Zitto Kabwe: Anayefikiri Tanzania itapata Katiba Mpya bila kwanza kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi hana ubongo

Huu sasa ni ukichaa!

Huyu mtu anazidi kuonyesha uhayawani alionao kichwani.

Na hawa ndio viongozi wanaotegemewa kuivusha Tanzania?

BURE KABISA.
Jibu hoja kwa hoja.

Kama ubongo wako unafanya kazi, elezea kwanini ni muhimu kuanza na Katiba mpya ambayo mwisho wa siku itapigiwa kura na zoezi hilo litasimamiwa tume ile ile mnayosema haipo huru ?
 
Hapana.

Ni wazi/dhahiri, sheria mama (Katiba), ndiyo inayotoa maelekezo namna ya kupata Tume Huru. Hapa hakuna mkanganyiko wa aina yoyote ile.
Kwani ile rasimu ya katiba ya warioba ni akina nani walioikwamisha ? Na watashindwaje kuikwamisha tena ? Ni mbinu gani itatumika ili wale jamaa wasiwe na nguvu kisheria kukwamisha huo mchakato ? Kwa sababu unadeal na watu wale wale ambao hutumia ile principle ya collective responsibility !! Sorry inawezekana upeo wangu ni mdogo katika hili jambo !! Lakini !!? Mmmh !!
 
Jibu hoja kwa hoja.

Kama ubongo wako unafanya kazi, elezea kwanini ni muhimu kuanza na Katiba mpya ambayo mwisho wa siku itapigiwa kura na zoezi hilo litasimamiwa tume ile ile mnayosema haipo huru ?
Hapo sasa !! Hili suala halitaki kudhihakiana wala kutukanana inatakiwa watu wachemshe bongo kweli kweli, maana kama ule mchakato wa katiba ulikwamishwa kipindi kile itashindikana vipi kukwamishwa tena mara hii ?? Kwa sababu sheria zitakazotumika kuendesha zoezi hilo ni zile zile za wakati ule !! Labda kwanza zibadilike zile sheria !!!
 
Kuna vijana wenzetu wanabeba chuki ambazo haziwahusu.
 
Jibu hoja kwa hoja.

Kama ubongo wako unafanya kazi, elezea kwanini ni muhimu kuanza na Katiba mpya ambayo mwisho wa siku itapigiwa kura na zoezi hilo litasimamiwa tume ile ile mnayosema haipo huru ?
Hapo umeiona hoja ipi aliyoiweka Zitto?

Hivi wewe hata kusoma yaliyoandikwa kwenye mada hii pekee ili upate jibu bado unaona shida?

Majibu yametolewa humu humu, bado unataka nikushike mkono kukuonyesha majibu ya swali lako yalipo?

Katiba ndiyo sheria mama inayoelekeza kila kitu, hata namna ya kuipata hiyo tume huru..., hilo wewe hulioni?

Utapata vipi tume huru ambayo unategemea itafanya kazi zake kwa uhuru katika mfumo usioruhusu huo uhuru? Hivi nyinyi watu wengine akili zenu mmeziweka wapi?
 
Issue ya ku demand Katiba Mpya kwenye jamii ya watu walioelimika haipaswi kuhodhiwa na chama fulani cha siasa. Ukiona maelezo yamejikita kwenye uchadema au uzambarau ujue kama taifa bado hatujajua nini cha kufanya.
Hauwezi kusema kuna watu wanahodhi mjadala wakati hauzuiwi kuchangia. Aidha, dhana ya kuwa taifa lote lazima lihusishwe sio sahihi. Constitution ya Marekani iliandikwa na James Madison na rafiki zake wasiozidi sita, wote matajiri, wazungu na wanaume. Katiba ya India ilipitishwa na Bunge maalum lililoundwa kwa madhumuni ya hayo mwaka 1947. Dr. Ambedkar ndie anapewa sifa ya kuiandika.
Mimi binafsi nawashukuru Chadema na ACT kwa kuhakikisha hoja hii inabakia kuwa hai.

Amandla...
 
Kwani ile rasimu ya katiba ya warioba ni akina nani walioikwamisha ? Na watashindwaje kuikwamisha tena ? Ni mbinu gani itatumika ili wale jamaa wasiwe na nguvu kisheria kukwamisha huo mchakato ? Kwa sababu unadeal na watu wale wale ambao hutumia ile principle ya collective responsibility !! Sorry inawezekana upeo wangu ni mdogo katika hili jambo !! Lakini !!? Mmmh !!
Hapana, upeo wako si mdogo.

Umeuliza maswali sahihi kabisa ambayo yanahitaji majibu.

Ninaloweza kukupa sasa hivi ni hili: Hiyo rasimu ya Warioba ni mfano mzuri sana wa makosa ambayo hayatakiwi kuendelea kufanyika; yaani kuendelea kuruhusu chama kimoja CCM ndicho kiwe na uamzi wa kila kitu kifanyike au kisifanyike. Ile rasimu ilikuwa inaendeshwa chini ya CCM na serikali yake. Walipoona maslahi yao yapo hatarini, wakaizima haraka bila hata ya kujali gharama zilizotumika hadi hapo rasimu hiyo ilipofikia.

