Mgombea wa CCM jimbo la Kigoma mjini, Kilumbe Ng'enda ametangazwa mshindi baada ya kupata kura 27, 688 huku Zitto Kabwe wa ACT Wazalendo akipata kura 20, 600. Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi, jimbo hilo Mwailwa Pangani amesema kura zilizopigwa ni 50268.
Zitto: Licha ya kuingiza kwenye vituo kura zilizokwishapigwa zipatazo 15,850 (kura 50 kila Kituo cha kupigia kura ) nimemshinda Mgombea wa CCM kwa kura 5218. Hata hivyo Mgombea wa CCM katangazwa mshindi kwa tofauti ya kura 7000. Tunafungua ukurasa Mpya wa mapambano ya demokrasia nchini.- Zitto Kabwe.