Zitto Kabwe amdhihaki Tundu Lissu kwa kumuita CHIBA. Aomba radhi baada ya kulalamikiwa

Zitto Kabwe amdhihaki Tundu Lissu kwa kumuita CHIBA. Aomba radhi baada ya kulalamikiwa

Acheni kukaza ubongo sasa. Ashawaomba msamaha na kutaja sababu iliyofanya akafanya hivo. Amekiri na kuomba radhi.

Binafsi nimemsamehe.
 
Inawezekana kuwa vigumu kuamini, lakini Zitto ameonyesha dhahiri kuwa ni LIMBUKENI, kutokana na mambo mengi anayoonyesha siku hizi hadharani.
Naona kuna jambo mhimu linalomsumbua akilini, jambo ambalo hana uwezo wa kulisawazisha ili akili yake itulie.
 
Zito huwa hajiangalii kwenye kioo nafikiri halafu huwa anafikiri ataishi milele kama babake msoga!
 
Anatakiwa ajiuzulu mara moja uongozi wa Jukwaa la Wanasiasa.

Huyu Zitto Kabwe ana dini kweli

Anakosa uhalali na hadhi ya kuwa KIONGOZI WA JUKWAA LA WANASIASA. A leader of such an August body should be of high integrity, inspirational and EMPATHETIC ! Vigezo vyote hivyo ZITTO hana.
 
Kwa kumbukumbu zangu, Kama sijasahau neno Chiba limetokana na mwimbaji mwenye asili ya Congo mikataba ya 80 alikua akiimbia bendi moja wapo,kati ya maquis du Zaire au orchestra Safari sound masantula,aliku na ulemavu wa mguu mmoja ulikuwa mfupi.naomba kusahihishwa.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app

Ni sawa nilipewa hadithi hii ni uncle wangu alikuwa mpenzi wa muziki zama hizo nikiwa mtoto sana.
 
Sema nao hawa viongozi wa chadema nao wanamfuatafuata sana zitto. Hawaishi kumtolea maneno ya kukera kila siku hata akinyamaza vp. Wanamfuata katika chama chake, wanamfuata yeye binafsi kila uchwao. Anafuatwa na misukule ya mbowe hadi viongozi misukule km lema, lissu na heche. Watu peke ninaowaona smart kichwani, yaani hawana huu ujinga ujinga wa kumfuatilia zitto kiboyaboya kwa sasa, ni mbowe na angalau mnyika. Mbowe hajasoma sana lkn kina tobo na huyu lema inabidi wasubiri sana kumfikia.

Zitto km binadamu, tena mwenye jinsi ya kiume, anaweza kuudhika na kujikuta anajibu mapigo km hivyo wakati mwingine kutoka na tabia hizo za kidada za kina lema. Wabadilike, waache siasa za kishamba na kizamani hizo.
Wewe ni miongoni mwa Mazuzu mliojaza makaeatasi nyumbani mkidani mmeelimika kumbe wajinga wakubwa. Kuwait'a watu Misukule na kusema wenzio hawajasoma huko kusoma kunaishia kiwango gani cha elimu?

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
 
Ameomba radhi! Seems alijua ni jina la utani lakini hakujua linahusishwa na ulemavu. Itakuwa ajabu hili tukitaka kulifanya topic.

Nashauri likomee hapo, kulizungumza zaidi halitamuumiza tu Zitto bali hata ndugu yetu. Mengine tuache yapite.
Hivi kwa nafasi ya mtu kama Zitto ni kweli anaweza kutumia neno asilolijua maana yake?
 
Zitto sasa amevuka mpaka na shime ndugu Tundu usimchekee tena hasa kwa hatua hiyo ya kukudhalilisha kwa kilema chako.

Hii ndiyo Tweet aliyoandika Twitter wakati akijibu hoja ya mdau


Baada ya kulalamikiwa na wadau, Zitto Kabwe aliomba msamaha na kudai kuwa hakuwa anajua maana ya neno ''CHIBA'' kama linamaanisha mlemavu, bali alijua ni maneno ya vijana tu

Nukuu
Kwa kweli sikufahamu kama jina Chiba linahusiana na ulemavu. Nilidhani ni majina ya Vijana ya kutaniana. Mama yangu mzazi alikuwa mlemavu kamwe siwezi kutweza ulemavu wa Mtu. Naomba radhi sana Kwa hili. Hakika Sio Sawa. Uzee umeingia tunapitwa na majina ya mtaani. Mniwie radhi

Duh...!.
Mkuu Zitto , ukipata muda, endelea kupitia bandiko hili, na uyafanyie kazi mapungufu yaliyoainishwa.

P
 
Inawezekana attacks anazopewa Zitto siku za karibuni zimemvuruga ameamua kufunguka kwa namna aliyofanya, atibue makusudi kisha aombe radhi.

Lakini pia inawezekana sababu aliyoitoa Zitto binafsi ni ya kweli, hakujua maana halisi ya hilo neno hasa ukizingatia neno lenyewe ni moja kati ya yale yanayozuka mitaani kila kukicha.

Hivyo basi, kwa upande wangu naona bora nikubaliane na sababu ya Zitto kwamba hakujua maana ya hilo neno, kwani kistaarabu mtu akikukosea halafu usipoikubali samahani yake ni wewe mkosewaji ndie utakuwa na matatizo, sio yeye mkosaji.
Sawa shaibu katibu mkuu
 
Back
Top Bottom