Zitto, hii ndiyo timu ya kupitia masuala ya Tume Huru ya Uchaguzi uliyotegemea au wamekuchakachua?

Zitto, hii ndiyo timu ya kupitia masuala ya Tume Huru ya Uchaguzi uliyotegemea au wamekuchakachua?

Mmoja wa Wajumbe ni huyu hapa

View attachment 2055090
1640352004420.png

BORA WANGEKUWA HAWA
 
Siasa ni mahesabu. Kwa hili crediti ni CCM na ACT. After all ndiyo vyama vikubwa nchini Tanzania. Chadema ni chama chenye mbunge mmoja tu wa kuchaguliwa. Si mbaya akawaacha vyama vyenye uwakilishi mkubwa wa wananchi wakapanga mambo ya kitaifa kwa niaba yao. Ndiyo democracy by representation inavyotaka.
We MB.WIGA wale wabunge 19 kule Bungeni wanakula kodi zetu kwakutambulishwa kama Wabunge wa chama gani ma.tako wewe?
 
Hongereni viongozi wote siasa mlioshiriki mjadala wa katiba mmefungua mlango mgumu Hongera zitto kabwe
 
Chadema hamkushiriki mkutano, acheni walioshiriki waunde timu inayowafaa. Kelele za nini. Nyie tazameni tu ,train ndiyo inaondoka hivyo bila nyie. Akili za kuambiwa na Lissu muwe mnachanganya na zenu.
Kwani tume ya uchaguzi ni kwaajili ya chadema au kwa ajili ya nchi?.Hizo akili zako nene ziko wapi kama unashindwa kuelewa jambo dogo kama hilo.Hili jambo raia yoyote wa nchi hii anao uhuru wakulijadili maana linahusu mustakabali wa nchi kwa ujumla.sasa wewe umekalia kuwaza vyama tu.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Please remain within the context of the issue.. Chadema wamealikwa wawe sehemu ya mkutano, wamekataa, lakini hapo hapo wanataka wafanye maamuzi ya yanayoendelea ndani ya kikao hicho hicho wao wakiwa nje..Hakuna uhusiano na swali unalouliza.
Wanaoona hila kwenye hii process siyo CDM tu hata wananchi wa kawaida. Usiwasingizie CDM kuhalalisha uhuni wa watu wachache kwa ajili ya maslahi yao..
 
Please remain within the context of the issue.. Chadema wamealikwa wawe sehemu ya mkutano, wamekataa, lakini hapo hapo wanataka wafanye maamuzi ya yanayoendelea ndani ya kikao hicho hicho wao wakiwa nje..Hakuna uhusiano na swali unalouliza.
Kwa hiyo "GERESHA BWEGE" huwa haitolewi maoni?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kwani tume ya uchaguzi ni kwaajili ya chadema au kwa ajili ya nchi?.Hizo akili zako nene ziko wapi kama unashindwa kuelewa jambo dogo kama hilo.Hili jambo raia yoyote wa nchi hii anao uhuru wakulijadili maana linahusu mustakabali wa nchi kwa ujumla.sasa wewe umekalia kuwaza vyama tu.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Kama unajua hilo kuwa linahusu mustakabali wa nchi, washaurini CDM wasiwe wanasusa mambo kama haya. Wao kama wawakilishi wa wananchi wawe wanashiriki kwenye michakato hii badala ya kulalamika wakiwa nje.

Tuliona hilo kwenye Bunge la Katiba, vikao mbalimbali vya Bunge na sasa kwenye mchakato huu wa Tume. Uchaguzi ni suala la kisiasa, hivyo ni bora chama cha kisiasa kikashiriki ipasavyo ktk mchakato wake na siyo kukimbia kama wafanyavyo CDM.
 
Tume inaundwa.
Ina wajumbe 10.
Mmoja mwandishi wa habari.
Mmoja jaji mstaafu
Mmoja mwanaharakati maarufu
Mmoja kiongozi wa dini (Mkristo)
Mmoja kiongozi wa dini (Muislam)
Mmoja kiongozi mstaafu wa chama cha upinzani
Mmoja kiongozi mstaafu wa chama tawala
Mmoja mhadhiri wa chuo kikuu kimoja
Mmoja mwananchi aliyetambulishwa kama mkulima.
Mmoja mwananchi aliyetambulishwa kama mjasiriamali.

Wananchi wanapiga makofi kwa sababu "hakuna mtu wa serikali hapo."

Wasichojua, watu hao 10 wote ni wa kitengo.

And this is how it works.
Na "baadhi ya washirika wenu katika harakati zenu" wapo kazini.
Yes, that is how it works.
Watu watakubeza lakini ukweli CCM haiwezi kukubali kutoka madarakani kirahisi. Hata kwenye uchaguzi kuna wagombea wengi wa vyama vya upinzani vidogo vidogo ni mamluki/kitengo.
 
Tume huru ya uchaguzi bila katiba mpya ni sawa na kuziba mashimo ya panya kwa mikate!

Maana Tanzania uchaguzi ni mfumo sio tume tu.Nguvu ya Rais na wateule wake, polisi, TISS, Jeshi, Tume, Tamisemi na wengineo lazima viangaliwe kwa pamoja kupitia katiba mpya.

Hiki kinachoitwa ni Tume huru ya uchaguzi ni changa la macho kwa wajinga ambao ndiyo wengi kwenye hii nchi.
 
Back
Top Bottom