Zitto Kabwe awa mbogo, awashukia vikali wanaodai Makamu wa Rais, Dkt. Mpango ni Mrundi

Zitto Kabwe awa mbogo, awashukia vikali wanaodai Makamu wa Rais, Dkt. Mpango ni Mrundi

Huyo ni mrundi roho mbaya za wahutu na mzee wa demotion Bashiru mnyarwanda including the late
Ngoja tumsubiri mwenyewe aje aseme , lakini kwanini mnamtuhumu leo na si miaka iliyopita ?
Kwaiyo wewe ccm na mataga mnamtetea Mrundi sio do you forget how people tortured by The late
 
ninachokiona sasa hivi ni cheap politics.....em tuacheni ujinga tuangalie viongozi wetu wapya watafanya nini na tuwaombee wafanye vizuri.....haya mambo ya kuleta habari za unyarwanda na urundi sahizi nafikiri ni kukosa kazi ya kufanya.....afterall kama hamna cheti chake cha uraia wa burundi basi hamuwezi kudai cheti cha kuzaliwa cha tanzania..
 
Kwani ni nani anayemtuhumu? kuna jibu moja Nyerere aliwahi kulitoa pale Hoteli ya Kilimanjaro baada ya mwandishi mmoja kuda "amesikia"... Wanaodai siyo raia ndio wanajukumu la kutoa uthibitisho wao. Wao watuambie kwanini wanasema siyo rais; kucheza ngoma haiwezekani kuwa ni ushahidi au uthibitisho...
Zitto Kabwe amejitokeza hadharani kutetea uraia wa Dr Mpango , Ameokota wapi hizo shutuma hadi azitetee hadharani ?
 
Ili kumridhisha nani???
I suppose wote tuki-traceback our ancestor's originality tunakua sio wakazi halali wa nchi hii.
Nisawa useme Red indians ndio wanatakiwa kushika uongozi wa US since they're native american.

Naelewa aina tatu za uraia kama anazo moja ya sifa hizo na anakidhi vigezo vya kuongoza basi There ain't any problem with that✌️
Lakini je toka anashika uongozi miaka yote hiyo hadi anakua waziri wa Fedha mbona hamku-Pull up his browsing history...?🙄
 
Huyu si Mwanasiasa wa kwanza kutuhumiwa kwamba si raia wa Tanzania , wako wengine kadhaa walishatuhumiwa akiwemo aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Generali Ulimwengu , wamo akina Eyakuze wa Twaweza pamoja na Maaskofu kadhaa wa Makanisa .

Walichokifanya ni kutoa nyaraka zao kuthibitisha uraia wao , wako ambao pia walithibitisha hata uraia wa babu zao baada ya kutakiwa kufanya hivyo , kwahiyo tuhuma za uraia wala si jambo geni , Nyalandu alidaiwa kuwa na uraia wa nchi mbili mbona hatukusikia akitetewa ?

Makamu wa Rais kama walivyo Watanzania wengine hana kinga dhidi ya shutuma zozote juu yake , anatakiwa ajitokeze hadharani kukanusha tuhuma hizo na kuthibitisha uraia wake , huo ndio Uzalendo , Kabudi na Mwandosya wamewahi kushutumiwa kuhusu vyeti feki lakini walijitokeza hadharani na kutoa ufafanuzi na wazushi wakashindwa , hiki ndicho anachopaswa kukifanya Dr Mpango ili kuweka mambo sawa kabla wadau hawajazusha mengine .

Hakuna haja ya wanasiasa kujivika utetezi wakati Mpango mwenyewe yupo , ajitokeze tu .
Ukishazoea kula nyama ya binadamu huwezi acha
Mlikua mnamnanga Magufuli sio Raia sasa mmekuja kwa Mpango
Yaaani mtu akishatoboa tu kimaisha wanafiki mpo nyuma yake
 
Huyu si Mwanasiasa wa kwanza kutuhumiwa kwamba si raia wa Tanzania , wako wengine kadhaa walishatuhumiwa akiwemo aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Generali Ulimwengu , wamo akina Eyakuze wa Twaweza pamoja na Maaskofu kadhaa wa Makanisa .

