Zitto acha kutafuta kiki, mbona hukushitaki hao washirika wako CCM leo unashoboka?

Zitto acha kutafuta kiki, mbona hukushitaki hao washirika wako CCM leo unashoboka?

Lakini tuulizane na tuambizane ukweli.
Wewe unaamini Serikali inaweza kumiliki wadunguaji wa aina Ile?
Kwa akili za serikali ile ya awamu ya tano? Mbona hilo sio la kujiuliza
Ila hata kama tuki assume sio wao, mbona hakukamatwa mtu hata mmoja kuhusiana na hilo tukio licha ya kufanyika kwenye maeneo yenye ulinzi mkali na kukamatwa kwenye CCTV Camera ambazo zilitolewa na kufichwa?
 
Hako ni kakikundi ambacho sio kinatafuta haki bali visasi vyao. Kuna watu wamelengwa, wanasahau awamu ya 5 kafa mtu mmoja tu! System nzima ni ile ile zaidi ya ku change positions.

Maloto katangulizwa kama kawaida. Watu wanawachora tu.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Kwani mnachoogopa ni nini? Si kwamba serikali ya Magufuli haihusiki na hayo yote bali ni Chadema ndio walikuwa wakifanya kuichafua serikali? Huyu jamaa anataka ku expose huo uhuni wa Chadema
 
Haihusiki mzee
Kwani mnachoogopa ni nini? Si kwamba serikali ya Magufuli haihusiki na hayo yote bali ni Chadema ndio walikuwa wakifanya kuichafua serikali? Huyu jamaa anataka ku expose huo uhuni wa Chadema
 
Hatua aliyochukua Luqman Maloto ni ya kupongezwa.

Naona wachangiaji wengi hapa mnaongea ki-kijiwekijiwe na wengine kwa uoga uoga. Lakini jambo alilofanya Luqman ni jambo zuri sana, maana matukio ya watu wasiojulikana yakiachwa bila ya kushughulikiwa ni hatari sana kwa mustakabali wa taifa, hususani katika ujenzi wa taifa la kistaarabu.

Ustaarabu ni kutambua kuwa hakuna aliye juu ya sheria.

Ustaarabu ni kutambua kwamba ni marufuku kumuadhibu au kumchukulia hatua mtu yeyote nje ya mahakama. Hata serikali inatakiwa watu wote inaowaona wanafanya makosa iwashtaki mahakamani na kuacha sheria ichukue mkondo wake.

Kwa hiyo masuala ya watu ambao walikuwa wanamkosoa Rais kukutwa na matukio ambayo serikali iliyakalia kimya na kutofanya upelelezi wa kutosha hayatakiwi kabisa katika jamii ya kistaarabu.

Suala la mamlaka zinazohusika kutofanya upelelezi wa kutosha kuwakamata wahusika ndiyo linajenga taswira kwamba serikali inahusika na huo utekaji.

Hivyo shauri hili alilofungua Maloto ni shauri jema sana, na limekuja kwa wakati sahihi. Shauri hili linaweza kuwa urithi (legacy) wa muhimu zaidi wa utawala wa Mama Samia Suluhu Hassan.
 
Zitto anajua Samia alikuwa Makamu wa Rais na anawajibika?
Pengine ndiyo njia ya kumkwamisha!
Nimewaza tu, watu wamekaa ki maslahi slahi tu hakuna cha uzalendo wala cha nini...Kila chenye kuwaletea personal gains wanakichukua kama agenda ya ki taifa....They have no permanent friends neither agendas but interests!
 
Nimefurahi sana leo chama changu kinaonyesha mwanga angalau wa tunakoelekea...May God bless our country, give wisdom and understanfing to our dear Jemedari Mkuu HE Dr. Samia Suluhu Hassan

Niseme tu kwa dhati ya moyo, katika kuijenga democracy mama ame fanya vizuri...Hatua ya pili ni kutimiza kwa vitendo utawala bora kwaku imarisha vyombo vya maamuzi, sheria na utekelezaji...Hili litawezekana tu kama tutakubali kuileta Katiba mpya itakayo punguza nguvu za individuals, kuongeza nguvu ya umma ili kupunguza unafiki na kujuana ili sasa merits ndizo ziwe determinants...Lakini pia kuwe na affirmative measures maana kuna watu CV zao zilivurugwa au kukwamishwa na ni wazuri na kuna wengine ambao CV zao zime bumbwa huku wakiwa hawana contents...Kuwe na scrutiny ya hali ya juu ku peruse CVs za elite class wote na kujua wapi ni pumba na wapi ni mchele kisha kuruhusu vipaji vijionyeshe tuisaidie nchi yetu na kuileta katika ramani ya dunia....
 
