afu asepe,
baada ya zitto kusepa cdm itakuwa kama TLP.
Zitto komaa na usiongee na mbwa,ongea na mmiliki wa mbwa afu usepe
 
Alikuwa wapi siku zote.
Its toooooooooo late...

Never too late. Upinzani Tanzania bado saaaana. Wote ni hao hao tu. Mnatakaje? Kwenye vita kila mtu na mbinu zake za kivita. Those that live in glass houses shouldn't throw stones.
 
Viongozi wa siasa hawawezi kuwa waadilifu hata siku 1...CDM poleni saba
 
acha kuwa kama mfuasi wa kibwetele kama tuhuma za zitto ni za kweli ila za mbowe sio?
 
Wewe una uraia wa nchi gani? Kwa nini pia unapenda kufananisha chama cha siasa na SACCOS?
Basi wote SACCOS tu.. Huwezi kuniambia chama chenye watu kama Komba,Kinana au Nape (CCM) au Mbowe, Lema na Slaa (CHADEMA)ni makini. CCM na CHADEMA sio waleta maendeleo bora waruhusu wagombea binafsi tujue moja. Na wewe unadhani mimi raia wa wapi?
 
AMA KWELI FADHILI MBUZI UTAMLA NYAMA.............

Nampa pole sana Mh Freeman Mbowe, mwenyekiti wa Chadema Taifa kwa kutukanwa na kukosewa adabu na kijana mdogo, Msaliti Zitto Kabwe, ambaye leo mafanikio yake yametokana na yeye Mh Mbowe, lakini kasahau na kaamua kukutuna ati wewe ndo kamati kuu!

vile vile nimpe pole Mh Tundu Lissu Mbunge wa Singida mashariki na Mwanasheria wa chama, kwa kuitwa Kifaranga na huyu kijana ----- asiye na Adabu, we mpuuuze kwani leo amewadhihirishia watanzania kuwa hafai hata kuwa Balozi wa nyumba kumi......

Zitto Z Kabwe mpaka sasa hujakanusha tuhuma za kweli kabisa kwamba ulihongwa Magari mawili na Mh mkono iliusimsimamishe mgombea Msoma Vijijini, badala yake uliishia kujitoa ufahamu na kuwatukana Viongozi mtandaoni kuonyesha ulivyofilisika mawazo kama si kufilisika hoja!

Zitto Kabwe amejitoa ufahamu na kudai eti mtu asiyemuheshimu mke wake aliyewazalia watoto wake hawezi kumfundisha mtu maadili.......
Zitto, kabla ujanyoosha kidole kwa mwenzako embu jaribu kujitazama wewe mpaka leo una umri miaka 37 umeshindwa kuoa, na kinacho kusumbua ni uzinzi, embu kumbuka April tukio la aibu ulilolifanya pale Mount Meru Arusha, baada ya kunywa KONYAGI, mbona sisi hatusemi..........

Si jambo jema kujadili misha ya Binafsi ya Kiongozi, kwani hakuna aliye mkamilifu Chini ya Jua.......

SI VEMA MAAMUZI YA KAMATI KUU KUMBEBESHA MH MBOWE NA LISSU PEKE YAO..

Tatizo la mhuni ni gumu kutatuliwa na wahuni wenzake,Mtakoma kwa kijana wa Kigoma, mmezoea kunyonga na kufukuza,
R.I.P CHADEMA
 
Wakuu, inasemekana Zitto Kabwe ali-post facebook hii kitu halafu aka-edit later.

Original post:

Revised Post:
"Lissu anasema nimepewa magari 2 na Mzee Mkono. Anasema kaambiwa na Mkono. NaaminiMkono alimwambia pia mwaka 2005 alimpa Freeman Aikaeli Mbowe tshs 40m ili Mbowe asifanye kampeni Musoma vijijini.

Nadhani alimwambia pia mwaka
2008 (baada ya orodha ya mafisadi kutangazwa 2007) Mkono alimpa Freeman tshs 20m za uchaguzi wa Tarime na Freeman akasema kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa. Nadhani alimwambia pia kuwa Mwaka 2010 Mkono alimpa Mbowe tshs 200m za kampeni ya Slaa.

Pia
hakusahau kumwambia kuwa Rostam Aziz alimpa Mbowe tshs 100m za kampeni. Lissu anajua kuwa gazeti la Tanzania Daima limeanzishwa na fedha za chama kutoka Conservative party?

