Zitto aanika siri nyeti za Mbowe! Adai hatakufa kama Chacha Wangwe
mkuu jamii inataka nini na wewe unasema nini hapa, ni sahihi kutumia fedha chafu katika jambo halali??? mpaka hapo credibility ya mwenyekiti ipo hoi

jamani tupeane ushahidi siyo umbea umbea tu. waliomtuhumu zitto wameleta ushahidi na zitto naye atuletee ushahidi tumwamini.
 
Kwa hiyo mtu akikutuhumu tu bila kutoa ushahidi basi mtu ajiuzuru tu,basi hii itakuwa nchi ya wajinga!

tunahitaji utetezi wa hizi tuhuma otherwise tuna haki ya kuamini kua ni kweli...
 
Siku zote huwa sana Zitto kuwa ni janga kwa kizazi hiki, wanaJF huyu Zitto alikuwa upande wa Mbowe kumpinga Chacha Wangwe, Na ni Zitto ndiye aliyekuwa kinara cha kumponda Wangwe na kumuita msaliti mnafiki lakin leo Zitto anakuja akijifanya kuwa yeye yupo upande wa marehemu wangwe.. Huu ni unafiki mkubwa usio hata na chembe ya aibu.
 
Last edited by a moderator:
Tuhuma kuwa Mbowe alipewa pesa na zikatumika kwenye kampeni za chama, tarime (ubunge) na kwa Dr Slaa (uraisi), sioni kama ni tatizo. Tena tulitakiwa kumsifu Mbowe kama strategic CEO anayeweza kusolicit funds kufanikisha malengo ya organisation. Hii ni kwa sababu hapa hakupewa kama Mbowe, bali CHADEMA. Nadhani tuhuma za Zitto zingekuwa na mashiko kama angesema kama Mbowe alishapewa pesa kwa ajili ya kusaliti chama kama ilivyo kwa Zitto aliyepewa magari ili auze jimbo. After all Zitto kama mtu aliyekuwa naibu katibu mkuu tutamshangaa kwa kukosa collective responsibility na bado akajipambanua kama kiongozi anayefaa kuaminiwa. Mbona hajalalamikia pesa ambazo CHADEMA ilishawahi kupewa na Sabodo ambaye naye ni mwanaCCM? Zitto asitutoe kwenye reli, ajibu hoja, " je alihongwa na akauza majimbo ya uchaguzi kwa CCM? Full stop.

Pili, inawezekanaje sasa hivi Zitto anataka tumuamini kwa asemayo, ili hali maneno yake yamekuwa yakibadilika siku hadi siku. Ikumbukwe, ni Zitto huyu huyu aliyesema kwenye press conference kuwa alijiondoa kuwa signatory wa chama tangu mwaka 2010, ilhali kumbe hajawahi hata kuwa. Pili ni Zitto huyu huyu aliyejipambanua kuwa ana majina ya watu walioficha fedha Uswisi, na hadi leo kushindwa kuyatoa, na badala yake kuishia kuapa kuwa hana. Tatu, ni Zitto huyu huyu aliyetudanganya kuhusu mshahara wa waziri mkuu. Nne ni Zitto huyu huyu kwenye moja ya maandiko yake amewahi kusema ana magari matano, lakini jana kasema anayo mawili. Sasa tutamwaminije. je huoni kuwa kama ilivyo kawaida yake anataka kudivert attention yetu? Uongo wake unaweza kuorozeshwa kwa listi ndefu sana.

Zitto si msafi tena na hasafishiki. Period

Mbowe kwisha kayeyuka kama nta....yale madai ya saccos yametimia hoja ni kwamba kwanini akubali kuchukua fedha za mafisadi ambao waliwasoma pale mwembe yanga? Kuna agenda gani ya siri kati yake na mkono pamoja na rostam? Chadema ni genge la wahuni na huyo babu yenu apumzike atakufa kwa presha
 
Mbowe anapewa pesa na CCM alafu anasema sio tatizo,huku upande wa pili wanamtukana Zitto na kusema anatumika na CCM bila ushahidi

Alafu badala ya kupeleka kwenye chama kama "msaada" toka CCM,yeye anaenda kukopesha Chama!!huyu hafai kuwa kiongozi

Sitashangaa kusikia hizo pesa ndo zilizotumika kufanya starehe Dubai na Joyce Mukya!
mkuu inashangaza sana wanachedema kushangilia maovu kama haya ni aibu kwa chama..
 
Kwa hiyo mtu akikutuhumu tu bila kutoa ushahidi basi mtu ajiuzuru tu,basi hii itakuwa nchi ya wajinga!

Huna taarifa kwamba amekiri kuwa kweli amepokea "misaada" toka CCM kwa ajili ya CHADEMA ila akaenda kukikopesha chama?
 
Amen chadema tutashinda kwa nguvu za Mungu hawa wahuni wadogo tutawafukuza wote.
 
hakika mtu alie li engeneer hili sakata ni jasusi wa hatari....
 
Haya maneno ndiyo yanaoyozidi kudhihirisha udhaifu wa Zito. Angekuwa mtu thabiti, asingenyamaza na madhamabi ya namna hii siku zote, ithabiti ni ama kujiuzulu, au kumpinga anayefanya makosa hadharani, siyo ukumbwe na kashafa ndiyo ujitetee kuwa wengine pia wanazo. Siku za nyuma kidogo alianadika kuwa amekuwa munge kwa miaka mingi na aliwahi kuwa kwenye kamati mbalimbali, ndiyo m,aana ana uwezo mkubwa wa kipesa, lao hii anaanza kukiri kuwa pesa hiyo huwa anapata kwa njia za hongo. Watu wa namna hiyo huwezi kuwaamini kuwa viongozi wa taifa.

Zitto ameshapambana sana na hayo ndani ya chama na ndiyo asili ya kuitwa msaliti ambayo kwa tafsiri ya akina Mbowe ni mnoko/mvurugaji wa deal..

Na kwa sasa akiwa nje,ni sahihi sasa kutuonyesha yale aliyokuwa anapambana nayo ndani ya Chadema na kwa nini mahusiano yake na wenye chama yamefikia hapa.
 
mkuu jamii inataka nini na wewe unasema nini hapa, ni sahihi kutumia fedha chafu katika jambo halali??? mpaka hapo credibility ya mwenyekiti ipo hoi

wewe ni stroke inakusumbua meza mavi kutwa ma 3.utapona......
 
sasa watetezi wa Mbowe na wa Zitto hapa mnisaidie.

Je, ni makosa Zitto kupewa magari mawili na Mkono na halali Mbowe kupewa Fedha na mtu huyo huyo kwa malengo tofauti??

Na Rostam naye anaingia vipi??
 
Mbowe kwisha kayeyuka kama nta....yale madai ya saccos yametimia hoja ni kwamba kwanini akubali kuchukua fedha za mafisadi ambao waliwasoma pale mwembe yanga? Kuna agenda gani ya siri kati yake na mkono pamoja na rostam? Chadema ni genge la wahuni na huyo babu yenu apumzike atakufa kwa presha

kwanza unatakiwa uprove kuwa ni kweli alichukua. Pili, unless useme beyond reasonable doubt kuwa alichukua kwa makusudi ya kusaliti chama. Mbona hujahoji pesa zilizotoka kwa Sabodo?
 
Dr.W.Slaa anaona aibu hata kuingia na kuchangia mijadala humu JF, Nafsi inamsuta.
 
NATAMANI ZZK AFANYE MKUTANO WOWOTEEEEEE WA HADHARA TUONE KAMA KALE KA KAULI KA TL KATAFANYA KAZI HAHAHAHAA...!!!

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom