Zitto hana chama, chama ni cha Wapemba na wafuasi wa Maalimu Seif

Zitto hana chama, chama ni cha Wapemba na wafuasi wa Maalimu Seif

Zito Anakwenda Buzebazeba Na Gundu Kuanzisha Chama Chake
 
ACT ni true trojarn horse kwa harakati za upinzani Tz
 
Huwa ana bifu na Zitto mara nyingi nimeona nyuzi zake za kumsiginia kunguni Mwami.
Sina bifu naye ila namfuatilia kwa sababu ni Mwanasiasa anayejua afanye nini wakati gani

Ninachompendea Zitto ni mtu anayependa sana kujifunza hivyo hachukizwi pale anapokosolewa
 
Huyu ndiye aliyekabidhiwa cheti cha usajili wa kudumu wa ACT sijui kama hata Zitto anamkumbuka.

View attachment 2402864

Chama cha ACT kimeanzishwa na kina JK, Membe, Januari, Mwigulu nk kama Backup ya CCM baada ya kuzidiwa na CDM. Zito ndio alipewa jukumu hilo. Hao kina Limbu walitangulizwa tu baadae akataka kulazimisha kuwa kiongozi. Lakini wenye chama wakafanya yao na Zito akapewa nafasi yake. Rejea uchaguzi wa 2015 ACT ikiwa changa kabisa, ilisimamisha wagombea wa nafasi zote kuanzia urais, ubunge na udiwani nchi nzima, huku haifahamiki hela zao zilitoka wapi.

Magufuli 2015 ndio aliharibu mpango wa ACT kuwa chama kikuu cha upinzani, kwani alikuwa hampendi Zito, na pia hakuwa analipenda kundi la JK ambao ndio wafadhili wa ACT. Ni bahati mbaya wakati Maalim Seif anaporwa chama na Magufuli kwa kumtumia Lipumba, Maalim Seif akatafuta chama akaona ACT ndio hakina kiongozi wa muda mrefu na sio cha muda mrefu kama ilivyo CDM, NCCR, TLP nk. Alijua fika akiwa ACT atakuwa na maamuzi yote kama alivyokuwa CUF, na kweli ndio ilivyokuwa, ndio maana alishikilia kumuunga mkono Lisu kwenye urais, na sio Membe kama ambavyo Zito alitaka kwani Membe ndio wenye chama.

Zito ataendelea kuwa kiongozi wa chama cha ACT, kama ataendelea kuwafanya hao Wapemba wafanye Siasa zinazotakiwa na CCM. Hao Wapemba watavurugana na zito siasa za kweli za ushindani zitakapoanza na CDM kushika nafasi yake kama inavyotegemewa. Na zito anajakikisha anafanya siasa zinazotakiwa na CCM, kwa kuwahadaa ACT Wapemba kuwa hizo ni siasa za kistaarabu. Hili jengo la ACT lina fedha ya ufadhilii wa CCM, ndio maana huoni wakitaja thamani ya jengo, wala chanzo cha fedha hizo.
 
Asante wenye masikio na wasikie.
 
Kwamba na wewe unakubaliana na huu uzushi?
Siasa ni biashara kama biashara nyingine bwashee

Kuuza Chama ni Sawa na kuuza Makolo SC yaani mnunuzi anachukua Chama na Wanachama

Mrena rip alinunua TLP

John Shibuda alinunua Tadea

Mo kainunua Makolo SC na akina Mshana jr kapewa nyongeza

Utopolo fc nao wako sokoni

Chama Dola tu ndio hakina Bei
 
ACT - Wazalendo haina wanachama wala jengo la ofisi inalomiliki Bara. ACT inategemea nguvu ya wanachama kutoka Zanzibar wengi wakiwa ni wale waliokuwa wafuasi wa CUF- Maalimu Seif.

ACT -Wazalendo haina Jengo la Chama kwa maana ya umiliki, jengo walilopewa na Maalimu Seif Foundation ni lile walilokuwa wanatumia waliokuwa Wabunge watiifu wa Maalimu Seif, linamilikiwa na familia ya Seif.

ACT Wazalendo haina mtandao Bara mtandao wake uko Zanzibar. Kwa mtu makini ataelewa hapa mwenye nguvu ya chama ni nani kati ya Zitto, Wazanzibari na familia ya Seif.

Siku wenye chama chao wakiamua kuondoka na jengo lao chama kitakufa Zitto atabaki na makaratasi ya Msajili wa vyama vya siasa tu. Jifunze kutoka kwa Lipumba na CUF yake.

Najua wafuasi wa Zitto hawapendi kusikia haya lkn, Ukweli ndio huo.

Zitto and others, Keep this short Thread you will thank me later.
Siku wenye chama chao wakiamua kuondoka na jengo lao chama kitakufa Zitto atabaki na makaratasi ya Msajili wa vyama vya siasa tu. Jifunze kutoka kwa Lipumba na CUF yake.[emoji818][emoji817]
 
Wachezaji kina Mdee na Zitto hahahaaa 😁😁😁

Zitto alikuwa CDM leo ni Kiongozi wa chama, Selasini alikuwa CDM leo ni mkiti wa chama. Bado Mdee kuanzisha chama.
Selasini na Zitto ni CCM kitambo sana
 
Back
Top Bottom