Nimefanya internship yangu kwa
Mkono and Company Advocates kuhusu masuala ya mikataba. Mzee Mkono ni Mzee wangu na alisaini petition ya kumtoa Waziri Mkuu Pinda. Lissu awaambie waliyemtuma wamwambie ukweli wote. Lissu ajue yeye ni kifaranga tu, Mimi namtaka mama wa kifaranga ajitokeze. Aeleze aliingia deal gani na Kinana na Sumaye mwaka 2005 kufuatia deni lake NSSF. Aweke wazi mkataba kati yake na NHC kuhusu nyumba ya Umma ilipo Club Bilicanas.

They must know I am not a push over. Chacha died, I won't. Mtu ambaye hawezi kuheshimu mke wake aliyemzalia watoto hawezi kunyooshea mtu kidole kuhusu maadili."

Kutoka Gazeti la Raia Tanzania
It is the last kick of a dying horse.
 
Leo ni mekata tamaa kuhusiana na siasa hasa za bongo mpinzani kupewa au kukopa pesa kwa mtu ambaye anasadikika ni fisadi na wachama tawala.Je mbavu za kumkosoa na kumwajibisha huyo wa chama tawala atakuwa nazo?

Kweli siasa mchezo mchafu.

source:gazeti la Rai
 
MOSES MACHALI.
"Hayo hapo chini ndiyo maneno aliyoyasema kupitia mtandao wa kijamii, jisomee ujue anachokisema na majibu ujipe mwenyewe>>>>"

Moses Machali
Kuna watu wanazungumzia nidhamu na kwamba ili mtu uweze kufanikiwa maisha ni lazima uwe na nidhamu. Nami nakubaliana na kauli hiyo, lakini tunapaswa kujiuliza ni nidhamu ya aina gani?

Inawezekana mtu akasema ZITTO hana nidhamu kwa chama chake lakini ikawa ni kinyume chake. Hii ni kwa sababu hana nguvu za kufanya maamuzi ndani ya chama na kwa hiyo akawa anatakiwa kutii mambo ambayo yako kinyume cha utaratibu wa chama chake lakini kwa kuwa yanatolewa na kusimamiwa na watu wenye nguvu basi akipinga anaonekana hana nidhamu. Binafsi niseme moja tu kwamba, wakati mwingine sisi wanasiasa tunakurupuka na kukosea.

Katika sakata la zitto na CDM nadhani pande zote zinaweza kuwa na makosa kwa kuwa hadi mambo yamefikia hapo yalipofika ni kwa sababu kumekosekana collective responsibilty na imekosekana pia nidhamu ya kiuongozi inavyoonekana kwa kuwa hata akina Mbowe; Dr. SLAA na wengine siyo malaika wakati mwingine nao hukosea tena sana.

Na kwa hiyo napingana na wale wote wanaosema mkosefu ni Zitto tu la hasha ni uonevu kwa upande mmoja.

Lakini pia napingana na wale wote wanaosema Zitto anaonewa tu la hasha inawezekana kweli kukawa kuna makosa tofauti na historia tunayoifahamu wachache. Ngoja niwakumbushe kidogo wana jamvi: Mwaka 2009 wakati wa uchaguzi ndani ya CDM uliibuka mgogoro kati kundi la Mbowe na kundi la Zitto ambapo wazee wa chama wakamtaka Zitto aache kugombea uenyekiti wa chama kwa kuwa yeye ni kijana bado ana muda mwingi na kwamba anaweza kugombea wakati mwingine na kwa hiyo amwachie mbowe kwanza akiongoze chama.

Finally Zitto alijiondoa kwa shingo upande yaani pasipo kupenda na wafuasi wengine wa Zitto wakakutana na majanga mazito ndani ya CDM na wakaamua kuondoka CDM wakaitwa majina ya kwamba wao ni sisimizi nk; wakati mwingine wakaitwa Wasaliti na watu wenye njaa nk. Waliopatwa na kadhia hiyo baadhi ni hawa wafuatao: mhe. david KAFULILA(MB), MARTINE DANDA kutoka Iringa.

Wengine ni akina Mhe. Mkosamali(mb) pamoja nami Machali(mb) na baadaye kabisa waliondoka akina Mama Msole nwengineo. Wapo wadau wasemao kwamba huenda mgogoro uliopo hivi sasa unatokana na kile kilichotokea 2009 kwa kuwa CDM walipaswa kufanya uchaguzi lakini wakaahirisha kwa kile kinachosema kwamba watamwambia nini Mhe. Zitto mwaka huu katika kugombea Uenyekiti wa chama kama ilivyo dhamira yake ya siku nyingi ya kukiongoza CDM.