Ni muhimu kabisa makosa kama hayo yasirudiwe tena katika kutengeneza katiba mpya. Pasiwe na chama chochote cha siasa kinachoweza kuingilia mchakato wa katiba hiyo.

Kenya waliweza, kwa nini tusiangalie wao walifanyaje?
 
Jibu hoja kwa hoja.

Kama ubongo wako unafanya kazi, elezea kwanini ni muhimu kuanza na Katiba mpya ambayo mwisho wa siku itapigiwa kura na zoezi hilo litasimamiwa tume ile ile mnayosema haipo huru ?
Kwani Zitto kajibu kwa hoja gani, ya ubongo?
 
Hauwezi kusema kuna watu wanahodhi mjadala wakati hauzuiwi kuchangia. Aidha, dhana ya kuwa taifa lote lazima lihusishwe sio sahihi. Constitution ya Marekani iliandikwa na James Madison na rafiki zake wasiozidi sita, wote matajiri, wazungu na wanaume. Katiba ya India ilipitishwa na Bunge maalum lililoundwa kwa madhumuni ya hayo mwaka 1947. Dr. Ambedkar ndie anapewa sifa ya kuiandika.
Mimi binafsi nawashukuru Chadema na ACT kwa kuhakikisha hoja hii inabakia kuwa hai.

Amandla...
Kwa bahati mbaya sana 'ACT' sasa wanaonekana kulikoroga, kiasi kwamba hiyo sifa unayowapa haistahili. Wakishikilia msimamo huu wa sasa itakuwa vigumu sana kuwatenganisha na wafadhiri wao wakuu CCM.
 
Kweli Zitto umefikia uwezo huu mdogo wa kufikiria? Hiyo tumehuru lazima iwe backed na sheria mama ambayo ni katiba, pasipo katiba mpya tume huru sahau.

Kumbuka katiba inasema rais akishatangazwa matokeo hayawezi kupingwa.

Sheria za uchaguzi zipo hovyo na hivyo kupelekea uundwaji wa tume kuwa hovyo.

Tume ni subset ya katiba na katiba sio subset ye tume. Hivyo katiba kwanza ndio tumehuru.
Kwa wakristo unaanza na Biblia ndipo unakutana na mgawanyiko wa vitabu.Agano la kale na Agano jipya.
Zitto ni MZITO kumeng'enya mambo.
 
Hapana, upeo wako si mdogo.

Umeuliza maswali sahihi kabisa ambayo yanahitaji majibu.

Ninaloweza kukupa sasa hivi ni hili: Hiyo rasimu ya Warioba ni mfano mzuri sana wa makosa ambayo hayatakiwi kuendelea kufanyika; yaani kuendelea kuruhusu chama kimoja CCM ndicho kiwe na uamzi wa kila kitu kifanyike au kisifanyike. Ile rasimu ilikuwa inaendeshwa chini ya CCM na serikali yake. Walipoona maslahi yao yapo hatarini, wakaizima haraka bila hata ya kujali gharama zilizotumika hadi hapo rasimu hiyo ilipofikia.

Ni muhimu kabisa makosa kama hayo yasirudiwe tena katika kutengeneza katiba mpya. Pasiwe na chama chochote cha siasa kinachoweza kuingilia mchakato wa katiba hiyo.

Kenya waliweza, kwa nini tusiangalie wao walifanyaje?
 
Katiba mpya ya muungano wenye kero chungu mzima ni kupoteza muda na hela za kodi. Wabara wanataka serikali 3 za muungano, Wazanzibari wanataka kurudisha sovereignity. Katiba mpya itakataliwa tuu baada ya muda kwa sababu pande mbili zinatofautiana. Wengi mnalazimisha vitu ambavyo haviendi na mwisho wake ni vurugu.
 
Huyu mbona siku zinavyoenda anazidi kutoeleweka na kuwehuka, Hiyo Tume Huru waliyoipata huko Zanzibar kwenye Maridhiano ya Chama chake na CCM iliwasaidia nini kwenye Uchaguzi wa 2020 au ule alioufuta Jecha.

Wenzake wameshamwambia Uchaguzi ni Issue ya Dola siyo Tume ya Uchaguzi peke yake ndiyo maana hadi Jeshi la Polisi linahusishwa kwenye mambo ya Hovyo bila Katiba Mpya hiyo Tume Huru anayoitaka haitakuwa Huru kwenye Urais wa Kifalme.

Anatumika vibaya sana huyu.
 
Kwa bahati mbaya sana 'ACT' sasa wanaonekana kulikoroga, kiasi kwamba hiyo sifa unayowapa haistahili. Wakishikilia msimamo huu wa sasa itakuwa vigumu sana kuwatenganisha na wafadhiri wao wakuu CCM.
Wana uhuru wa kutoa mawazo. Wanaotofautiana nao wana haki vile vile ya kuwapinga na kuonyesha mapungufu yaliyomo katika msimamo wao. Uzuri wa wao kuwa na msimamo huo umewafanya wengi kuchambua kwa dhati dhana ya Tume Huru kabla ya Katiba Mpya. Baadhi yetu tumejifunza mengi kutokana na mjadala huo ambao usingekuwepo kama wote wangekubaliana.

Amandla...
 
Back
Top Bottom