Zitto amesema IGP Siro anapaswa kujiuzuru maana amekataa kutii amri ya askari wa mwamvuli wa rais SSH kwa kukataa kumkamata askofu Gwajima.
Na kwa kufanya hivyo Siro amegoma kutii amri toka kwa rais SSH.
Source; StarTV medani za siasa.
Kosa kubwa alilofanya SSH ni kuonyesha woga na kuogopa walioteuliwa na Mwenda zake. Itamkosti sana.
Mwenda zake hakuogopa mtu yeyote hata angekua nani alisema akamatwe na kutiwa ndani na ikiwezekana kutaifisha mali zake alizopata kwa rushwa na wizi. Hii ilisababisha watendaji wake wote wamuogope ndani ya chama na serikali.
Siro alipaswa atenguliwe mara tu baada ya kuwaruhuhusu wanazengo kuweka njama ya kuichafua nchi kwa kubambikia watu kesi za ugaidi na kumfumbia macho Gwajima atumie dini yake kuwa kama mwongozo kwenye nchi isiyofungamana na dini yoyote.
Kuchanganya dini na siasa kwa misimamo mikali ni jambo la hatari kuliko kudai Katiba Mpya.
Dini ya Gwajima imetoka Ulaya sio Usukumani ,namba 666 imetoka ulaya sio usukumani, Covid 19 imetoka China.
Chanjo etoka Ulaya tangu chajo ya ndui.
Sawa leo Gwajima anatumia dini iliyotoka ulaya kupinga wazungu waliompa PhD na elimu ya dini yao.
Yote anayoyahubiri yameandikwa kwenye mitandao ya Wazungu sio Wasukuma wala wangoni wala wachaga.
Mwamko wa makanisa ya Kilokole ulianzia Marekani na sio Usukumani sasa leo ametumia Elimu na dini za kizungu kutajirika anataka kuwaita wazungu ni Mabeberu ,wauaji, wanyama wa 666. Bila kujua kuwa yeye pia ni 666 mkubwa kabisa na mjanja mjanja mpenda fedha na madaraka huku akiwa anazitumia kujilimbikizia mali kwenye kundi la maskini wanaomzunguka.
Ni bora angetokea Mganga wa kienyeji toka Sumbawanga akapinga Chanjo huyo nisingemshangaa.Ningesema ni mzalendo na mwafrika wa asili.