INASEMEKANA kwamba baadhi ya viongozi wa CDM wenye nguvu ndani ya chama wametafakari ni namna gani Zitto hapenyi katika kinyanganyiro cha uchaguzi ikaonekana ni ngumu sana na kwamba inabidi kuangalia namna ya kufanya na huenda ndiyo haya tunayoyaona sasa. Aidha Ikumbukwe kuwa kuna nyakati vyombo vya habari vilimnukuu Mhe. Mbowe akisema kwamba Dr. Slaa ndiye atakaechukua fomu za kugombea Urais na kwamba yeye hatagombea tena(Mbowe), Lakini Zitto amekuwa akitangaza nia ya kugombea Urais anakutana na vikwazo au mikwara mingi kutoka kwa baadhi ya viongozi na wanachama wa CDM. Na baadhi ya vyombo vya habari vilipata kumnukuu Mzee Mtei akimshauri Mhe. Zitto kuachana na masuala ya kutangaza nia ya kuombea urais kwamba ni kusababisha fujo au vurugu ndani ya CDM na kwamba atulie hadi wakati ukifika.

Tujiulize mimi na wewe, inakuaje Zitto akitangaza nia iwe kosa lakini Mbowe akitangaza nia iwe ni sawa wakati kwa mujibu wa katiba ya CDM kuna mamlaka inayotakiwa kumtangaza mgombea urais ni nani lakini pia sidhani kama kuna mahala katiba ya CDM inakataza Mwanachama wake kutangaza nia ya kugombea nafasi fulani kama vile urais.

Kama kuna kipengele hicho CDM wanapaswa kukionesha ili kuondoa mashaka yaliyopo juu ya kwamba wanamuonea Mhe. Zitto. Hata hivyo wapo wanachama wengi wametangaza nia kugombea Ubunge ndani ya CDM mwaka 2015 kama ilivyokuwa kwetu sisi kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010; tulitangaza nia sana tu; wote akina Wenje, akina HAINESS KIWIA na wengine na hawakuelezwa kwamba wanaleta fujo ndani ya CDM.

Ndugu zangu ndiyo maana ninakuwa na mashaka wakati mwingine kwa kusema kwamba huenda kweli Mhe. Zitto akawa anaonewa kama anavyosema, mtazamo huu unatokana na records hizo za nyuma. CDM wajitokeze kufafanua hoja hizo ili nasi makomredi wao kimkakakti tuweze ku clear dout. Inawezekana baadhi wakaja na maneno maneno yaliyozoeleka kwamba nimetumwa na Zitto nk.
La hasha ni utashi wangu tu kutokana na uzoefu wangu katika siasa za CDM na sasa niko NCCR-Mageuzi. Uzoefu wangu usibezwe kwa kuwa ninayo
Email This
BlogThis!
Share to Twitter
Share to Facebook
at 1/05/2014 03:10:00 AM


Mkuu na swali jepesi juu ya hoja ya Machali. Ivi Kwanini Zimbabwe waingereza walikua hawataki kulipa fidia za ardhi iliyokua inamilikiwa na wazungu wachache, kulipa kupitia serikali ya Mugabe kutokana Na Mkataba Wa fidia walioingia Kati ya serikali na waingereza?
 
ila watu wanavituko sana ivi mini kabaang wa kutuambia sisi wakazi wa dar tunaongoza kwa kula vichwa na miguu ya kuku???
 
zito hawezi kuongea na mbwa tundu lisu.anaongea na mwenye mbwa mbowe
 
Ndg wanaJF naomba mnisaidie, hivi huko Kigoma kuna nini?

Nauliza hivi kwa kuwa watu wengi niliowakubali na pengine kuwafanya mfano wangu wa kuigwa (ROLE MODELS) wamenisaliti. Kuja kutafakari woote walionisaliti hasa wanatoka sehemu moja, Kigoma!

