Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Sio Wanazi wote walihukumiwa katika Nuremberg trials. Waliohukumiwa ni waliohusika na mauaji. Kuna watu katika utawala wa Hitler walijaribu hadi kumuua.
Kama kivuli tu angejiuzulu, makamu wa rais ni mtu wa pili kwenye madaraka, ndiyo maana aliofariki Magufuli, Samia kachukua urais.
Hizi habari z akusema "makamu wa rais ni kivuli tu" ndiyo zimewapiga watu daflao walipoona Samia anaenda kushika urais baada ya kufa Magufuli.
Wao waliona wanamuweka kama kivuli tu, wakati katiba inasema akifariki rais Makamu ndiye anashika urais, rais akiwa nje mara nyingi makamu anakaimu urais.
Na hata kama ni kivuli, it doesn't matter. Ukishakubali kuwa makamu wa rais kivuli katika serikali inayoua watu, na wewe unawajibika katika mauaji hayo. Ukisema mimi nilikuwa kivuli tu, huo si utetezi, hapo umekubali kosa.
Hii ndiyo ile ile habari ya The Nuremberg Trials ya wanajeshi waliojitetea kwamba "sisi tuliua kwa kupokea amri kutoka juu tu". Ukikubali amri kutoka juu ya kuua watu, ukajitetea kwamba mimi nilikuwa kivuli tu, kapuku tu, foot soldier tu, na wewe unawajibika kwa mauaji hayo.
Sasa Zitto mbona hamsemi rais wa sasa na anafanya kama nchi imebadilisha chama na uongozi wakati rais wa sasa alikuwa makamu wa rais wa Magufuli?