Pengine ndiyo njia ya kumkwamisha!
Nimewaza tu, watu wamekaa ki maslahi slahi tu hakuna cha uzalendo wala cha nini...Kila chenye kuwaletea personal gains wanakichukua kama agenda ya ki taifa....They have no permanent friends neither agendas but interests!
Wacha inyeshe tujue panapovuja
 
Nimefurahi sana leo chama changu kinaonyesha mwanga angalau wa tunakoelekea...May God bless pur country, give wisdom and understanfing to our dear Jemeddari Mkuu HE Dr. Samia Suluhu Hassan

Niseme tu kwa dhati ya moyo, katika kuijenga democracy mama ame fanya vizuri...Hatua ya pili ni kutimiza kwa vitendo utawala bora kwaku imarisha vyombo vya maamuzi, sheria na utekelezaji...Hili litawezekana tu kama titakubali kuileta Katiba mpya itakayo punguza nguvu za individuals, kuongeza nguvu ya umma ili kupunguza unafiki na kujuana ili sasa merits ndizo ziwe determinants...Lakini pia kuwe na affirmative measures maana kuna watu CV zao zilivurugwa au kukwamishwa na ni wazuri na kuna wengine ambao CV zao zime bumbwa huku wakiwa hawana contents...Kuwe na scrutiny ya hali ya juu ku peruse CVs za elite class wote na kujua wapi ni pumba na wapi ni mchele kisha kuruhusu vipaji vijionyeshe tuisaidie nchi yetu na kuileta katika ramani ya dunia....
Perfect👍
 
Hatua aliyochukua Luqman Maloto ni ya kupongezwa.

Naona wachangiaji wengi hapa mnaongea ki-kijiwekijiwe na wengine kwa uoga uoga. Lakini jambo alilofanya Luqman ni jambo zuri sana, maana matukio ya watu wasiojulikana yakiachwa bila ya kushughulikiwa ni hatari sana kwa mustakabali wa taifa, hususani katika ujenzi wa taifa la kistaarabu.

Ustaarabu ni kutambua kuwa hakuna aliye juu ya sheria.

Ustaarabu ni kutambua kwamba ni marufuku kumuadhibu au kumchukulia hatua mtu yeyote nje ya mahakama. Hata serikali inatakiwa watu wote inaowaona wanafanya makosa iwashtaki mahakamani na kuacha sheria ichukue mkondo wake.

Kwa hiyo masuala ya watu ambao walikuwa wanamkosoa Rais kukutwa na matukio ambayo serikali iliyakalia kimya na kutofanya upelelezi wa kutosha hayatakiwi kabisa katika jamii ya kistaarabu.

Suala la mamlaka zinazohusika kutofanya upelelezi wa kutosha kuwakamata wahusika ndiyo linajenga taswira kwamba serikali inahusika na huo utekaji.

Hivyo shauri hili alilofungua Maloto ni shauri jema sana, na limekuja kwa wakati sahihi. Shauri hili linaweza kuwa urithi (legacy) wa muhimu zaidi wa utawala wa Mama Samia Suluhu Hassan.
Naunga mkono. Kesi kufika tu mezani kwa Mahakama hata kama haitafika mwisho ni ushindi
 
Ujweli halisi,na huyo liquiman hiyo inaweza kuwa bahasha ambayo itamgharimu sana!
Mkuu sasa woga wako ni nini? Kwamba unamuonea huruma Lukmani wewe?? Hiyo huruma umeanza tangu lini?
 
Hako ni kakikundi ambacho sio kinatafuta haki bali visasi vyao. Kuna watu wamelengwa, wanasahau awamu ya 5 kafa mtu mmoja tu! System nzima ni ile ile zaidi ya ku change positions.

Maloto katangulizwa kama kawaida. Watu wanawachora tu.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Wasi wasi wako ni nini? Au na wewe ni mtuhumiwa?
 
Samia hakwepi hili jambo.

Kwakuwa makamu wa Rais wa Magufuli.

Anahusika 100% kwa kila jambo alilofanya Magufuli kama msaidizi wake namba moja.
 
Si utulie tu, au unaogopa kusikia ukweli utakao kuumiza?
Nimefundishwa kusimama na ukweli na nikiumizwa na ukweli maana yake nimegeuka kuwa heretic. Sasa kuamini tofauti na wewe usifikiri ni kupotoka hadi pale ukweli utapojifunua.

Ubaya haya mambo hayaishagi, siku moja hawa hawa wataanza tena kulialia! Unfortunately inaweza kuwa worse!

Siasa kama huchanganyi na zako ndio yanayomtokea Musiba! Hakujua itatokea siku kama hizi! Hao vijana pia hawajajifunza maana hawasukumwi na haki! Moja ya sifa ya haki hukata kuwili kama upanga. Wanaweza kukata kuwili hawa? Yetu macho!

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Mnaleta tabia ya kufunga watu midomo kwasababu za kimahaba kwa wale muwapendao, upande wa pili nao wakiguswa kwa maoni wanayoona yanamkera mama yao nao wanasema fulani amenunuliwa, hii sio sawa.

Hii tabia ya kukwepa uwajibikaji na kuingilia uhuru wa wengine kutoa maoni yao ikomeshwe, ila kama mna ushahidi fulani amenunuliwa mnakaribishwa kuuweka hadharani, ili tusitengeneze taifa la waoga na walalamikaji.
Kuwajibika? Tunataka uwajibikaji? Au tunachagua wa kuwajibika? Hili jukwaa siku hizi gumu sana. Basi tusubiri hiyo kesi tuone .....

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom