Zitto aanika siri nyeti za Mbowe! Adai hatakufa kama Chacha Wangwe
people should not stay in one side!! MBOYE SIO MSAFI THE WAY PEOPLE THINK,cdm kwa sasa ni lazima wa overhaul safu ya uongozi yenye watu waadilifu mapema sana || binafsi nimekosa imani nayo kabisa || kama wako tayari kuhongwa ili waachie jimbo je hao ni wanasiasa wa dhati au ni wafanyabiashara
 
Katika mahojiano aliyoyafanya M/Kiti wa chadema na gazeti la Raia
Tanzania ametoa hiyo kauli. Na hii ni baada ya Zitto kumtuhumu ya
kuwa alipewa Fedha na waheshimiwa/vigogo wa CCM.

Kumbe CCM imewasaidia wengi sana Tanzania....................
Huyu ni M/Kiti wao bado hawa wa ngazi za chini. Hivi ni nani aliye
msafi chadema ambaye anaweza kusimama mbele ya Watanzania.???
 
Mkuu na swali jepesi juu ya hoja ya Machali. Ivi Kwanini Zimbabwe waingereza walikua hawataki kulipa fidia za ardhi iliyokua inamilikiwa na wazungu wachache, kulipa kupitia serikali ya Mugabe kutokana Na Mkataba Wa fidia walioingia Kati ya serikali na waingereza?
uhusiano wa hoja unaoitoa na hoja ya machali ipo wap?
 
Swali sio Chadema Wala CCM wananchi wa Tanzania wanatakiwa kuacha kushabikia watu Bali kuangalia chama gani kina Sera nzuri na kuangalia kilicho madarakani kinatekeleza Sera zake au ni kupotezea watu muda bila kuwapa maendeleo.
Tunahitaji sana progressive politics na sio ushabiki kama wa mpira wa kujaa kwenye mikutano ya hadhara hizo ni siasa za kizamani siasa za kisasa ni kuwa fikia watu kupitia media kwa twitter, Facebook , TV , Radio na nyumba kwa nyumba kutumia leaflet , mahali pa kazi kwa idhini ya management na sio kupotezea muda watu kwenye mikutano ya hadhara. Wanasiasa ukiona watu wengi wanajaa kwenye mikutano yako ujue kuwa wengi hawana ajira na sio Jambo la kufurahia inatakiwa uwape ufumbuzi wa tatizo la ajira.
Nawaomba wanasiasa wa Tanzania mpunguze kuwapotezea muda wananchi angalieni njia hizo mbadala nilizoziweka hapo juu njisi ya kuwafikia watu kirahisi na kisasa bila kuwapotezea muda maana mnawazidishia Umaskini . Msipoangalia historia itawahukumu kwamba mlikuwa mnafanya mambo bila kutumia akili.

Vilevile huu ushabiki wa sijui Zito sijui nani ni upuuzi mtupu badala ya kutatua matatizo ya maisha mnapoteza muda na pesa zenu kumzungumzia mtu. Huu ni ujinga wa hali ya juu kuna watoto hawana madawati , madarasa na mavazi ya kuendea shule pamoja na wakina mama wajawazito badala ya kujadili kutatua matatizo mnaendeleza ushabiki ndio maana Tanzania ina kila kitu lakini inaendelea kuwa maskini.
 
Katika mahojiano aliyoyafanya M/Kiti wa chadema na gazeti la Raia
Tanzania ametoa hiyo kauli. Na hii ni baada ya Zitto kumtuhumu ya
kuwa alipewa Fedha na waheshimiwa/vigogo wa CCM.

Kumbe CCM imewasaidia wengi sana Tanzania....................
Huyu ni M/Kiti wao bado hawa wa ngazi za chini. Hivi ni nani aliye
msafi chadema ambaye anaweza kusimama mbele ya Watanzania.???

Kwa hiyo ccm wana fedha chafu!?
 
''Nitakuwa wa mwisho kutoka CDM'' Atafanya kazi na nani kwa matus hayo kwa Mbowe. Somebody who is aspiring to contest for presidency in future tayari amejiharibia, mtu smart hawezi kumchagua kuwa raisi as ataweza toa siri za nchi au kuuuza nchi kwa maadui baada ya kukorofishana na wenzake in the government.

We know that siasa SI HASA tunachoona au kusikia as vingine ni kama hizo pesa za kina Mkono, remember that Nyerere alikikubali CHADEMA tangu kikiwa kichanga na Mkono anatoka kumoja na Nyerere, yawezekana Mkono ni mpambanaji ndani ya CCM au wakati haujawadia wa yeye kuwa-join wapambanaji kwa uwazi.

