Zitto: Baadhi ya mitambo ya Vyombo vyetu vya na dola mlitumika kumchafua BM

Zitto: Baadhi ya mitambo ya Vyombo vyetu vya na dola mlitumika kumchafua BM

Zitto katoa kashfa nzito kuvihusu vyombo vya dola kwa kutumika kumchafua Membe ikiwamo mitambo ya vyombo hivyo kutumika kuchapisha magazeti ya kumchafua.

Maoni yangu:

Hii kashfa ni kubwa mno kutolewa na mfanya siasa kama Zitto tena mbele ya Amri Jeshi Mkuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na ni lazima Mamlaka vitolee ufafanuzi tuhuma hizo.

Pia, Zitto aitwe na atoe uthibitisho wa kashfa hiyo.

Ni aibu endapo kashfa hiyo itaachwa na kufumbiwa macho pasina mtoa tuhuma hizo kuhojiwa ili athibitishe pasi na chembe ya shaka kwazo.
Hajasemwa uongo. Ni ukweli. Ila nachomshangaa anajifanya kuwa hajui ni kwa sababu ya rais kupewa nguvu zilizopitiliza na katiba yetu? Mbona ameweka break kwenye kudai katiba na anatumika kufifisha juhudi?
 
Kumjibu mpuuzi kama zitto ni kupoteza muda tu

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app

Jibu hoja acha kuleta propaganda zenu za kichumia tumbo. Gazeti la TANZANITE lilikuwa linachapishwa na mitambo ya Serikali na hiyo inajulikana na hakuna atakayebisha!! Kitu kilicho wazi unataka ushahidi wa nini? Acheni upuuzi menu.
 
Zitto Kabwe (Mb) ametusaidia kuunganisha doti na nukta kuhusu umauti wa the late ex-FM na issue ya deni la Mr Funeral. Wake up guys!
Kwani si inajulikana, au we hujui! Ilibidi yule aleftishwe ili nchi itulie mana ilikuwa inaongezwa kinyumenyume hata usalama walimchoka kabisa
 
Zitto katoa kashfa nzito kuvihusu vyombo vya dola kwa kutumika kumchafua Membe ikiwamo mitambo ya vyombo hivyo kutumika kuchapisha magazeti ya kumchafua.

Maoni yangu:

Hii kashfa ni kubwa mno kutolewa na mfanya siasa kama Zitto tena mbele ya Amri Jeshi Mkuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na ni lazima Mamlaka vitolee ufafanuzi tuhuma hizo.

Pia, Zitto aitwe na atoe uthibitisho wa kashfa hiyo.

Ni aibu endapo kashfa hiyo itaachwa na kufumbiwa macho pasina mtoa tuhuma hizo kuhojiwa ili athibitishe pasi na chembe ya shaka kwazo.
Kafuatilie kesi ya Membe. Membe alipofungua kesi ilibidi TISS wakubaliane naye ili wamnunulie musiba mitambo mipya ili wasiunganishwe kwenye kesi.
 
Kwani amesema uwongo? Amesema ukweli ili fundisho vyombo hivi visitumike vibaya kuchafua watu kwa manufaa ya kisiasa
Zitto ameongea ukweli kabisa na tunahitaji mabadiliko makubwa kwenye vyombo hivyo ili visitumike na wanasiasa dhidi ya maadui zao wa kisiasa.

Usalama wa Taifa, Mapolisi, Takukuru, Magereza JWTZ vifanye kazi zao kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Nchi.

Ni ajabu sana baadhi ya vyombo kutumia Wahuni kama Musiba kiwachafua Wananchi.
 
Katumwa huyo na smile!

Kwani Mr smile alikuwepo kwenye kumuaga!!?

Zito ananunua ugomvi na dola tena wa bure KABISA!!!

Yeye angeaga na kutuliza tu,dola haishindwi na uchawi wa ziwa Tanganyika!

Asije sababisha akawa tagert bila kutegemewa!

Dola haitukanwi,kama yeye anajiona ni mwanaupinzani maarufu ajiulize Maalum seif watu washa sahau kabisa kwamba alikuwepo ACT wazalendo!!
Kiongozi mkuu wa chama cha upinzani bila shaka ametumwa na kundi la upande huu ili kutetea ule msimamo wa the late ex-FM.

It means hapo tayari kuna vita baridi na moto kwa pamoja. Ukirejea maneno ya Waziri & Mbunge wa Mtama utaelewa vizuri.

Njia pekee ya kutokea, kwa mtazamo wao, ni kuikuza issue ya Mr Funeral na the late ex-FM ili liwe suala ama mgogoro wa taifa zima (and here, frankly, they've a point).

Lengo kubwa hapa ni malipo ya zile bilioni 9. Hakuna miongoni mwao atakayeridhika iwapo Mr Funeral hatawajibika. Na kuwajibika kwake ni sawa na karipio kubwa lingine kwa utawala wa Mr Chuma. All dots are clearly connected and astonishingly related.
 
Zitto katoa kashfa nzito kuvihusu vyombo vya dola kwa kutumika kumchafua Membe ikiwamo mitambo ya vyombo hivyo kutumika kuchapisha magazeti ya kumchafua.

Maoni yangu:

Hii kashfa ni kubwa mno kutolewa na mfanya siasa kama Zitto tena mbele ya Amri Jeshi Mkuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na ni lazima Mamlaka vitolee ufafanuzi tuhuma hizo.

Pia, Zitto aitwe na atoe uthibitisho wa kashfa hiyo.

Ni aibu endapo kashfa hiyo itaachwa na kufumbiwa macho pasina mtoa tuhuma hizo kuhojiwa ili athibitishe pasi na chembe ya shaka kwazo.
Tumekwisha toka kwenye nyakati hizo za kubana uhuru. Kama siyo kweli wahusika wakanushe
 
Back
Top Bottom