Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amelalamikia hujuma katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Mtambwe, Pemba uliofanyika Oktoba 28, 2023, huku Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ikieleza kushangazwa na madai hayo.
Kulingana na Zitto, hujuma kama hizo ndizo zilizo haribu uchaguzi wa mwaka 2020 na ndio maana wanatarajia kufanya kongamano Desemba 8 mwaka huu kutathmini mwenendo wa Serikali wa Umoja wa Kitaifa (SUK) ndani ya miaka mitatu.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jaji George Joseph Kazi amekanusha kuwepo kwa hujuma katika uchaguzi huo, akisema hawajapokea malalamiko kutoka kwenye chama hicho.