Zitto hafai kuaminika kwenye struggle za nchi hii, yule ni compromised Politician

Mzee Mgaya hakuwepo kwenye msafara huo kweli??

Tupatupa wa Lumumba???

Jaribu kukumbuka vizuri
 
Zitto kasingiziwa kipi? vile vikao alivyokuwa anafanya enzi za JK kwa siri usiku halafu akiulizwa anadai JK ni sawa na baba yake then anakuja kutaka uenyekiti wa Chadema nani mwenye akili timamu atamuamini?
 
Wacha porojo sijui umekuwa akili mwaka gani. Hakuna anayemjua Zitto atleast kuanzia 2014 asiyejua tabia zake halisi, ni undumilakuwili.

Ni huyo Zitto na wenzake kina Kitila ndio walikuwa na mpangonwa kumpindua Mbowe 2014 akipata msaada toka kwa aliyekuwa Rais wa wakati huo, bahati nzuri Chadema wakamshtukia wakamtimua.

Hakuna uahirikiano utakaofanya na mtu asiye na msimamo, labda uwe mjinga usiyejitambua, coz siku yoyote akikubadilikia utabaki peke yako unachekwa kwa aibu na wanaojielewa.

Kama Zitto leo anataka ushirikiano kuna vile vyama marafiki wa ACT waliohudhuria kile kikao cha kujadili Katiba Mpya wakaja na mapendekezo haihitajiki kwa sasa, hao ndio wanafaa kuwa marafiki zake.
 
Zitto kasingiziwa kipi? vile vikao alivyokuwa anafanya enzi za JK kwa siri usiku halafu akiulizwa anadai JK ni sawa na baba yake then anakuja kutaka uenyekiti wa Chadema nani mwenye akili timamu atamuamini?
Lakini wakuwaamini ni wale waliozunguka nchi nzima wakitoa list of shame wakisema lowassa ni fisadi papa, wakisema hata Mungu atawabariki wale watakaompiga mawe, wakisema matatizo ya nchi yamesababishwa na fisadi lowassa, wakasema kuwa ATC wazalendo ni chama cha lowassa, halafu baadae wakamchukua Lowassa wakampa kijiti cha kugombea uraisi via chama chao. Au sio mkuu?
 
Chadema mnaiweka hata pasipostahili, shughulikieni kwanza matatizo na ndani kwenu ndio muanze kuiwaza Chadema.

Mwambie Zitto ajipange na vijana wake atleast wawe na msimamo mmoja, sio yeye atake Tume Huru, then Nondo atake Katiba Mpya.
 
Hao waliowahi kusema hivyo atleast sasa wamebadilika, wanaonekana kuifuata njia iliyo sahihi na umma wa watanzania unawaamini, uthibitisho wa hili ni kesi ya mchongo ya Mbowe na uungwaji mkono walioupata ndani na nje ya nchi mpaka DPP akaweka mpira kwapani.

Huyo Zitto wako mpaka leo bado haaminiki, alishasema juzi tu awamu hii hatakuwa wakupinga pinga, ni rafiki wa ikulu, na kuthibitisha hilo anafanya vile Samia anavyotaka, mfano Samia alisema Katiba Mpya isubiri, Zitto wako nae ameamua kusubiri.

Sasa wewe msemaji wake unataka nani amuamini Zitto wako?
 
Nyie ndio kila kukicha hamuachi kutuletea issue za Zitto…hata akipost Matokeo ya team yake ya Liverpool lazima m comment mambo ya siasa…jifunzeni kuendelea na biashara yenu ya Siasa…kama kusalitiwa mmeshasalitiana sana ndani ya Chama chenu…

Zitto kawasaliti kuliko Slaa?, Kuliko Mashinji, kuliko Mwita, kuliko Partrobas, kuliko Halima Mdee?

Tatizo lenu mna mihemko sana mnataka nyie ndio muwe Kamusi ya Siasa za Upinzani…kila mtu afanye siasa zake na msipangiane
Chadema mnaiweka hata pasipostahili, shughulikieni kwanza matatizo na ndani kwenu ndio muanze kuiwaza Chadema.

Mwambie Zitto ajipange na vijana wake atleast wawe na msimamo mmoja, sio yeye atake Tume Huru, then Nondo atake Katiba Mpya.
 
Wamebadilika wapi? Ingelikuwa ni Zitto katoka gerezani directly ikulu zingefunguliwa thread 500 humu akituhumiwa.

Zitto ni mtu mwenye mawazo huru, sasa shida ni pale mnapotaka afuate njia za Chadema hilo haliwezekani maana yeye ni ACT, sasa kwanini mtake kumdictitate?