Jibu la Mbowe nisahihi that ZZK hawezi elewa sababu ya yeye kupewa pesa na hana sababu ya kutueleza. I can say that Mbowe amepevuka kisiasa na it was right for not allowing ZZK to contest for chairmanship. Mnaweza kumpima sasa kuwa ni mpenda sifa, watu(CCM) wanapofurahia anavyotoa matusi kwa Mbowe kwake ni burudani. Na chama atakachojiunga nacho wakae kwa tahadhari as he has proved that yeye si mwanasiasa. Angetulia hata wana CDM wangeweza kumtetea. Kwa sasa yeye ni adui wa watanzania ambao walikuwa na mtumaini na CDM kuwatoa utumwani bila kujali huko jikoni mapishi yanaendeleaje.
 
Pamoja na mihela yote na viwanja/majumba/hoteli ulizorithi kwa baba yako lakini
bado unapokea vijisenti vya CCM???? Si mnazihiita ni pesa chafu refer 'List of shame'

Sasa mimi ambae ni kijana nina kadi ya chadema sina kazi, kwetu hakuna mali, nimesoma
sina kazi nitaziacha kweli hizo PESA za CCM zikija nje nje????
 
Hapa zililetwa tuhuma kwamba Zitto kapewa pesa dola mia ngapi sijui na CCM,mapovu yaliwatoka sana

Leo mwenyekiti "wetu" kala ela za Rostam,Mkono na CCM wanasema sio kosa!

Alafu bora angepeleka kwenye chama na kusema ni MSAADA kutoka CCM kwaajili ya kujiandaa na uchaguzi,yeye kaenda KUKOPESHA chama kwa RIBA kubwa na kufungua gazeti binafsi!

Huyu mtu hatufai.
 
MOSES MACHALI.
"Hayo hapo chini ndiyo maneno aliyoyasema kupitia mtandao wa kijamii, jisomee ujue anachokisema na majibu ujipe mwenyewe>>>>"

Moses Machali
Kuna watu wanazungumzia nidhamu na kwamba ili mtu uweze kufanikiwa maisha ni lazima uwe na nidhamu. Nami nakubaliana na kauli hiyo, lakini tunapaswa kujiuliza ni nidhamu ya aina gani?

Inawezekana mtu akasema ZITTO hana nidhamu kwa chama chake lakini ikawa ni kinyume chake. Hii ni kwa sababu hana nguvu za kufanya maamuzi ndani ya chama na kwa hiyo akawa anatakiwa kutii mambo ambayo yako kinyume cha utaratibu wa chama chake lakini kwa kuwa yanatolewa na kusimamiwa na watu wenye nguvu basi akipinga anaonekana hana nidhamu. Binafsi niseme moja tu kwamba, wakati mwingine sisi wanasiasa tunakurupuka na kukosea.

Katika sakata la zitto na CDM nadhani pande zote zinaweza kuwa na makosa kwa kuwa hadi mambo yamefikia hapo yalipofika ni kwa sababu kumekosekana collective responsibilty na imekosekana pia nidhamu ya kiuongozi inavyoonekana kwa kuwa hata akina Mbowe; Dr. SLAA na wengine siyo malaika wakati mwingine nao hukosea tena sana.

Na kwa hiyo napingana na wale wote wanaosema mkosefu ni Zitto tu la hasha ni uonevu kwa upande mmoja.

Lakini pia napingana na wale wote wanaosema Zitto anaonewa tu la hasha inawezekana kweli kukawa kuna makosa tofauti na historia tunayoifahamu wachache. Ngoja niwakumbushe kidogo wana jamvi: Mwaka 2009 wakati wa uchaguzi ndani ya CDM uliibuka mgogoro kati kundi la Mbowe na kundi la Zitto ambapo wazee wa chama wakamtaka Zitto aache kugombea uenyekiti wa chama kwa kuwa yeye ni kijana bado ana muda mwingi na kwamba anaweza kugombea wakati mwingine na kwa hiyo amwachie mbowe kwanza akiongoze chama.

Finally Zitto alijiondoa kwa shingo upande yaani pasipo kupenda na wafuasi wengine wa Zitto wakakutana na majanga mazito ndani ya CDM na wakaamua kuondoka CDM wakaitwa majina ya kwamba wao ni sisimizi nk; wakati mwingine wakaitwa Wasaliti na watu wenye njaa nk. Waliopatwa na kadhia hiyo baadhi ni hawa wafuatao: mhe. david KAFULILA(MB), MARTINE DANDA kutoka Iringa.

