Kipangaspecial
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 20,778
- 28,722
Jibu hoja kwa hoja.Huu sasa ni ukichaa!
Huyu mtu anazidi kuonyesha uhayawani alionao kichwani.
Na hawa ndio viongozi wanaotegemewa kuivusha Tanzania?
BURE KABISA.
Katiba ni ya raia siyo vyama vya siasa...." Yeyote yule anayefikiri kuwa Tanzania itapata katiba mpya bila kwanza kuwa na Tumehuru ya uchaguzi hana ubongo" Zitto
Kwani ile rasimu ya katiba ya warioba ni akina nani walioikwamisha ? Na watashindwaje kuikwamisha tena ? Ni mbinu gani itatumika ili wale jamaa wasiwe na nguvu kisheria kukwamisha huo mchakato ? Kwa sababu unadeal na watu wale wale ambao hutumia ile principle ya collective responsibility !! Sorry inawezekana upeo wangu ni mdogo katika hili jambo !! Lakini !!? Mmmh !!Hapana.
Ni wazi/dhahiri, sheria mama (Katiba), ndiyo inayotoa maelekezo namna ya kupata Tume Huru. Hapa hakuna mkanganyiko wa aina yoyote ile.
Hapo sasa !! Hili suala halitaki kudhihakiana wala kutukanana inatakiwa watu wachemshe bongo kweli kweli, maana kama ule mchakato wa katiba ulikwamishwa kipindi kile itashindikana vipi kukwamishwa tena mara hii ?? Kwa sababu sheria zitakazotumika kuendesha zoezi hilo ni zile zile za wakati ule !! Labda kwanza zibadilike zile sheria !!!Jibu hoja kwa hoja.
Kama ubongo wako unafanya kazi, elezea kwanini ni muhimu kuanza na Katiba mpya ambayo mwisho wa siku itapigiwa kura na zoezi hilo litasimamiwa tume ile ile mnayosema haipo huru ?
Kuna vijana wenzetu wanabeba chuki ambazo haziwahusu.Hapo sasa !! Hili suala halitaki kudhihakiana wala kutukanana inatakiwa watu wachemshe bongo kweli kweli, maana kama ule mchakato wa katiba ulikwamishwa kipindi kile itashindikana vipi kukwamishwa tena mara hii ?? Kwa sababu sheria zitakazotumika kuendesha zoezi hilo ni zile zile za wakati ule !! Labda kwanza zibadilike zile sheria !!!
Hapo umeiona hoja ipi aliyoiweka Zitto?Jibu hoja kwa hoja.
Kama ubongo wako unafanya kazi, elezea kwanini ni muhimu kuanza na Katiba mpya ambayo mwisho wa siku itapigiwa kura na zoezi hilo litasimamiwa tume ile ile mnayosema haipo huru ?
Hauwezi kusema kuna watu wanahodhi mjadala wakati hauzuiwi kuchangia. Aidha, dhana ya kuwa taifa lote lazima lihusishwe sio sahihi. Constitution ya Marekani iliandikwa na James Madison na rafiki zake wasiozidi sita, wote matajiri, wazungu na wanaume. Katiba ya India ilipitishwa na Bunge maalum lililoundwa kwa madhumuni ya hayo mwaka 1947. Dr. Ambedkar ndie anapewa sifa ya kuiandika.Issue ya ku demand Katiba Mpya kwenye jamii ya watu walioelimika haipaswi kuhodhiwa na chama fulani cha siasa. Ukiona maelezo yamejikita kwenye uchadema au uzambarau ujue kama taifa bado hatujajua nini cha kufanya.
Hapana, upeo wako si mdogo.Kwani ile rasimu ya katiba ya warioba ni akina nani walioikwamisha ? Na watashindwaje kuikwamisha tena ? Ni mbinu gani itatumika ili wale jamaa wasiwe na nguvu kisheria kukwamisha huo mchakato ? Kwa sababu unadeal na watu wale wale ambao hutumia ile principle ya collective responsibility !! Sorry inawezekana upeo wangu ni mdogo katika hili jambo !! Lakini !!? Mmmh !!
