Zitto ataka wanaoikosoa ACT-Wazalendo waanzishe chama chao

Imenichukua takriban wiki moja kusoma malalamiko ya wote dhidi ya maamuzi ya ACT kujiunga SUK.

Nilichokuwa nasubiri ni kuona hao watu wanakuja na solution/mapendekezo juu ya nini ACT wazalendo wangekifanya baada ya hapo kama wasingejiunga na SUK! Well kuna baadhi ya wanachadema wamekimbia nchi- Sijui kama hilo ndio jibu! Lakini ni hatua mojawapo, muda utatuonyesha. Kuna covid-19 ikaamua kuapishwa na spika- nayo ni hatua mojawapo ambayo kikundi fulani kimeona ni dawa ya kubadili mtazamo wa CCM. Mimi naamini kuwa yote haya yanafanyika kwa nia njema sana ya kubadili mbinu za CCM mbele ya wapinzani.

Ni ukweli usiofichika kuwa mbinu ya kuwaingiza wananchi barabarani ilishindikana, kwa vile watawala walitumia nguvu za ziada za kukabiliana na wananchi. Swali linabaki pale pale, tunafanya nini katika hatua ijayo. Sijasikia lolote toka kwa CHADEMA zaidi ya kudeal na covid-19 na waliokimbia nchi.

Binafsi sikilaumu chama chochote kile kwani yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi ni mshtuko mkubwa kwa kila chama. Hakuna aliyejua watawala wangeenda mbali namna hii bila aibu mbele ya macho ya waangalizi wa nje na ndani. Hakukuwa na haiba kabisa, ni ubabe wa aina yake.

Katika wakati kama huu, ili kuwaunganisha wanachama wa kila chama kunahitajika kurudi nyuma kwanza hatua kadhaa ili kujipanga upya. Ni strategy muhimu sana hii katika uwanja wa vita, vinginevyo mtamalizwa wote na msiwe na askari hata wa kupiga kelele. Hivyo kwangu alichokifanya ACT ni kurudi nyuma na kujipanga upya. Tunasubiri move ya CHADEMA, kwani sijaisikia!

Hata hivyo nyie mnaolaumu bado mna nafasi ya kueleza ACT wangefanya nini? Tiririkeni!
 
Zito kiasilia ni bahili isitoshe hizo pesa wanagawana na viongozi wenzao wengi na zitazosalia zitaimarisha chama, ukumbuke hiyo ni Rushwa lazima matumizi yake yanafanyika kwa siri kukwepa ushahidi wa mali kuonekana , Zito shamba lake ni Siasa amevuna pesa nyingi kupitia Siasa tokea utawala wa mkapa kikwete hata awe na pesa nyingi huwezi kumjua kwani mda wote hujidai Masikini saa 24
 

Kwa hiyo unaamini ruzuku aliyolipwa CHADEMA kwa karibia miaka 5 apewe Zitto Kabwe kama sadaka mara moja tu? Na kwa lipi haswa hadi alipwe hela zote hizo ?
 
Hata wewe haulewi maana ya dola milion 5 USD unataja tu namba, laiti ungeelewa usingeamini kirahisi hivyo kwamba Serikali inaweza kumpa Zito Kabwe hela zote hizo, for what ?
Serikali ina pesa nyingi mno vipesa kama dola milion 5 kwao ni vipesa kidogo mno
 
Serikali ina pesa nyingi mno vipesa kama dola milion 5 kwao ni vipesa kidogo mno

Ndo maana nasema unarusha tu namba lkn hauelewi maana yake nini, labda hauelewi unaweza kufanya nini dola US milioni 5, vinginevyo usingeamini kirahisi hivyo, ...
 
Kwa hiyo unaamini ruzuku aliyolipwa chadema kwa karibia miaka 5 apewe Zito Kabwe kama sadaka mara moja tu ? Na kwa lipi haswa hadi alipwe hela zote hizo ?
CHADEMA ina watumishi wengi gharama za kuendesha chama ni kubwa isitoshe CHADEMA hutumia gharama kubwa kujihami dhidi ya hujuma za CCM ikiwemo utitiri wa kesi za kubambikiwa na mambo mengineyo ya hovyo tokea CCM, CHADEMA inatumia pesa nyingi kuzuia dhahama za CCM na mengineyo mengi ya ajabu tokea CCM ikiwemo chaguzi za marudio
 

Naifahamu vizuri historia ya Maalim Seif na Znz, nashukuru kwa mtiririko wako mzuri kuhusu safari ya kisiasa ya Maalim Seif. Ila uliponiquote sina popote nilipomtaja Maalim Seif, maana najua Maalim Seif ni tofauti na ACT ambayo iko chini ya Zito. Nimemtaja Zito maana ndio mwenye chama cha ACT. Maalim Seif ni taasisi yenye kama yeye, popote au chama chochote atakachoenda Wapemba wenzake watamfuata. Kwa maneno marahisi, Maalim Seif hahitaji chama chochote kufanya siasa za huko Znz, maana tayari ana wafuasi wa rohoni, ila ni wachache sana unapoitaja Tanzania.Rejea anguko la CUF baada ya Seif kuondoka kudhibitisha Seif ni taasisi ndani ya Taasisi.

