Tuhuma kuwa Mbowe alipewa pesa na zikatumika kwenye kampeni za chama, tarime (ubunge) na kwa Dr Slaa (uraisi), sioni kama ni tatizo. Tena tulitakiwa kumsifu Mbowe kama strategic CEO anayeweza kusolicit funds kufanikisha malengo ya organisation. Hii ni kwa sababu hapa hakupewa kama Mbowe, bali CHADEMA. Nadhani tuhuma za Zitto zingekuwa na mashiko kama angesema kama Mbowe alishapewa pesa kwa ajili ya kusaliti chama kama ilivyo kwa Zitto aliyepewa magari ili auze jimbo. After all Zitto kama mtu aliyekuwa naibu katibu mkuu tutamshangaa kwa kukosa collective responsibility na bado akajipambanua kama kiongozi anayefaa kuaminiwa. Mbona hajalalamikia pesa ambazo CHADEMA ilishawahi kupewa na Sabodo ambaye naye ni mwanaCCM? Zitto asitutoe kwenye reli, ajibu hoja, " je alihongwa na akauza majimbo ya uchaguzi kwa CCM? Full stop.
Pili, inawezekanaje sasa hivi Zitto anataka tumuamini kwa asemayo, ili hali maneno yake yamekuwa yakibadilika siku hadi siku. Ikumbukwe, ni Zitto huyu huyu aliyesema kwenye press conference kuwa alijiondoa kuwa signatory wa chama tangu mwaka 2010, ilhali kumbe hajawahi hata kuwa. Pili ni Zitto huyu huyu aliyejipambanua kuwa ana majina ya watu walioficha fedha Uswisi, na hadi leo kushindwa kuyatoa, na badala yake kuishia kuapa kuwa hana. Tatu, ni Zitto huyu huyu aliyetudanganya kuhusu mshahara wa waziri mkuu. Nne ni Zitto huyu huyu kwenye moja ya maandiko yake amewahi kusema ana magari matano, lakini jana kasema anayo mawili. Sasa tutamwaminije. je huoni kuwa kama ilivyo kawaida yake anataka kudivert attention yetu? Uongo wake unaweza kuorozeshwa kwa listi ndefu sana.
Zitto si msafi tena na hasafishiki. Period