Kwani Zitto kajibu kwa hoja gani, ya ubongo?Jibu hoja kwa hoja.
Kama ubongo wako unafanya kazi, elezea kwanini ni muhimu kuanza na Katiba mpya ambayo mwisho wa siku itapigiwa kura na zoezi hilo litasimamiwa tume ile ile mnayosema haipo huru ?
Kwa bahati mbaya sana 'ACT' sasa wanaonekana kulikoroga, kiasi kwamba hiyo sifa unayowapa haistahili. Wakishikilia msimamo huu wa sasa itakuwa vigumu sana kuwatenganisha na wafadhiri wao wakuu CCM.Hauwezi kusema kuna watu wanahodhi mjadala wakati hauzuiwi kuchangia. Aidha, dhana ya kuwa taifa lote lazima lihusishwe sio sahihi. Constitution ya Marekani iliandikwa na James Madison na rafiki zake wasiozidi sita, wote matajiri, wazungu na wanaume. Katiba ya India ilipitishwa na Bunge maalum lililoundwa kwa madhumuni ya hayo mwaka 1947. Dr. Ambedkar ndie anapewa sifa ya kuiandika.
Mimi binafsi nawashukuru Chadema na ACT kwa kuhakikisha hoja hii inabakia kuwa hai.
Amandla...
Kwa wakristo unaanza na Biblia ndipo unakutana na mgawanyiko wa vitabu.Agano la kale na Agano jipya.Kweli Zitto umefikia uwezo huu mdogo wa kufikiria? Hiyo tumehuru lazima iwe backed na sheria mama ambayo ni katiba, pasipo katiba mpya tume huru sahau.
Kumbuka katiba inasema rais akishatangazwa matokeo hayawezi kupingwa.
Sheria za uchaguzi zipo hovyo na hivyo kupelekea uundwaji wa tume kuwa hovyo.
Tume ni subset ya katiba na katiba sio subset ye tume. Hivyo katiba kwanza ndio tumehuru.
Hapana, upeo wako si mdogo.
Umeuliza maswali sahihi kabisa ambayo yanahitaji majibu.
Ninaloweza kukupa sasa hivi ni hili: Hiyo rasimu ya Warioba ni mfano mzuri sana wa makosa ambayo hayatakiwi kuendelea kufanyika; yaani kuendelea kuruhusu chama kimoja CCM ndicho kiwe na uamzi wa kila kitu kifanyike au kisifanyike. Ile rasimu ilikuwa inaendeshwa chini ya CCM na serikali yake. Walipoona maslahi yao yapo hatarini, wakaizima haraka bila hata ya kujali gharama zilizotumika hadi hapo rasimu hiyo ilipofikia.
Ni muhimu kabisa makosa kama hayo yasirudiwe tena katika kutengeneza katiba mpya. Pasiwe na chama chochote cha siasa kinachoweza kuingilia mchakato wa katiba hiyo.
Kenya waliweza, kwa nini tusiangalie wao walifanyaje?
Jikite kujibu swali languKwani Zitto kajibu kwa hoja gani, ya ubongo?
Wana uhuru wa kutoa mawazo. Wanaotofautiana nao wana haki vile vile ya kuwapinga na kuonyesha mapungufu yaliyomo katika msimamo wao. Uzuri wa wao kuwa na msimamo huo umewafanya wengi kuchambua kwa dhati dhana ya Tume Huru kabla ya Katiba Mpya. Baadhi yetu tumejifunza mengi kutokana na mjadala huo ambao usingekuwepo kama wote wangekubaliana.Kwa bahati mbaya sana 'ACT' sasa wanaonekana kulikoroga, kiasi kwamba hiyo sifa unayowapa haistahili. Wakishikilia msimamo huu wa sasa itakuwa vigumu sana kuwatenganisha na wafadhiri wao wakuu CCM.
Hujui?Hivi katiba mpya inasaidiaje wapinzani kupata madaraka?!