Kwa tafsiri ya neno msukule ambayo ni binadamu aliyetolewa ufahamu na kuwekwa mafichoni ili kutumika kufanikisha majukumu fulani fulani, ni wazi kuwa pana haja sasa ya kupanua wigo kuwaongeza humo wengi tu na wa aina hiyo tofauti ikiwa tu hawa wengine kutokuwa mafichoni. Ninasema hivi kwa sababu hizi:
1. Watanzania wameambiwa kuwa uchaguzi mkuu 2020 uko pale pale. Pana idadi kubwa ya walioaminishwa hilo na hivi sasa wako kwenye maandalizi kabambe ya kuelekea kutia nia.
2. Wameambiwa mzee baba yuko kwenye kutathmini kuachia ligi kuu na michezo mingine kuendelea. Pana idadi yao kubwa yao ambao wameaminishwa hilo pia na hivi sasa wako kwenye maandalizi kabambe kuanza mazoezi kujiwinda na ubingwa mara tu ruhusa itakapotolewa.
Yako mengi achilia mbali ya kuaminishwa kuwa:
4. hakuna takwimu mpya kuhusiana na Corona nchini tokea Apr 29.
5. vifo vya kushangaza tunavyoshudia ni vya kawaida tu na kwanza eti ni vichache tu,
6. vita vya Corona tumeshashinda,
7.wenzetu waliochukua hatua hali ni mbaya kuliko sisi
8. Huu ugonjwa ni kaupepo, kasikosioathiri waafrika wala kuwa na madhara kwenye nchi za joto,
9. Nk, nk.
Hii ni bila kujali hali ya ugonjwa inapungua au la, na hakuna dalili zipi za ugonjwa huu wenye kuuwa saba, angalau lini au vipi utadhibitiwa.
Uwezo wa watu hawa kufikiria nao uwezo unafikirisha. Kwa kutoweza kustahimili hoja, midomo yao imewajaa matusi yasiyo mithilika na kejeli zisizokuwa ba mbele wala nyuma na wala mashiko yoyote.
Ama kweli misukule haiko madarini mwa manyumba peke yake, bali hata barabarani na sasa ipo hadi jf ikiwa na ID genuine na hali kadhalika fake za kutumia!