Namzungumzia Zito maana ndio mwenye chama cha ACT, ili ACT ikue hasa huku bara ilipaswa kutembea pembeni ya bega la cdm, hapo ingepata imani kubwa sana ya wapinzani. Ukweli usioacha shaka ni kuwa cdm ndio yenye wafuasi wa upinzani wengi hasa vijana, na ccm tayari ni chama kilichopitwa na wakati, ila ina mwenyekiti mwenye kiburi cha madaraka kwa kofia ya urais. Matumizi haya mabaya ya madaraka, kwa makusudi au kwa bahati mbaya inasemwa kuwa ni uimara wa ccm jambo ambalo si kweli. Mwenyekiti huyu akitoka madarakani, ni nadra mwenyekiti ajaye wa ccm kuwa na misimamo yake, kwani tayari nchi ipo kwenye mahusiano mabaya kimataifa, na sehemu yenye tatizo ni demokrasia na Utawala bora kwa sababu ya rais huyu. Mbinyo atakaoupata mwenyekiti ajaye wa ccm ni kuheshimu utawala bora na demokrasia, hivyo uwanja wa siasa utarudi kama inavyopaswa ikiwemo uhuru wa vyombo vya habari , kwa vyovyote vile ccm tayari itakuwa imelamaa kwenye ushindani kwani inategemea zaidi kubebwa, hivyo cdm itaonekana tena maana ina wafuasi watiifu, wakati huo ACT itakuwa imepoteza imani kwa watu wenye imani ya upinzani, na eneo dogo la Znz ambapo Maalim Seif yupo, atakuwa amezeeka hivyo kushindwa kwenda na changamoto za wakati huo. Je ni nani atavaa viatu vya Seif na awe na ushawishi kama Seif? Je Zito huku Bara atatoboa kutokana na maamuzi ya chama chake kwa sasa?
 
Ndo maana nasema unarusha tu namba lkn hauelewi maana yake nini, labda hauelewi unaweza kufanya nini dola US milioni 5, vinginevyo usingeamini kirahisi hivyo, ...
Kwako binafsi unaona ni pesa nyingi lakini kwa Serikali ni pesa kidogo sana kwani utulivu wa Serikali ya Zanzibar utapelekea kupata misaada mingi tokea nje na hiyo pesa unarudi ndani ya mda mchache sana
 
Mbona wakati anahamasisha watanzania wajiunge na chama cha Act wazalendo hakusema waanzishe chama chao ?au ndio upimbi unamsumbua baada ya kuusaliti umma wa watanzania yeye na Maalim Seif ?
Pesa waliyochukua imemtia kiburi
 
Maamuzi ya ACT lakini CHADEMA mnalia lia
Naona safari hii umelambishwa shubiri,umetupwa kama ganda la muwa lisilo na thamani.

Hutokaa uisahau ccm ya kina ngosha, sasa kaa chini utulieze akili yako ili ulee watoto wako wasiyo na baba.
 
Kilichowazuia kutoka barabarani ni nini wakati mlitakiwa kuidai hiyo haki na hamkutoka?
Zitto kachanganya na za kwake baada ya kuona mmemterekeza siku ya kuandamana.
Sasa wenye hasira na hiyo SUK anzisheni chama nanyi mkapinge kujiunga nayo.
Kuandama kwenye serikali dhalimu siyo rahisi maana unaweza kosa viungo vyako vyote
 
Safi sana maswali yamekuwa mengi, unapokuwa na kiongozi kama Zitto Kabwe na Maalim Seif pamoja hutakiwi kuwa na mashaka nao kuhusu maamuzi yoyote, maalim siku zote amekuwa muaminifu na husimama upande wa wananchi ni suala la kuwapa muda tu kwa kile walichokiamua kwenye Kamati tukaona impact yake
 
We kamanda unajilopokeaga tu.. Hivi unajua dola milion 5 ni kitu gani katika uhalisia?
Ni bilion 10 tu, kwa mfano yeye akiweka kibindoni bilion 2, halafu nane zilizobaki akawagawia genge lake ili wamuunge mkono watulie wewe huoni kuwa inawezekana kabisa?

Jiwe anafahamika kuwa ni mwepesi wa kupenyeza rupia ili kutuliza upinzani mkali mfano mmojawapo ni jinsi alivyomtuliza Mange kwa mpunga mrefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…