Watu wa mikoa ya pembezoni huwa wananyanyapaliwa sana kwa kubambikiwa uraia wa nchi jirani.
Zitto yuko sahihi kukasirika
Hilo ni tatizo la ccm, walianza enzi za Mkapa kutumia fimbo ya uraia kuwapiga wanaowakosoa. Basi. Yaani mtu anayeikosoa serkali ya ccm atazushiwa siyo raia. Alianza Jenerali Ulimwengu ambaye aliikosoa sana serikali ya ccm enzi ya Mkapa, kwa ubinafsishaji wa kifisadi, na mikataba ya kifisadi ya madini.
Ulimwengu akatangazwa siyo raia. Kwa wale wasiofahamu, Jenerali Ulimwengu ni msomi mahiri. Alisoma sheria chuo kikuu cha Dar enzi hizo siasa za ukombozi zimepamba moto. Yeye na wenzake, walidiriki kushiriki vita mstari wa mbele kule Msumbiji, kuiunga mkono FRELIMO.
Baada ya masomo nadhani alifanya kazi Daily News, chini ya Mkapa, na kuna wakati alikuwa Algeria, kama coordinator wa umoja wa vijana Afrika. Baada ya hapo alirudi Tanzania na akawa DC nadhani hapa Dar. Nakumbuka alikuwa mmoja wabunge (G. 55?) Waliounga mkono serikali tatu enzi hizo. Baadaye aliachana na active politics akarudia fani ya magazeti, akiwa na gazeti la Rai, baadae Dimba na Mtanzania. Baada ya Nyerere kuachana na urais, akiwa kwenye Tume ya mataifavya kusino, South Commission, alimtumia sana Ulimwengu kama mkalimani katika lugha ya Kifaransa, wakati akiwa mpatanishi katika mataifa mbalimbali
Uchaguzi Mkuu wa 1995 alitumia gazeti lake la Rai kumpigia kampeni kali Mkapa, akiwa na wenzake kina Johnson Mbwambo. Nakumbuka siku anatangaza kuingia kinyan'ganyiro cha Urais, Mkapa alizungukwa na watu wawili. Upande mmoja Mark Bomani (kama sikosei) na upande wa pili Jenerali Ulimwengu.
Baada ya kushinda, Ulimwengu alipewa fursa kadhaa kuiwakilisha nchi katika forum kadhaa za kimataifa. Lakini mara Mkapa alipoanza sera za ubinafsishaji holela, wakasigana na Ulimwengu, ambaye alitumia tena magazeti yaleyale yaliyomsifia mwanzo, Mr. Ben, Mr. Clean, sasa akaanza kumkosoa.
Wakati huo Ulimwengu alikuwa na cheo fulani Baraza la Michezo la Taifa, BMT, na nyadhifa kadhaa zingine. Alipotangazwa tu siyo raia, vyote vikaporomoka.
Hiyo ilimchanganya sana Jenerali.
Tokea hapo rungu la uraia limetumiwa sana na serikali za ccm kupambana na wanaowakosoa kwa hoja. Siku zote ccm hawajui kujibu hoja. Kama siyo uraia, watatumia Polisi kukutuhumu uchochezi, uhujumu uchumi, utakatishaji fedha, au hata kukupima mkojo, wakubambikizie madawa ya kulevya. Ndio yalitaka kumkuta Tundu Lissu, bahati njema alikataa kutoa mkojo.
Shida ya Lissu ni mtu wa Singida, katikativya nchi. Unambambikizaje kuwa siyo raia?
Kwa hiyo Magufuli naye hakusita kutumia karata hiyo. Na kwakuwa ni mbabe, yeye sasa akaenda mbali hadi kuitumia kwa maaskofu.
Kwa hiyo nikisikia wengine wakimtaja Waziri Mpango, nachekelea tu, ni kejeli kwa ccm na silaha yake feki.
Nashangaa kuna watu wanamtaja Magufuli kama Mwanamajumui (Pan Africanist) eti shujaa wa Afrika . Hiyo si kweli. Mwanamajumui wa kweli anaamini katika Afrika moja, sio mipaka iliyowekwa na wakoloni. Nyerere ndio, huyo ni Mwanamajumui. Kaipigania Afrika . Hakuwahi hata mara moja kutenda dhambivya ubaguzi, kusema fulani siyo raia. Huo ni ujinga.