Wengine ni akina Mhe. Mkosamali(mb) pamoja nami Machali(mb) na baadaye kabisa waliondoka akina Mama Msole nwengineo. Wapo wadau wasemao kwamba huenda mgogoro uliopo hivi sasa unatokana na kile kilichotokea 2009 kwa kuwa CDM walipaswa kufanya uchaguzi lakini wakaahirisha kwa kile kinachosema kwamba watamwambia nini Mhe. Zitto mwaka huu katika kugombea Uenyekiti wa chama kama ilivyo dhamira yake ya siku nyingi ya kukiongoza CDM.

INASEMEKANA kwamba baadhi ya viongozi wa CDM wenye nguvu ndani ya chama wametafakari ni namna gani Zitto hapenyi katika kinyanganyiro cha uchaguzi ikaonekana ni ngumu sana na kwamba inabidi kuangalia namna ya kufanya na huenda ndiyo haya tunayoyaona sasa. Aidha Ikumbukwe kuwa kuna nyakati vyombo vya habari vilimnukuu Mhe. Mbowe akisema kwamba Dr. Slaa ndiye atakaechukua fomu za kugombea Urais na kwamba yeye hatagombea tena(Mbowe), Lakini Zitto amekuwa akitangaza nia ya kugombea Urais anakutana na vikwazo au mikwara mingi kutoka kwa baadhi ya viongozi na wanachama wa CDM. Na baadhi ya vyombo vya habari vilipata kumnukuu Mzee Mtei akimshauri Mhe. Zitto kuachana na masuala ya kutangaza nia ya kuombea urais kwamba ni kusababisha fujo au vurugu ndani ya CDM na kwamba atulie hadi wakati ukifika.

Tujiulize mimi na wewe, inakuaje Zitto akitangaza nia iwe kosa lakini Mbowe akitangaza nia iwe ni sawa wakati kwa mujibu wa katiba ya CDM kuna mamlaka inayotakiwa kumtangaza mgombea urais ni nani lakini pia sidhani kama kuna mahala katiba ya CDM inakataza Mwanachama wake kutangaza nia ya kugombea nafasi fulani kama vile urais.

Kama kuna kipengele hicho CDM wanapaswa kukionesha ili kuondoa mashaka yaliyopo juu ya kwamba wanamuonea Mhe. Zitto. Hata hivyo wapo wanachama wengi wametangaza nia kugombea Ubunge ndani ya CDM mwaka 2015 kama ilivyokuwa kwetu sisi kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010; tulitangaza nia sana tu; wote akina Wenje, akina HAINESS KIWIA na wengine na hawakuelezwa kwamba wanaleta fujo ndani ya CDM.

Ndugu zangu ndiyo maana ninakuwa na mashaka wakati mwingine kwa kusema kwamba huenda kweli Mhe. Zitto akawa anaonewa kama anavyosema, mtazamo huu unatokana na records hizo za nyuma. CDM wajitokeze kufafanua hoja hizo ili nasi makomredi wao kimkakakti tuweze ku clear dout. Inawezekana baadhi wakaja na maneno maneno yaliyozoeleka kwamba nimetumwa na Zitto nk.
La hasha ni utashi wangu tu kutokana na uzoefu wangu katika siasa za CDM na sasa niko NCCR-Mageuzi. Uzoefu wangu usibezwe kwa kuwa ninayo
Email This
BlogThis!
Share to Twitter
Share to Facebook
at 1/05/2014 03:10:00 AM


Well Said,

Thanks
 
Ni yamkini kuwa, waliopo hatuwataki na wanaotubembeleza tuwapokee hatuwaamini kabisaaa.....wanasiasa wote ni wachumia tumbo, kama mtaani tuanze tu kwenda wenyewe.
 
Ngoja Lowassa nae ataje alio wapatia pesa ndani ya chadema tuone nani atabaki....
 
Eti sababu ya kupewa pesa na Kikwete na CCM ni kwaajili ya kwenda kukikopesha chama

Shame on him
 
wote ni wajisiriamali tu wanatumia siasa kama mtaji
 
Pamoja na mihela yote na viwanja/majumba/hoteli ulizorithi kwa baba yako lakini
bado unapokea vijisenti vya CCM???? Si mnazihiita ni pesa chafu refer 'List of shame'

Sasa mimi ambae ni kijana nina kadi ya chadema sina kazi, kwetu hakuna mali, nimesoma
sina kazi nitaziacha kweli hizo PESA za CCM zikija nje nje????

wao wanapokea halafu wanakwambia wewe usipokee , kura uwape wao, umeona wapi kitu kama hicho??
 
Sabodo ni mwanaCCM mzuri sana na ametoa pesa mara nyingi tena hadharani kuunga mkono harakati za CHADEMA.

Kwangu mimi hili ni jambo la kawaida sana.
 
Back
Top Bottom