Zitto acha kutafuta kiki, mbona hukushitaki hao washirika wako CCM leo unashoboka?

Zitto acha kutafuta kiki, mbona hukushitaki hao washirika wako CCM leo unashoboka?

Hako ni kakikundi ambacho sio kinatafuta haki bali visasi vyao. Kuna watu wamelengwa, wanasahau awamu ya 5 kafa mtu mmoja tu! System nzima ni ile ile zaidi ya ku change positions.

Maloto katangulizwa kama kawaida. Watu wanawachora tu.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Hakika nchi hii iliharibiwa sana katika miaka michache iliyopita! Hivi, mstari wa kutenganisha kutafuta haki na kulipiza kisasi unachorwa wapi? Hivi kweli kutaka kujua ni kwanini uhalifu wa raia kutekwa, kuumizwa, kupotea na kuuawa haujafuatiliwa na vyombo vyenye dhamana hiyo ni kulipiza kisasi? Kwa hakika "kakikundi" siyo hawa wanaotafuta majibu ya udhalimu uliotendeka awamu ya tano bali ni wale walioasisi na kutenda udhalimu huo. Kwa mambo yale ya kutisha tusingetarajia raia mwema wa nchi hii kubeza na hata kutilia shaka mawazo ya raia wenzake ya kutaka kupata majibu kutoka kwa watu wenye dhamana kikatiba na kishearia. Mtu mwovu hutamani kuaminisha umma kuwa uovu ule ulikuwa na baraka za uongozi wote wa awamu hiyo! Jambo hilo siyo kweli hata kidogo. Uovu huo uliasisiwa na kutekelezwa na watu wachache sana tena waliokuwa wakifanya kazi hiyo nje ya mifumo rasmi ya uendeshaji wa nchi. Hawa wanaobeza jitihada za kupata majibu kutoka kwa wahusika ama ni wanufaika au watekelezaji wa uovu huo. Haiwezekani hata kidogo kuwa udhalimu huo ulifanyika kutokana na maamuzi ya vikao rasmi vya kiserikali au vyombo vya ulinzi na usalama.
 
Hamsemi labda anajua kilichokuwa kinaendelea kwenye serikali iliyopita ,maana jiwe alijitanabaisha ni "Serikali yangu ya Magufuli" means ilikuwa one-man show.
Sasa kwa nini Samia alikubali kukaa kwenye serikali ya one man show?

Unajua ukishakubali kukaa kwenye serikali ya one man show unawajibika kwa maamuzi ya seriklai hiyo?

Unaelewa Nuremberg Trials ni nini na ilitoa hukumu gani kuhusu wanajeshi na wanachama wa wa Nazi waliohukumiwa kwa kushiriki kwenye mauaji ya Wayahudi na kutoa utetezi wa kwamba wao walifanya kwa "maagizo kutoka juu" tu?
 
Sasa kwa nini Samia alikubali kukaa kwenye serikali ya one man show?
Ki protocol ni ngumu kuondoka maana ingeleta sintofahamu ,ilibidi afe kisabuni hadi mwisho.
Unajua ukishakubali kukaa kwenye serikali ya one man show unawajibika kwa maamuzi ya seriklai hiyo?

Yes kiuhalisia inabidi uwajibike ,kwakuwa wao wanalijua hilo ndiyo maana walijiwekea KINGA ili wasiingie kwenye "kuwajibika".
Unaelewa Nuremberg Trials ni nini na ilitoa hukumu gani kuhusu wanajeshi na wanachama wa wa Nazi waliohukumiwa kwa kushiriki kwenye mauaji ya Wayahudi na kutoa utetezi wa kwamba wao walifanya kwa "maagizo kutoka juu" tu?

Hata huku kwetu haikubaliki ,kama ulishiriki wewe kama wewe hata kama ulipewa maagizo kutoka juu lazima ile kwako uliyetenda na si aliyeagiza , Hii ni kama kesi ya Zombe kutoa maagizo wafanyabiashara wa madini wakauawe mabwepande ,askari alijitetea kwamba aliagizwa na Zombe,pia zombe na yeye akajitetea kwamba yeye hajashika mtutu na kuua ,kwahiyo Zombe akachomoka.
 
😁😁😁
EAAZV.jpeg
 
Ki protocol ni ngumu kuondoka maana ingeleta sintofahamu ,ilibidi afe kisabuni hadi mwisho.

Yes kiuhalisia inabidi uwajibike ,kwakuwa wao wanalijua hilo ndiyo maana walijiwekea KINGA ili wasiingie kwenye "kuwajibika".

