Zitto Kabwe amdhihaki Tundu Lissu kwa kumuita CHIBA. Aomba radhi baada ya kulalamikiwa

Zitto Kabwe amdhihaki Tundu Lissu kwa kumuita CHIBA. Aomba radhi baada ya kulalamikiwa

Hajafurahishwa na kupona kwake.Afu siyo bahati mbaya ni makusudi matupu ona hizo emoji za vicheko na dhihaka.Kumbuka hujafa hujaumbika na aliyemsababishia ivo alipata thawabu yake ivo tuliza mshono Z.
 
Sema nao hawa viongozi wa chadema nao wanamfuatafuata sana zitto. Hawaishi kumtolea maneno ya kukera kila siku hata akinyamaza vp. Wanamfuata katika chama chake, wanamfuata yeye binafsi kila uchwao. Anafuatwa na misukule ya mbowe hadi viongozi misukule km lema, lissu na heche. Watu peke ninaowaona smart kichwani, yaani hawana huu ujinga ujinga wa kumfuatilia zitto kiboyaboya kwa sasa, ni mbowe na angalau mnyika. Mbowe hajasoma sana lkn kina tobo na huyu lema inabidi wasubiri sana kumfikia.

Zitto km binadamu, tena mwenye jinsi ya kiume, anaweza kuudhika na kujikuta anajibu mapigo km hivyo wakati mwingine kutoka na tabia hizo za kidada za kina lema. Wabadilike, waache siasa za kishamba na kizamani hizo.
 
nafikiri ni afadhali ZITO amemtania hivyo ili ufafanuzi juu ya jina chiba utolewe. wengi tulikuwa hatujui kama Tundu Lisu kuitwa Chiba ni kumtania kuhusu ulemavu wake wa mguu tena aliopigwa risasi. hakuzaliwa hivyo na ni kitu kilichompa maumivu yeye na sisi tulio wengi. najua kuanzia sasaivi hilo jina halitatumiwa tena labda na Kigogo2014 aliyelianzisha.
 
Nisingeona radhi yake tena ukiangalia time aliyoandika utaona hata yeye hakujua vyema tafsiri ya hilo neno. Inaweza kutokea kwa yeyote! Mfano nikisema "Zuzu amegoma" wote hapa tunajua maana ya neno Zuzu?

Sometimes kwenye siasa kuna maneno ya kejeli bila hata kujua maana halisi. Mfano Lissu alipenda kumuita JPM "dikteta uchwara" , Mnyika alimuita Kikwete "dhaifu" na wote hakuna aliyewahi kuomba radhi. Hili Zitto kawa muungwana hakuna haja ya kuyakuza zaidi.
Kwa huu mwandiko, wewe Zitto hii ni akaunti yako nyingine.
 
Tujifunze kumuelewa mtu anapoomba radhi.
 
Ameomba radhi! Seems alijua ni jina la utani lakini hakujua linahusishwa na ulemavu. Itakuwa ajabu hili tukitaka kulifanya topic.

Nashauri likomee hapo, kulizungumza zaidi halitamuumiza tu Zitto bali hata ndugu yetu. Mengine tuache yapite.
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Hapana, Sony Chiba alikuwa ni DJ maarufu miaka ya 80, alikuwa ni mlemavu ndio hapo jina hilo Chiba walipobatizwa vilema wengi miaka hiyo. Ni kama vile umuone mlemavu umuite mabaga fresh.
Kwa kumbukumbu zangu, Kama sijasahau neno Chiba limetokana na mwimbaji mwenye asili ya Congo mikataba ya 80 alikua akiimbia bendi moja wapo,kati ya maquis du Zaire au orchestra Safari sound masantula,aliku na ulemavu wa mguu mmoja ulikuwa mfupi.naomba kusahihishwa.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Zitto sasa amevuka mpaka na shime ndugu Tundu usimchekee tena hasa kwa hatua hiyo ya kukudhalilisha kwa kilema chako.

