Zitto aituhumu Serikali kuficha takwimu za wagonjwa na vifo vya COVID-19, adai Zanzibar pekee vifo ni 32 na wagonjwa 235

Zitto aituhumu Serikali kuficha takwimu za wagonjwa na vifo vya COVID-19, adai Zanzibar pekee vifo ni 32 na wagonjwa 235

Hii report itaondoka na vichwa vya watu...HALi ni ...
 
Hali inatisha sana!!
Kwani swala la vifo ni jambo la muungano? Zitto akasome katiba ya Tanzania kama swala la marehemu ni mambo ya muungano

Wazanzibari wanatangaza Vigo vyao na sisi vyetu asichanganye mambo
 
Kwani swala la vifo ni jambo la muungano? Zitto akasome katika ya Tanzania kama swala ya marehemu ni mambo ya muungano

Wazanzibari wanatangaza vyao na sisi vyetu asichanganye mambo
Wewe huelewi hata kinachoongolewa. Out of context out of content.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli, Majaliwa Ummy Pls kuweni na hofu ya Mungu toka vifo vya corona vimeanza kujitokeza kwenye mitandaoni tu watu wanalipotiwa kwa siku kufa ni zaidi ya kumi

Na ni kila siku zaidi ya mwezi jamani nyie mnataka tuamini ni 16? Je watu ambao sio maarufu hali ipoje?

Serikali toeni takwimu sahihi hasa za vifo Dar, Dodoma, Arusha na mwanza tuna haki ya kupata takwimu sahihi.
 
Wewe huelewi hata kinachoongolewa. Out of context out of content.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ndie hujui kama zitto Zanzibar wanatangaza vifo vyao kupitia waziri wao Wa afya na sisi tunatangaza vyetu sababu mambo ya vifo sio jambo la muungano.

sasa mjinga Zitto hajui hata katiba inasemaje kadakia tu hewani ohhh serikali waongo mbona Zanzibar waongo mbona Zanzibar wamekufa 32 so what? Kwani kuna mashindano ya kufa kwa corona kati ya Zanzibar na Tanzania bara?
 

Attachments

  • IMG-20200507-WA0015.jpg
    IMG-20200507-WA0015.jpg
    77.7 KB · Views: 1
Aambiwe Rais kwamba kukosekana kwa taarifa sahihi kuhusu ukubwa wa tatizo la kirusi cha korona
ndio tatizo juu ya tatizo kwa sasa. Hii inapelekea watu kutochukua tahadhari. Aambiwe Rais kwamba hawa wanaokufa wanaacha familia zilizokuwa zinawategemea.

Taarifa ni mhimu kujenga uelewa mmoja wa ukubwa wa hili tatizo kama taifa.

Kama ugonjwa umedibitiwa haupo tena tupewe taarifa rasmi. Nakama ugonjwa bado una trend tupeni updates wote tujilinde kwa kutumia taarifa sahihi.

Kwa hali ya sasa nikama tumeachwa njia panda haieleweki nini kinajiri .matokeo yake unaingia kwenye daradara unakuta wengine wamevaa barakoa wengine hawajavaa.Hata masoko ni hivyo hivyo .

Hali ya sasa inaonesha kuna kutokujali maisha ya watu . its like we have given up the battle and the stronger up there thinks they're safe enough. Siungi mkono rock down .Ila naunga mkono upimaji utolewaji na utolewaji wa taarifa sahihi ili tujilinde siye na familia.

Narudia tena. The way it stand nikama wananchi tumetelekezwa
 
kuna methali zingine huonekana kama za kijinga au kipuuzi,lakini zina maana sana, ukificha ficha sana kifo kina umbua, hivi inatusaidia nini kuficha ficha maradhi ya covid, siasa mpaka katika vitu vya msingi tena hatari kama magonjwa ya mlipuko.

sioni dalili nzuri sana huko tunako elekea, kwa vile ninaona siasa zinaingia mpaka huku kwenye mambo hatari hivi.
 
Kwa tafsiri ya neno msukule ambayo ni binadamu aliyetolewa ufahamu na kuwekwa mafichoni ili kutumika kufanikisha majukumu fulani fulani, ni wazi kuwa pana haja sasa ya kupanua wigo kuwaongeza humo wengi tu na wa aina hiyo tofauti ikiwa tu hawa wengine kutokuwa mafichoni. Ninasema hivi kwa sababu hizi:

1. Watanzania wameambiwa kuwa uchaguzi mkuu 2020 uko pale pale. Pana idadi kubwa ya walioaminishwa hilo na hivi sasa wako kwenye maandalizi kabambe ya kuelekea kutia nia.

2. Wameambiwa mzee baba yuko kwenye kutathmini kuachia ligi kuu na michezo mingine kuendelea. Pana idadi yao kubwa yao ambao wameaminishwa hilo pia na hivi sasa wako kwenye maandalizi kabambe kuanza mazoezi kujiwinda na ubingwa mara tu ruhusa itakapotolewa.

Yako mengi achilia mbali ya kuaminishwa kuwa:

4. hakuna takwimu mpya kuhusiana na Corona nchini tokea Apr 29.
5. vifo vya kushangaza tunavyoshudia ni vya kawaida tu na kwanza eti ni vichache tu,
6. vita vya Corona tumeshashinda,
7.wenzetu waliochukua hatua hali ni mbaya kuliko sisi
8. Huu ugonjwa ni kaupepo, kasikosioathiri waafrika wala kuwa na madhara kwenye nchi za joto,
9. Nk, nk.

Hii ni bila kujali hali ya ugonjwa inapungua au la, na hakuna dalili zipi za ugonjwa huu wenye kuuwa saba, angalau lini au vipi utadhibitiwa.

Uwezo wa watu hawa kufikiria nao uwezo unafikirisha. Kwa kutoweza kustahimili hoja, midomo yao imewajaa matusi yasiyo mithilika na kejeli zisizokuwa ba mbele wala nyuma na wala mashiko yoyote.

Ama kweli misukule haiko madarini mwa manyumba peke yake, bali hata barabarani na sasa ipo hadi jf ikiwa na ID genuine na hali kadhalika fake za kutumia!
 
Mbona rahisi tu.
Zanzibar vifo 32, jumla kuu 16......Bara kuna vifo -16 (hasi 16).
Yaani Bara anaidai covid vifo 16
 
Back
Top Bottom