Hata huku kwetu haikubaliki ,kama ulishiriki wewe kama wewe hata kama ulipewa maagizo kutoka juu lazima ile kwako uliyetenda na si aliyeagiza , Hii ni kama kesi ya Zombe kutoa maagizo wafanyabiashara wa madini wakauawe mabwepande ,askari alijitetea kwamba aliagizwa na Zombe,pia zombe na yeye akajitetea kwamba yeye hajashika mtutu na kuua ,kwahiyo Zombe akachomoka.
Ukichunguza sana utaona hizi ni cheap politics tu. Zitto hataki kumuwajibisha Samia, japo kisiasa tu, kama kisheria haiwezekani.

Kwa sababu anaangalia maslahi yake zaidi kuliko kuangalia principles.

Tangu Samia achukue urais, sijawahi kumsikia Zitto akimsema vibaya Samia hata mara moja.
 
kwa katiba yetu rais ndio kila kitu,makamo ni kuvuli tu,sijui kwa nchi nyingine
Kama kivuli tu angejiuzulu, makamu wa rais ni mtu wa pili kwenye madaraka, ndiyo maana aliofariki Magufuli, Samia kachukua urais.

Hizi habari z akusema "makamu wa rais ni kivuli tu" ndiyo zimewapiga watu daflao walipoona Samia anaenda kushika urais baada ya kufa Magufuli.

Wao waliona wanamuweka kama kivuli tu, wakati katiba inasema akifariki rais Makamu ndiye anashika urais, rais akiwa nje mara nyingi makamu anakaimu urais.

Na hata kama ni kivuli, it doesn't matter. Ukishakubali kuwa makamu wa rais kivuli katika serikali inayoua watu, na wewe unawajibika katika mauaji hayo. Ukisema mimi nilikuwa kivuli tu, huo si utetezi, hapo umekubali kosa.

Hii ndiyo ile ile habari ya The Nuremberg Trials ya wanajeshi waliojitetea kwamba "sisi tuliua kwa kupokea amri kutoka juu tu". Ukikubali amri kutoka juu ya kuua watu, ukajitetea kwamba mimi nilikuwa kivuli tu, kapuku tu, foot soldier tu, na wewe unawajibika kwa mauaji hayo.

Sasa Zitto mbona hamsemi rais wa sasa na anafanya kama nchi imebadilisha chama na uongozi wakati rais wa sasa alikuwa makamu wa rais wa Magufuli?
 
Lakini tuulizane na tuambizane ukweli.
Wewe unaamini Serikali inaweza kumiliki wadunguaji wa aina Ile?
Ndiyo. Kwa hizi ajira za kujuana inawezekana sana.

Tuombe Mungu Kagame asije kutuvamia kama alivyoivamia Kongo.
 
Zitto ni mnafiki, ndumilakuwili na mzandiki wa kutupa! hana chembe ya upinzani zaidi ya maslahi binafsi ya tumbo lake!
 
Lakini tuulizane na tuambizane ukweli.
Wewe unaamini Serikali inaweza kumiliki wadunguaji wa aina Ile?
Ficha ujinga wako .Ni Mungu tu aliamua Tundu Lissu aishi .Hata kama wengi kuwa watunguaji Mahiri kiasi gani ,Mungu akiamua uishi utaishi.
 
Kama kivuli tu angejiuzulu, makamu wa rais ni mtu wa pili kwenye madaraka, ndiyo maana aliofariki Magufuli, Samia kachukua urais.

Hizi habari z akusema "makamu wa rais ni kivuli tu" ndiyo zimewapiga watu daflao walipoona Samia anaenda kushika urais baada ya kufa Magufuli.

Wao waliona wanamuweka kama kivuli tu, wakati katiba inasema akifariki rais Makamu ndiye anashika urais, rais akiwa nje mara nyingi makamu anakaimu urais.

Na hata kama ni kivuli, it doesn't matter. Ukishakubali kuwa makamu wa rais kivuli katika serikali inayoua watu, na wewe unawajibika katika mauaji hayo. Ukisema mimi nilikuwa kivuli tu, huo si utetezi, hapo umekubali kosa.

Hii ndiyo ile ile habari ya The Nuremberg Trials ya wanajeshi waliojitetea kwamba "sisi tuliua kwa kupokea amri kutoka juu tu". Ukikubali amri kutoka juu ya kuua watu, ukajitetea kwamba mimi nilikuwa kivuli tu, kapuku tu, foot soldier tu, na wewe unawajibika kwa mauaji hayo.

