Zitto akosoa wasifu wa Membe kuacha uanachama wake ACT-Wazalendo. Alaani walioshiriki kumchafua kupitia magazeti

Zitto akosoa wasifu wa Membe kuacha uanachama wake ACT-Wazalendo. Alaani walioshiriki kumchafua kupitia magazeti

Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameonyesha kutoridhishwa na wasifu wa Bernard Kamillius Membe (69) kutogusia uwepo wake ndani ya chama hicho cha siasa.

Membe ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa alijiunga na ACT-Wazalendo Julai 15, 2020 akitokea chama tawala- Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichomlea. Hata hivyo, Mei 29, 2022 mwanasiasa huyo alirejea CCM.

Leo Jumapili, Mei 14, 2023, mwili wa Membe unaagwa Kitaifa katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kisiasa, wanadiplomasia na Serikali wakiwemo, Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu wake, Dkt. Philip Mpango na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Mara baada ya Zitto kuitwa kutoa salamu za rambirambi kwa niaba ya vyama vya siasa, alianza kwa kutoa angalizo kwamba atatumia zaidi ya muda uliopangwa wa dakika mbili.

“Sitaongea kwa dakika mbili, tunasherehekea maisha ya mtu aliyefanya mengi katika Taifa hili. Sitaongea kwa niaba ya vyama vya siasa kwa sababu sijaongea nao kupewa hiyo ruhusa, nitaongea kwa niaba yangu binafsi kama mtu ninayemfahamu Membe na pia kama kiongozi wa chama ambacho Membe alikuwa mwanachama.

“Na ni muhimu sana historia iwekwe vizuri, maana nimemsikiliza Jaji akisoma wasifu wa marehemu hajaweka kama Membe aliwahi kuwa mwananchama wa ACT -Wazalendo na alikuwa mgombea Urais katika uchaguzi mkuu uliopita,” amesema Zitto.

Katika wasifu uliosomwa mbele ya waombolezaji eneo la siasa, umegusia kuwa amewahi kuwa Mbunge wa Mtama kuanzia 2000 hadi 2015 na alijitosa kwenye kinyang’anyiro cha urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2020 na kuishia nafasi ya tano. Huku ukiacha ushiriki wake ndani ya ACT-Wazalendo pamoja na kugombea urais na ndicho kimemfanya Zitto kufafanua.
Inaonekana Zitto ana uchungu sana na alimpenda sana mwendazake, huko nyuma aliwahi kusema wanaompenda mwendazake wakazikwe nae huko na sasa nae zamu yake imefika, aach porojo aonyeshe mfano wa kupenda kwa vitendo.
 
Kwanini Zitto asiwalaumu TISS wanapofanya kazi kwa maslahi ya CCM, badala yake anawalaumu TISS wanapofanya kazi kwa maslahi ya watu binafsi?

Au TISS wakiibeba CCM kwa Zitto sio tatizo kwasababu anajua ana "interest" zake huko, hata hizi shutuma zake kama zingekuwa zimewagusa marafiki zake ndani ya CCM asingesema chochote, ni mnafiki tu.

Makonda alipompiga Mzee Warioba ngumi wakati wa awamu ya rafiki yake, Zitto aliwahi kukemea kile kitendo? Ulimboka kutekwa na kuteswa Mabwepande, Zitto alikua hajazaliwa?!
Kumbe wewe humjui huyu Mrundi, anajua sana kujipendekeza kwa wakubwachuki kwa mwendazake ilianza pale alipojitoa ufahamu wakati wenzake walisusia ufunguzi wa bunge yeye akabaki mjengoni na akapongeza sana na mwendazake, yeye alidhani mwendazake atampa uwaziri wa nishati na madini lakini mwendazake akamshiti wakati yeye alijua ataukwaa uwaziri aikiweka historia kama waziri kutoka upinzani, maono na ndoto zake zikafa kibudu na hapo ndipo chuki ikaanza.Huyu jamaa alitolewa kwenye kamati ya bunge ya mashirika ya umma baada ya kubainika kuwa alifanya mtaji wa kujipatia mlungura, na kuna wakati alitiahidi kuwataja walioficha pesa Uswisi lengo ilikuwa awa blackmail hao wenye vijisenti. huyu jamaa amebaki kusafiria nyota ya matukio, ni mjanja tu wa mjini.
 
Kwani uongo, hao tiss sio kutumika tu kutukana viongozi, bali ndio walitumika kuharibu chaguzi za nchi hii kipindi chote cha dhalimu. Huo ni ukweli ulio wazi na Zito kausema tu kukazia ukweli huo.
Vipi uchaguzi wa 2010 ulikua halali?
 
Kwamba Zittow hakumsikia membe akikana kuwa hakuwahi kuwa mwanachama WA ACT?
 
Ulikuwa na afadhali kuliko ule uhayawani wa dhalimu wa 2020.
Tunaongelea uhalali, Nyeusi ni nyeusi na nyeupe ni nyeupe. Uchaguzi ulikua halali au si halali?Nilishuhudia akina mahanga wakiwa na mabox ya kura.Sasa kwanini ujitoe ufahamu na kufanya jambo la wizi wa kura kaleta Magufuli?CCM ndio wanaamua nani awe Rais,mbunge au diwani na wapi.Hata uchaguzi ujao wataamua hivohivo, Wakitaka mbeya yote iwe ccm wanafanya na hakuna wa kupinga, Wakitaka Sugu apewe nusu mkate wanafanya. 2025 kuna majimbo upinzani watachukua na hii itakua hisani ya ccm,si umemsikia boss wako Lisu?
 
Tunaongelea uhalali, Nyeusi ni nyeusi na nyeupe ni nyeupe. Uchaguzi ulikua halali au si halali?Nilishuhudia akina mahanga wakiwa na mabox ya kura.Sasa kwanini ujitoe ufahamu na kufanya jambo la wizi wa kura kaleta Magufuli?CCM ndio wanaamua nani awe Rais,mbunge au diwani na wapi.Hata uchaguzi ujao wataamua hivohivo, Wakitaka mbeya yote iwe ccm wanafanya na hakuna wa kupinga, Wakitaka Sugu apewe nusu mkate wanafanya. 2025 kuna majimbo upinzani watachukua na hii itakua hisani ya ccm,si umemsikia boss wako Lisu?

Magufuli hakuiba kura usichanganye boss, Magufuli alinajisi uchaguzi. Nakupa mfano mmoja, huwa kuna ajali za meli ziwani, lakini huwezi kusema ajali ya MV Bukoba ilikuwa ni kawaida eti kisa huwa kunatokea ajali nyingine huko ziwani.

Ni kweli CCM kwa kushirikiana na vyombo vya dola inaweza kupora uchaguzi, na kuamua nani atangazwe mshindi. Lakini hii sio sifa bali ni upuuzi, nashangaa unapoiongelea kama ni sifa.
 
Nimeona mahala Zitto akitamka kwa kujiamini kuwa taifa letu lilifikia pabaya sababu Tiss ilitumiwa na watu wa serikali ili kutukana viongozi wastaafu na waiowastaafu.

Hapa alimaanisha wazi kuwa Tiss walimtumia Musiba.

Tiss ni idara ya serikali na sio mtu. Ni taasisi ya umma ambayo ikichafuliwa kwa tuhuma kama hizi hachafuki mtu bali ofisi ya umma.

Je ni kweli taifa letu linakuwa na idara kama hii ambayo inatumika kutukana viongozi?
Haijachafuliwa Bali ilijichafua yenyewe
 
Back
Top Bottom