Me ninachowaza tupaze sauti kama wanataka kuwapa watanzania tume huru ya katiba basi basi iwe huru kweli kweli isiingiliwe na mihimili mingine kabisa!
Kwa mfano unaposema tume itaongozwa na labda Jaji fulani ambaye kachaguliwa na Rais moja kwa moja lazima awe biased,
Au Rais ndo anateuwa wajumbe lazima ateuwe anaojua watamfavor,
Tume huru iongozwe na watu ambao hawana affiliation na serikali, kwa mfano taasisi za dini, vyama upinzani vyote viwe na wajumbe angalau hata wawili kwa kila chama, taasisi zinazotetea haki za binadamu wajumuishwe,
Ndani ya hawa wajumbe wafanyiane vetting wenyewe kumchagua mwenyekiti, makamu n.k badala ya Rais kupendekeza viongozi