Mimi ni mkristo na kuna mambo samiah amefanya vizuri sana anastahili pongezi.
Lakini hili la kusafirisha wanyama hai nitalipinga sio kwasababu yeye ni muislamu,au kwakuwa yeye ni mzanzibar au kisa yeye ni mwanamke!!!..arooo!!!
Wanyama ni rasilimali ya taifa ,nyara za taifa ,urithi wa taifa hili,pride ya taifa hili.
Mkiwauza huko nje wakawekwa kwenye zoo zao watakuja huku kufanya nini sasa !?
Kuna mambo tuwe tunafikiria basi
Kama wamejazana huko porini hadi kuingia makazi ya watu wachinjeni tuuzieni mimi sijawahi kula nyama ya swala au nyati tangu nizaliwe hio fursa nitaichangamkia haraka sana (demand &supply).
Kama hawaliwi wavuneni ngozi,kwato,sumu muuze kama products tupate hizo hela.
Acheni mambo ya kijinga
Mkuu naona huelewi principal za uchumi za kibeberu dhidi ya Afrika…endelea tu kuomba Mungu apatikane JPM mwingine…bila hivyo utaumiza kichwa sana