Zitto Kabwe asubiriwa na Bunge kueleza lengo la barua yake Benki ya Dunia kuzuia mkopo wa kuboresha Elimu (SEQUIP)

My take huyu jamaa anayejiita Zitto sisi wananchi wa Kigoma tutamuadhibu kwenye sanduku la kura.
Wakati mwingine watu wanakuwa kama hawana akili.

Mtetezi wa wanyonge, wanafunzi wanazuiwa kwenda shule, wanahabari wanao nyanyaswa, uhuru wa kufanya siasa, uhuru wa kujieleza na hakiza binadamu .

halafu mtu anamchukia.


Hivi watanzania nani aliyetuloga?
 
Yeye anaenda kupiga kelele nje ya nchi! Kumbe Zitto anapiga kelele na kelele huwa hazisikilizwi kwani hazina tija sasa anazihangaikia nini? Bunge litaacha mambo muhimu ya maana na kushughulikia kelele zisizo na tija za Zitto!
Ndugai toka lini Bunge likasikiliza na kujadili hoja za upinzani na kuzikubali! Bunge hili la CCM? Haiwezekani.
 
Usaliti ni nini?

Unajuaje huyu ni msaliti na huyu anafanya upinzani unaotetewa kikatiba?

Zitto kafanya usaliti kivipi na kwa nini unafikiri ni usaliti na si upinzani wa kisiasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwambie Lema aandike barua akiomba Chadema inyimwe mkopo.

Hiyo siku unyumbu utakutoka na utaanza kuelewa ni maana ya usaliti na msaliti ni nani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zitto amemjibu Ndugai hivi...
 
Nimeshangazwa sana na kauli ya spika wa bunge bwana Ndugai kusema kuwa mbunge Zitto Kabwe amezuia mkopo kutoka World Bank kauli iliyopingana vikali na maelezo yaliyotolewa na rais na wateule wake wengine waliosisitiza kuwa hatujanyimwa mkopo na WB.

Hivi hii imekaaje jamani mbona kama vile sielewi.
 
Maandalizi ya kumuuza mtu wa kumchalenji mkulu wakati wa uchafuzi, ili ionekane uchafuzi ulikuwa wa kidomo cha korasia. Hivyo mtu anauzwa kwa watu, wamuone mmoja wao(mtetezi wa wanyongwa).
 
Kazi za mbunge zimeainishwa wapi na ni zipi?

Kwa nini mbunge kuwasiliana na benki ya dunia si sehemu ya kazi za mbunge?

Wapi imeandikwa hivyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni mojawapo ya kazi za Bunge ndiyo, ila Ofisi ya Bunge ikiwa ina taarifa, na imeridhia. Siyo mtu analipuka tu kutoka jimboni kwake anaadika barua tena ya kipumbavu, kisa ni mbunge. Wenye roho kama yangu Mungu apishie mbali asitupatie mamlaka. Hii issue ukinipa mimi halafu nina mamlaka, lazima mtu awaeleze vizuri watanzania alikuwa na nia gani
 
Kwa hiyo Serikali imuombe Zito Kabwe na akubali kuiambia WB iachie fedha, vinginevyo hakuna mkopo kutoka WB mpaka Zito Kabwe aridhike kwamba kama serikali ,,mmejirekebisha” na Jimbo lake la Kigoma Ubunge mmuachie vinginevyo no money, Duh!
 
Ni sawa unachosema. Na kwa mantiki hiyo alitakiwa aandike barua kama Zitto au kama Kiongozi wa ACT wazalendo, na si kama Mbunge wa Bunge la JMT.
 
Sema mtalazimisha ushindi. Lakini hilo halitawasaidia, unadhani anahitaji kuwa bungeni ili atoe maoni yake na kusikilizwa? Tutaanzisha petition ya bidhaa za Tanzania kususiwa kimataifa hadi mshike adabu. Na sio kazi kubwa sana.
Hahaha wabongo bhana, hapa unaona utawakomesha ccm?
 
Kwanini Mh Ndugai ni msahaulifu kivile?? Ameshasahau alichomtendea Mh Tundu Lissu?? Au yeye hakuwa Mbunge na angehitaji majadiliano kabla??

Tuyaache hayo je si anafahamu kiini cha haya yote? Nani alitoa kauli za kibaguzi juu ya elimu kwa wasichana wetu wanaokatiza elimu yao kwa ujauzito?? Aliwahi kumtaka mtu huyo kutoa ufafanuzi juu ya kauli ile??

Je si wazi kuwa Bunge letu haliko Huru?? Je Mh ZZK angelileta Bungeni angelipitisha lijadiliwe?? Au kasahau alipoambiwa na Mkuu wa ule Mhimili iliojichimbia chini zaidi ya mingine kuwa awatimue mle Mjengoni palipo na kinga ili wakose pakusemea waje warokokee nje ili ni deal nao??

Mimi ningemshauri Mh Ndugai asimamie Bunge kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Bunge. Akiona anaingiliwa aweke wazi na akishindwa akae pembeni kulinda heshima yake na hadhi ya Bunge. Hata hili la kumuandikia barua Mh ZZK ni kuendelea kujidhalilisha na kujianika Kimataifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni bonge la mpumbavu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Filipo humu tunajadili hoja matusi ni dalili ya kutokuwa na hoja, sasa na yeye akujibu kwa tusi? Ili na wewe umjibu kwa tusi? Na yeye akutusi? Jibu kwa hoja labda tu haukubali Uhuru wa mtu kutoa maoni take popote pale duniani. Wewe kama unaona haki hiyo haikufai basi kaa kimya waachie wanaojitambua.
 
Interest,
Mie napendekeza tutume jopo la majadiliano liende world bank wakawaeleze kwanini huo mkopo Ni muhimu, waende Prof kabudi Prof ndalichako, Dr mahiga, Prof mchome, na Prof Tibaijuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…