Sasa Zitto mbona hamsemi rais wa sasa na anafanya kama nchi imebadilisha chama na uongozi wakati rais wa sasa alikuwa makamu wa rais wa Magufuli?
we jamaa una akili nyingi ila hapa umepunyanga ,mifano yako yote uliyootoa hapa haiendani na nilichoandika.Mimi nimesema kwa katiba tuliyonayo makamo wa raisi ni kivuli,wewe badala ya kujibu hiyo hoja ili tujue ni kivuli kivipi wewe uansema angejiuzulu,sasa akijiuzulu si anachaguliwa mwingine halafu yanakua yaleyale,kwani wewe hujui kwamba makamo wa rais kwenye nchi yetu ni mkata utepe tu bora waziri mkuu ana nguvu kumliko.pili unasema eti sio kivuli kwakuwa akifariki rais yeye ndio anakamata mamlaka ,sasa hapo si mpaka afe,sisi hatuongelea rais akifa maana kwa nchi yetu hatujazoea rais kufa au kuuawa madarakani ndio maana makamo anawekwa yoyote yule ila kwa yaliyotokea sysytem zitakua zimejifunza.pia sijasema eti katika serikali iliyouwa watu makamo atajitetea sehemu kwamba mimi nilikua kivuli ,maana hakuna sehemu yeye anateuliwa na kuambiwa wewe ni kivuli,pia wala hakuna hiyo kesi kwamba rais aliyekuwepo kafanya mauaji anakamatwa mamako kwa kuwa serikali ni moja sio kweli.huo mfano wa wanajeshi sio relevant maana wanajenshi hao ndio walioshika bundukio kwenda kuua so hawawezi kusema eti tulipokea maagizo wakati wao ndio wameenda kuua mtu(fatilia kesi yaa zombe na sabaya) rais wa sasa ni rais ana nguvu zote ila kipindi alivyokua makamo alikua kama housegirl tu hata wakina tundulisu wanapigwa risasi bora makonda alikua na taarifa zote kuliko huyo makamo.so kwa katiba ya nchi yetu usikatae tupambane tupate katiba mpya
 
Zito anajua mengi sana
😀😀😀😀 eti anajua mengi sana. Kama unamaanisha kweli basi wewe utakuwa kati ya watu ambao IQ zao ni -ve 10. Mimi ninachomkubali Zito ni jinsi alivyo Bingwa wa kucheza na vichwa vya watu wajinga kwa kutengeneza scenario za kuwaaminisha watu. Na katika hili amefanikiwa kiasi chake.

Pia jamaa ni fundi hasa wa mipango. Jamaa alipoona Maalim Seif(R.I.P) ameshazeeka na afya yake haipo vema , haraka jamaa akazidisha ukaribu na Cuf ya Seifu kisha kukubaliana kujiunga ACT.

Ninachokiona jamaa alicheza na nyakati kwani kwa jinsi Seif alivyokuwa akiaminika kwa wafuasi wake basi hata kwa kuondoka kwake itakuwa ngumu wafuasi hao kuwaambia waondoke ACT. Hawatataka kumsaliti Seif na hiyo kwao ni kama usia.

Sasahivi jamaa huko znz ni mtu na nusu.

Ndio maana nasema Zitto ni Kichwa sana
 
Hako ni kakikundi ambacho sio kinatafuta haki bali visasi vyao. Kuna watu wamelengwa, wanasahau awamu ya 5 kafa mtu mmoja tu! System nzima ni ile ile zaidi ya ku change positions.

Maloto katangulizwa kama kawaida. Watu wanawachora tu.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Kwa hiyo wewe unaona wote wakalishe matako kama wewe unayeota moto kwenye jua kali. Amka kwani wewe huumii wenzako wanapoteswa na kupotezwa?!
 
we jamaa una akili nyingi ila hapa umepunyanga ,mifano yako yote uliyootoa hapa haiendani na nilichoandika.Mimi nimesema kwa katiba tuliyonayo makamo wa raisi ni kivuli,wewe badala ya kujibu hiyo hoja ili tujue ni kivuli kivipi wewe uansema angejiuzulu,sasa akijiuzulu si anachaguliwa mwingine halafu yanakua yaleyale,kwani wewe hujui kwamba makamo wa rais kwenye nchi yetu ni mkata utepe tu bora waziri mkuu ana nguvu kumliko.pili unasema eti sio kivuli kwakuwa akifariki rais yeye ndio anakamata mamlaka ,sasa hapo si mpaka afe,sisi hatuongelea rais akifa maana kwa nchi yetu hatujazoea rais kufa au kuuawa madarakani ndio maana makamo anawekwa yoyote yule ila kwa yaliyotokea sysytem zitakua zimejifunza.pia sijasema eti katika serikali iliyouwa watu makamo atajitetea sehemu kwamba mimi nilikua kivuli ,maana hakuna sehemu yeye anateuliwa na kuambiwa wewe ni kivuli,pia wala hakuna hiyo kesi kwamba rais aliyekuwepo kafanya mauaji anakamatwa mamako kwa kuwa serikali ni moja sio kweli.huo mfano wa wanajeshi sio relevant maana wanajenshi hao ndio walioshika bundukio kwenda kuua so hawawezi kusema eti tulipokea maagizo wakati wao ndio wameenda kuua mtu(fatilia kesi yaa zombe na sabaya) rais wa sasa ni rais ana nguvu zote ila kipindi alivyokua makamo alikua kama housegirl tu hata wakina tundulisu wanapigwa risasi bora makonda alikua na taarifa zote kuliko huyo makamo.so kwa katiba ya nchi yetu usikatae tupambane tupate katiba mpya
Kwanza kabisa naomba uondoe hiyo dhana ya "we jamaa una akili sana...", itavuruga mjadala tu.