Nilipokuwa na umri wa 18 tu nilimkubali nakumpenda sana Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Dr Aman Walid Kabourou ambaye pia alikuwa katibu mkuu CHADEMA cha ajabu na sintosahau mwaka 2005 pale Dr wangu huyu aliposhindwa ubunge lakini wakati nauguza majeraha yangu haya nikasikia Dr Kabourou huyooo CCM! Mara kateuliwa kuwa Mbunge EAC na sasa M/Kiti wa mkoa Kigoma CCM. Thanks Dr Kabourou umenisaliti lakini umenipa somo la maisha ya kuwa sintamwamini ama kumfuata mtu yeyote zaidi bali ntajifunza kanuni, sheria na taratibu za taasisi husika ziniongoze, siyo MTU! Afer all, the Bible says, "AMELAANIWA AMTEGEMEAYE MWANADAMU."

Lakini mbaya zaidi miaka ya 2008/9 nilimsikiliza kijana mmoja anayejiamini, anajenga na kutetea hoja zake vizuri anaitwa David Kafulila, ama kweli nilimkubali! Siku chache nikashtukia anatimuliwa CHADEMA huku akitetewa na baadhi ya watu akiwepo Zitto Kabwe nikafikiri labda anaonewa lakini kwa hakika aliondolewa akapokelewa NCCR baadae akawa mbunge wao 2010 kupitia jimbo 1 huko Kigoma Kusini. Kilichonishtua kijana huyu ndani ya miezi michache tu akaibua tuhuma nzito juu ya m/kiti wake taifa Mh. James Mbatia. My ghosh, jana tu ulipokelewa leo yamekuwa haya!

Haya basi labda hawa wanasiasa twende kwingine, kama mnazi wa SIMBA hakuna mtu tuliyemkubali kama Kipa namba 1 na NAHODHA wetu JUMA KASEJA. Cha ajabu mara kasepa YANGA.Jaman watani wa jadi! Ok karudi tukamsamehe haijapoa uh huyoooooo tena YANGA! Jaman Kigoma mtaniua!

Nami niseme nini kuhusu yule m/kiti wangu wa CDM tawi la SAUT 2009/10 Mh Machali sasa mbunge NCCR Kasulu-Kigoma, RICHARD TAMBWE HIZA yule m/kiti wa CUF Temeke na mgombea wa chama icho Temeke 2005 sasa Mkurugenzi wa PROPAGANDA CCM, Shekh maarufu Isa Haji Ponda mwenye saili ya Kigoma, ata sikuelewa hasa madai yake yalilenga nini hasa na kwa maslahi ya nani? Yule mwimbaji maarufu Dimond Platinum mara kwa Wema mara sijui Wolper mara kujenga Msikiti mkubwa!

Na sasa yule mwanasiasa anayedaiwa maarufu Zitto Zuberi Kabwe! Najua atawahangaisha sana lakini naamini hana chochote kabisa la kutusaidia waTz. Kwangu mimi nilimdelete tangu 2009 kwa kauli zake tata zisizokuwa na msaada kwa CDM na ata taifa hili. Leo wengine watauawa bure kwa ajili yake but mkumbuke kati ya viongozi wachache wa cdm wasioonja kichapo cha polisi basi nadhani Zitto namba moja. Mtakufa kipumbavu kwa ajili ya b7!

Naomba NDG wanajamvi tusaidizane why always KIGOMA, Kulikoni? Kigoma kuna'ni??????????????????????
 
ZITO AFUKUZWE TU HANA JIPYA. Kama ni uvumilivu basi umefikia kikomo! Kwa hapo alipofika hastahili tena kuwa mwanachama wa CHADEMA aende huko alikotumwa watampokea. Na chama kikikuchoka una haja gani ya kung'ang'ania si uondoke tu kama wenzako walivyofanya.
 
Wapenda mabadiliko ya kweli tunahitaji umakini wa hali ya juu katika huu mgogoro kwa maana upande wa MM umejipanga vizuri zaidi ya hata hiyo CC. Na sio ajabu wengine wanailaumu cc kwa kuchelewa kuchukua maamuzi haya. Kwa gear waliyoanza nayo ya mkutano wa SERENA usitegemee watatulia tu hivi hivi, huenda zikatoka hata siri za ndani (ambazo kimsingi ni weaknesses za taasisi au mtu yeyote) lakini daima wanaotoa hivi vyote kitakachowasuta ni nia na dhamira zao ....yaani wanachowaza moyoni na wanachotueleza sisi.
 
Acha ujinga wewe hujui hata siasa zilivyo, mbona mbowe na lissu hawakufunguka na kuwaeleza umma kuwa zitto alipoewa magari 2 na mkono? usiwe na akili za nyumbu
 
Back
Top Bottom