Hii ndiyo Tweet aliyoandika Twitter wakati akijibu hoja ya mdau

Baada ya kulalamikiwa na wadau, Zitto Kabwe aliomba msamaha na kudai kuwa hakuwa anajua maana ya neno ''CHIBA'' kama linamaanisha mlemavu, bali alijua ni maneno ya vijana tu

Nukuu
Kwa kweli sikufahamu kama jina Chiba linahusiana na ulemavu. Nilidhani ni majina ya Vijana ya kutaniana. Mama yangu mzazi alikuwa mlemavu kamwe siwezi kutweza ulemavu wa Mtu. Naomba radhi sana Kwa hili. Hakika Sio Sawa. Uzee umeingia tunapitwa na majina ya mtaani. Mniwie radhi

Ana uzee gani zitto kabwe ni stress tu za siasa zinamsumbua.neno chiba lipo kitambo tu.vijana wazamani wanalijua vyema hilo neno Sony Chiba.
 
Sidhani kama alifanya hivyo kwa makusudi ukizingatia Mama yake alikuwa na Ulemavu.., Na Lissu sio Mlemavu naturally...

Nawashauri wapinzani wote waache kwenda personal na waanze ku-attack issues..,

Hizi gutter politics can only go so far.... Tukumbuke tunajenga nyumba moja...,

Thinking about it....[emoji848]
Au tunabomoa nyumba moja ?
Kama mama yake alikuwa mlemavu lazima atakuwa analijua hilo jina la Chiba.asijetee kachemka kiongozi mkuu.
 
Zitto sasa amevuka mpaka na shime ndugu Tundu usimchekee tena hasa kwa hatua hiyo ya kukudhalilisha kwa kilema chako.

Hii ndiyo Tweet aliyoandika Twitter wakati akijibu hoja ya mdau

Baada ya kulalamikiwa na wadau, Zitto Kabwe aliomba msamaha na kudai kuwa hakuwa anajua maana ya neno ''CHIBA'' kama linamaanisha mlemavu, bali alijua ni maneno ya vijana tu

Nukuu
Kwa kweli sikufahamu kama jina Chiba linahusiana na ulemavu. Nilidhani ni majina ya Vijana ya kutaniana. Mama yangu mzazi alikuwa mlemavu kamwe siwezi kutweza ulemavu wa Mtu. Naomba radhi sana Kwa hili. Hakika Sio Sawa. Uzee umeingia tunapitwa na majina ya mtaani. Mniwie radhi

Huyu siasa kwake zimekua ngum KILA anachopanga hakiendi, amebaki kuwa Chawa, na mtu wa vijembe basi, na mbaya zaidi hujiona bado mwanasiasa machachari kumbe Zama zake zimeisha ,
 
Huyu ni juzi tu alikuja na Quote ya kusema "usimseme vibaya mwenzako kwasababu ya utofauti wenu kwasababu kuna siku mtakuja kuwa marafiki tena na utapata aibu"

Huu sasa ni unafki
ZZK amethibitisha usahaulifu wake.
 
Zitto sasa amevuka mpaka na shime ndugu Tundu usimchekee tena hasa kwa hatua hiyo ya kukudhalilisha kwa kilema chako.

Hii ndiyo Tweet aliyoandika Twitter wakati akijibu hoja ya mdau

Baada ya kulalamikiwa na wadau, Zitto Kabwe aliomba msamaha na kudai kuwa hakuwa anajua maana ya neno ''CHIBA'' kama linamaanisha mlemavu, bali alijua ni maneno ya vijana tu

Nukuu
Kwa kweli sikufahamu kama jina Chiba linahusiana na ulemavu. Nilidhani ni majina ya Vijana ya kutaniana. Mama yangu mzazi alikuwa mlemavu kamwe siwezi kutweza ulemavu wa Mtu. Naomba radhi sana Kwa hili. Hakika Sio Sawa. Uzee umeingia tunapitwa na majina ya mtaani. Mniwie radhi

Haka kasaka fursa kana mambo ya hovyo sana. Baadhi ya wazanzibari washaanza kukashitukia.
 
Kwa kumbukumbu zangu, Kama sijasahau neno Chiba limetokana na mwimbaji mwenye asili ya Congo mikataba ya 80 alikua akiimbia bendi moja wapo,kati ya maquis du Zaire au orchestra Safari sound masantula,aliku na ulemavu wa mguu mmoja ulikuwa mfupi.naomba kusahihishwa.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Sony chiba ni japenese martial artist alikuwa na mguu mfupi aliwika sana miaka ya 80
 
Back
Top Bottom