Nimekwambia kwamba hata kama kwa katiba ni kivuli, hiyo hoja ni moot kwa sababu kwa logic ya The Nuremberg Trials, hata ukiwa kivuli tu, lakini ukikubaliana na amri kutoka juu, unawajibika.

Nimekuwekea mpaka link ya The Nuremberg Trials, nikailelezea.

Sasa usichoelewa ni nini hapo?

Nimekwambia kwamba, hoja ya "Makamu wa Rais ni kivuli tu" ni sawa na hoja ya mwanajeshi mwenye cheo kidogo sana anayeamrishwa kuua na mkubwa wake, akashiriki kwenye mauaji, halafu katika utetezi akasema "mimi nilikuwa mwanajeshi mdogo tu, nimefanya mambo kwa kupokea amri kutoka juu"

Guess what, kusema hivyo si utetezi, udogo wako katika organization haukupi kinga kama umeyakubali maagizo na kuyatekeleza.

Umakamu wa Rais wa Samia kuwa kivuli (which is not true, kwa sababu Makamu wa Rais anamrithi rais, anakaimu nafasi ya ras etc, lakini tuseme ni kivuli for the sake of argument), so hata kama Makamu wa Rais ni kivuli, kuwa kivuli hakumpi kinga kwenye matendo yaliyotendwa na serikali yake, as long as alikuwa sehemu ya uongozi wa juu wa serikali hiyo.

Sasa hapo huoni kwamba utetezi wa "Samia alikuwa kivuli tu" ni sawa na utetezi wa kusema "mimi nilikuwa koplo tu jeshini, sikuamua mauaji yatokee" wakati mauaji yametokea na wewe umeya endorse kwa kubaki jeshini hata hujajiuzulu useme sitaki kushirikishwa na mauaji haya? Tena umetoa kauli za kashfa kusema askari wetu hawakosi?

Unamtetea Samia katika jambo ambalo hawezi kutetewa kimantiki.

Samia alijua mauaji yanatokea, alikuwa katika uongozi wa serikali iliyoshiriki moja kwa moja au kuzembea na kuruhusu mauaji hayo, hivyo, anawajibika.

Ukitaka kumbeba kw amahaba binafsi sawa, mebebe, lakini kimantiki anahusika.
 
Makamu wa Rais kazi zake ni mazingira, mambo ya muungano na kuzindua zindua tu.
Hawajibiki kwa mambo ya boss wake.
Zitto anajua Samia alikuwa Makamu wa Rais na anawajibika?
 
Makamu wa Rais mambo yake ni masuala ya mazingira, muungano na uzinduzi.
Hahusiki kwa 100% na kila jambo la mkuu wake.
Samia hakwepi hili jambo.

Kwakuwa makamu wa Rais wa Magufuli.

Anahusika 100% kwa kila jambo alilofanya Magufuli kama msaidizi wake namba moja.
 
Makamu wa Rais kazi zake ni mazingira, mambo ya muungano na kuzindua zindua tu.
Hawajibiki kwa mambo ya boss wake.
Tusidanganyane, katiba iko hapa

SEHEMU YA PILI

MAKAMU WA RAIS

Mkamu mmoja wa Rais, kazi na mamlaka yake Sheria ya 1994 Na.34 ib.11
Sheria ya 2000 Na.3 ib.9 47.-
(1) Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa ndiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano kwa jumla, na hususan-
(a) atamsaidia Rais katika kufuatilia utekelezaji wa siku hata siku za Mambo ya Muungano;
(b) atafanya kazi zote atakazoagizwa na Rais;
(c) atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi.

(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 37(5), Makamu wa Rais atapatikana kwa kuchaguliwa katika uchaguzi ule ule kwa pamoja na Rais, baada ya kupendekezwa na chama chake wakati ule ule anapopendekezwa mgombea kiti cha Rais na watapigiwa kura kwa pamoja. Mgombea kiti cha Rais akichaguliwa basi na Mahakmu wa Rais atakuwa amechaguliwa.

(3) Mtu atateuliwa kugombea kiti cha Makamu wa Rais kwa kufuata kanuni kwamba endapo Rais wa Jamhuri ya Muungano atatoka sehemu moja ya Muungano, basi Makamu wa Rais atakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano
 
Back
Top Bottom