Na umejuaje kama wamebadilika? Tumeshuhudia marudio ya kupokea rejected products za CCM kuja Chadema mara nyingi na zikapewa nafasi za kugombea baadae zikarudi CCM.

Wanasiasa wote ni ma opportunist, nashangaa mnaomsema zitto. Wote hao ni ma opportunist.
 
Kila mtu afanye siasa kwa style yake. Zitto mlishamfukuza kaanzisha chama chake lakini mpaka leo Zitto, Zitto.
Kama vyama vyote vya upinzani vingekuwa vina mtazamo unaofanana, basi hakuna haja ya kuwa na chama cha upinzani zaidi ya kimoja.
Unaelezwa msimamo wa cha fulani uamue mwenyewe kujiunga, hapo hakuna shida, amefukuzwa na chadema tabia zake ziwe wazi ili wanaojiunga naye wajue wako upande gani.
 
Na hao wanaojifanya wana uchungu nakumbuka Halima Mdee alivyokuwa anamshambulia Zitto kwa maneno mabaya na matusi ila usaliti aliowafanyia Chadema, ni wa kiwango kikuu.
 
Unaelezwa msimamo wa cha fulani uamue mwenyewe kujiunga, hapo hakuna shida, amefukuzwa na chadema tabia zake ziwe wazi ili wanaojiunga naye wajue wako upande gani.
Tabia gani? Wewe ndie una analyze tabia za watu?

Mko obssesed na zitto. Fanya siasa zenu na yeye afanye zake.

Chama chake kidogo hata hakiwezi kushindana na nyinyi bara lakini sijui kwanini kinawaogopesha.
 

Kuvunjika kwa koleo hakujawahi kuwa mwisho wa uhunzi.

Kwamba Mandela ali engage na kina Buthelezi?

Hatuwezi kuwaamini Mbowe au Lissu ku engage na Zitto ikiwezekana tukapata katiba hii mwaka huu?

Kwanini linalowezekana leo kungoja kesho?

Mbona yote yako mikononi mwetu?
 
Ooh leo mmekubali Slaa na Mdee ni wasaliti? hii nimeipenda waambie na wenzako lumumba wajue.

Zitto kusemwa kwa usaliti wake ni haki yake hapa duniani siku zote akipandacho mtu ndicho akivunacho
 
Wacha kulazimisha kumsemea mtu usiyemjua, Zitto ana mawazo huru yapi? yakusikiliza mahitaji ya mtawala na yeye akaamua kuyafuata (Katiba Mpya isubiri!)

Zitto kwanza hawezi kufungwa gerezani kwasababu hana qualities hizo, na zaidi sio threat kwa CCM, usimsemee usiyemjua, yule ni opportunist na watanzania sio wajinga wanajua mbivu na mbichi.

Nimekwambia kule juu nakwambia tena, Chadema wanajielewa na watanzania wanawaelewa, hizo rejects zako mwisho ilikuwa Lowassa, baada ya hapo hakuna tena mambo hayo ni Lissu na wengine watafuata, na siaamini kama wataweza kurudia rejects.
 
Mwambieni Mbowe asiwe na ukaribu na 'Wasaliti'

Kila Mara wako pamoja kuanzia kule Segerea hadi nyumbani Mikocheni wakati nyie oya oya mchuzi juu mnakutana nae kwny mikutano ya hadhara tu

Msilolijua Hata kina Halima Mdee wameenda mara kadhaa kule Segerea kumpa Pole Mzee na wakakaa na kuyajenga mara kadhaa lakin nyie mmegeuka Vipaza sauti visivyo na ufahamu wa yanayoendelea chini ya kapeti
Ooh leo mmekubali Slaa aliwasaliti Chadema? hii nimeipenda waambie na wenzako wajue.

Zitto kusemwa kwa usaliti wake ni haki yake hapa duniani siku zote akipandacho mtu ndicho akivunacho
 
Mbowe alifungwa lini kama sio enzi za magufuli, na hapo ni kwasababu aliokuwa anawatanguliza akina slaa waliondoka chadema, akina tundu lissu na lema wako canada.
Kwahiyo siasa ya upinzani sharti ufungwe ndipo uonekane mpinzani?
Unasema nalazimisha kumsemea mtu wakati uko hapa hapa unamsemea zitto kwa mabaya.
Pambana na chama chenu mwacheni na chama chake si mlimfukuza?
 
Mbowe kuwa na ukaribu na wasaliti hakuondoi ukweli kwamba msaliti ni msaliti, punguza jazba.

Hata wakikutana popote hakuna tatizo muhimu Mbowe anajitambua na bado anawapeleka mbio CCM mpaka DPP anaweka mpira kwapani, kaa unywe maji mengi usife kwa pressure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…