Zitto Kabwe atoa hoja nzito juu ya uwekezaji wa DP World Tanzania

Hakuna hoja yoyote! Mshauza bandari yetu kwa ndugu zenu waarabu. Hata kwenye gesi mlikuja na porojo za aina hii hii. Mwisho wa siku hata wamiliki wake hatuwajui.
Hakuna Bandari iliyouzwa, au ulipata mgao?
 
Tunayo sheria ya single source, hatuna haja ya kutangaza tena muda mwingine tunaweza kuamua tu.

Bandari inatafutiwa mwekezaji ambaye ataiendesha na kuiendeleza. Vitu vya kawaida kabisa.
 
Hivi unaongelea habari ya MOU wakati vipengere vya mkataba vimeshajitanaibisha? Au unabebwa na upepo wa Zitto?
Skia mkuu na uache upotoshaji wewe na Zitto wako.
MAMBO YASIYOFAA KABISA MKATABA WA BANDARI.

1. TANZANIA HAIRUHUSIWI KUJITOA KWENYE MKATABA

Ibara ya 23(4) ya mkataba huo inakataza wahusika wa mkataba ambao ni serikali ya Tanzania na Kampuni mwekezaji DPW kujitoa(Denounce) katika mkataba, Kuvunja, Kuahirisha(suspend), au Kusitisha(terminate).

Na ni masikitiko sana kuwa ibara hii imesisitiza kuwa haturuhusiwi kujitoa kwenye mkataba huu hata kama kuna ukiukwaji mkubwa wa masharti(Material Breach), hata kama kuna mabadiliko makubwa ya kimazingira katika utekelezaji wa mkataba(fundamental change of circumstances), hata kama kuna mgogoro mkubwa wa kidiplomasia(severe diplomatic/condular dispute), au sababu zo,ote zile zinazotambulika na sheria za kimataifa.

Maneno haya yameandikwa hivihivi kwenye huo mkataba. Si mlisema ule Fei toto, sasa upo huu mbele yenu.

2. MKATABA HAUNA MUDA

Ibara ya 23 ya mkataba inasema kuwa ukomo wa mkataba huu ni mpaka shughuli za mradi zitakapokuwa zimekamilika. Maneno haya yameandikwa hivihivi.

Serikali inawajibika kutoa maelezo kuhusu hili. Katika sheria hakuna mkataba usio na muda isipokuwa mkataba wa kuuza au kununua tu.

Ukimuuzia mtu kitu haumwambii tumia mpaka muda fulani, ni moja kwa moja. Je na huu mkataba ni hivyo ??.

3. MIGOGORO KUHUSU MRADI KUTATULIWA AFRIKA KUSINI.

Ibara ya 20 ya mkataba inasema migogoro kuhusu mkataba wa mradi utatatuliwa Johannesburg Afrika Kusini na Sheria itakayotumika ni sheria za umoja wa mataifa UNICITRAL Arbitration Rules.

Kumbuka mwaka 2017 tulitunga sheria yetu kwa ajili ya kulinda rasimali zetu.

Katika sheria hii The Natural Wealth and Resources , Parmanent Sovereignty Act 2017, tuliweka wazi katika kifungu cha 11 kuwa Migogoro yoye inayohusu Rasilimali za Taifa hili itatatuliwa na vyombo vya hapa nchini kwa sheria zetu.

Na hiii ilikuja baada ya kuonekana hawa wanaojiita wawekezaji wanatunyonya kisha tukilalamika wanatuburuza kwenye vyombo vyao tena kwa sheria zao.

Unamshitaki mtu kwenye mahakama yake mwenyewe kwa kutumia sheria alizotunga yeye mwenyewe, halafu unategemea upate haki.

Tulitunga sheria hii kujikomboa na huu ukoloni. Mkataba huu sasa unataka kuturudisha huko.

4. TANZANIA HAINA MAMLAKA YA KUTAIFISHA MALI ZA MWEKEZAJI.

Ibara ya 14 ya mkataba inakataa kabisa Serikali ya Tanzania kutaifisha mali yoyote ya mwekezaji.

Yaani hakuna sababu yoyote iwe ya kimadai au kijinai itakayoifanya serikali itaifishe mali ya mwekezaji.

Mnajua kuwa suala la kutaifisha lipo kisheria hasa inapothibitika jinai. Lakini hii si kwa mwekezaji wa Bandari.

Ibara hii inasisitiza kuwa endapo itatokea mali zao kutaifishwa na serikali basi fidia na stahiki ya kuridhisha italipwa na serikali. Neno STAHIKI YA KURIDHISHA limetumika hivyohivyo kwenye mkataba.

Hatujui hiyo ya kuridhisha itakuwa ni kiasi gani lakini limeandikwa hivyohivyo.

5. KUTUNGA SHERIA MPYA.

Ibara ya 27 inasema baada ya mkataba kusainiwa Tanzania haitakuwa na mamlaka ya kutunga sheria, kanuni mpya ambayo itapingana na mkataba.

Tafsiri yake, kama mna marekebisho yenu ya kikodi, sera pengine kutokana namabadiliko na mda kupita hamtaruhusiwa.

Uchambuzi utaendelea.
 
Kwa huu mlolongo wa ujinga ulioandika hapa, nakujibu kama ifuatavyo.

Kwanza hakuna Mkataba, mkataba hadi azimio la Bunge Baada ya 10th June, baada ya hapo ridhaa itatoka kwenda kujadili kati ya TPA na DP World, ikishindikana ndani ya miezi 12, mkataba unakufa. So Usiwe mjinga kiasi hicho.
 
kubwa ni mashaka ya serikali uwa inaingi mikataba ya ajabu mno huku taifa likipata maslahi kidogo.
 
Sijasoma mkataba huu ila nimesoma nikataba mingi amabyo selikali ya Tanzania imeingia...ni mikataba ya kishenzi sana mikata mibovu kuwahi kuiona.....

Hofu ni juua ya bunge ambalo...litapitisha hii mikataba ..ni bunge lq hovyo mnooo

Huu mkataba Kuna vitu havipo sawa hata kama sijausoma
 
Tunayo sheria ya single source, hatuna haja ya kutangaza tena muda mwingine tunaweza kuamua tu.

Bandari inatafutiwa mwekezaji ambaye ataiendesha na kuiendeleza. Vitu vya kawaida kabisa.

..nafahamu hiyo sheria ya single source ipo.

..lakini kwa suala hili la bandari naamini sheria hiyo inatumika kama kichaka cha upigaji.

..mimi sipingi bandari kutafutiwa muwekezaji ili kuboresha huduma zake.

..lakini ni vizuri serikali ikasema inatafuta muwekezaji wa aina gani.

..Je, serikali inauza bandari, inakodisha, inatafuta mbia, au management company?

..Kwanini serikali haitoi majibu ya uhakika?

..Zitto, Musukuma, Kibaji, Hamad Rashid, ndio wamekuwa wasemaji wa serikali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…