WanaJF!
Binafsi nina amini katika 'uongozi' na sio hali ya taasisi, hii ni kwa
kumaanisha kuwa endapo akipatikana kiongozi bora, basi hata taasisi iwe
hoi namna gani itanyooka tu na kuwa yenye tija na yenye manufaa makubwa
kwa umma.
Nina yasema haya kwa kutambua kuwa hivi karibuni una tarajiwa kufanyika
uchaguzi wa ndani ya CHADEMA ambao umekuwa ukifanyika kwa kila baada ya
miaka mitano, hivyo mimi kama mwananchi mpenda amani, haki na usawa,
nimeona nitoe yaliyo moyoni kuhusu uchaguzi huo.
Zitto ni kijana ambae amehusika kwa kiasi
kikubwa katika haya mabadiliko tunayo yaona hivi sasa kwa CHADEMA na
taifa kwa ujumla wake, ni kijana ambae amejitoa kuhakikisha haki ina
tolewa, usawa una kuwepo na sheria zinafuatwa, na hayo amekuwa
akihakikisha yanafanywa na kuonekana kufanyika.
Zitto ndiye amekuwa tanuru la vuguvugu lenye
kutoa hamasa na ujasili kwa vijana kuamka na kuhoji juu ya mambo
mbalimbali yanayogusa mstakabali wa taifa letu, kwani itakumbukwa vijana
wengi walijiunga na CHADEMA kwa kuvutiwa na ushawishi wa Zitto, uwezo
wa kujenga hoja na uzalendo wake.
Aidha, itakumbukwa kuwa
Zitto ndiye aliye
ifyeka njia na kuwaandalia mazingira ya kuaminiwa na wananchi hawa
wabunge wapya wa CHADEMA, kwani ni
Zitto ndiye
aliyekuwa akiibua mambo mbalimbali ya kifisadi serikalini, hii ilijenga
imani kuwa ya wananchi kwa kijana huyu na kupelekea CHADEMA kujulikana
nchini.
CHADEMA (nikiwa na maana ya wanachama) kama itajivika ujasiri na kukataa
hali ya kuendeshwa na kikundi cha watu wachache na ikathubutu kumpa
ridhaa ndugu
Zitto nafasi ya uenyekiti wa chama
hicho, binafsi nitatoa kura zangu kuanzia ya urais, ubunge mpaka
udiwani kwa CHADEMA bila kujali ni nani aliye simamishwa kugombea nafasi
hizo (soma aya ya kwanza).
ANGALIZO: USHABIKI WA ITIKADI ZA KISIASA NI KIKWAZO KWA MAENDELEO YA
NCHI.