Walichokifanya ni kutoa nyaraka zao kuthibitisha uraia wao , wako ambao pia walithibitisha hata uraia wa babu zao baada ya kutakiwa kufanya hivyo , kwahiyo tuhuma za uraia wala si jambo geni , Nyalandu alidaiwa kuwa na uraia wa nchi mbili mbona hatukusikia akitetewa ?

Makamu wa Rais kama walivyo Watanzania wengine hana kinga dhidi ya shutuma zozote juu yake , anatakiwa ajitokeze hadharani kukanusha tuhuma hizo na kuthibitisha uraia wake , huo ndio Uzalendo , Kabudi na Mwandosya wamewahi kushutumiwa kuhusu vyeti feki lakini walijitokeza hadharani na kutoa ufafanuzi na wazushi wakashindwa , hiki ndicho anachopaswa kukifanya Dr Mpango ili kuweka mambo sawa kabla wadau hawajazusha mengine .

Hakuna haja ya wanasiasa kujivika utetezi wakati Mpango mwenyewe yupo , ajitokeze tu .
Nani kalalamika
 
Philip Isdor Zabayanga Mpango
Kumekucha Sasa Hivi
Vyeo Vina Mambo Yaani Hata Mate Hajameza Kwenye Kiti Chake Tayari!!!😣😏😣😏😏

Waha
 
Ili kumridhisha nani???
I suppose wote tuki-traceback our ancestor's originality tunakua sio wakazi halali wa nchi hii.
Nisawa useme Red indians ndio wanatakiwa kushika uongozi wa US since they're native american.

Naelewa aina tatu za uraia kama anazo moja ya sifa hizo na anakidhi vigezo vya kuongoza basi There ain't any problem with that✌️
Lakini je toka anashika uongozi miaka yote hiyo hadi anakua waziri wa Fedha mbona hamku-Pull up his browsing history...?🙄
Wala hatutofautiani na wewe , tuko pamoja kwenye hili
 
Kwani ni nani anayemtuhumu? kuna jibu moja Nyerere aliwahi kulitoa pale Hoteli ya Kilimanjaro baada ya mwandishi mmoja kuda "amesikia"... Wanaodai siyo raia ndio wanajukumu la kutoa uthibitisho wao. Wao watuambie kwanini wanasema siyo rais; kucheza ngoma haiwezekani kuwa ni ushahidi au uthibitisho...
Uthibitisho wa wanaomtuhumu ni video clip moja yenye mashairi ya KIHA ambapo Dr. Mpango ameonekana akishiriki kucheza. Seems ilikuwa ni wakati wa campaign za Ubunge. Nothing more. Kama Waha ni Warundi basi Dr. Mpango ni Mrundi.

Hoja nyepesi...just!
 
Kigogo angekuwa known ingependeza zaidi ili awe liable anapothibitika kumchafua mtu, lakini kujificha kwa fake ID halafu unaropoka ropoka sio fair, Dr. Mpango himself alishasema yeye ni Muha, Kigogo kwa kujaribu ku prove wrong kaweka video Dr. Mpango akicheza ngoma ya "kirundi" na anaowaita ni "warundi", hili peke yake kwangu halitoshi kuthibitisha bila shaka kwamba Dr. Mpango ni Mrundi, kwani kwa kawaida maeneo ya mipakani mara nyingi tamaduni zao hufanana kati ya nchi moja na nyingine, mbaya zaidi Kigogo nae anatumia taarifa za mtu mwingine kutoa hizo shutuma ambapo mtu huyo nae anatumia fake ID.
Yaan watu huwa wanakosa vya kuzungumza,,makabila ya mipakani yanaingiliana sana kitamaduni na yaweza kuwa kabila ni moja hilohilo, waha na warundi wanaingiliana sana, Sawa na wajaluo au wamasai kwa Tz na kenya.

Kwa mtu wa Buhigwe pale mnanila unamtofautishaje na mtu wa pale Mabamba Burundi? Siku za masoko watu wanaenda fuata ndizi na kuku au maharage Burundi na jioni wanarudi Tz, Kiha na kirundi wao ndio wanaweza kujuana lakini mtu mwingine huwezi jua, ni Sawa na Wasukuma, Nyantuzu na Wanyamwezi,, Wahaya na watusi wa Rwanda na Uganda...Rwekaza ni jina liko pande zote watusi na Wahaya...Chuki hizi hazitusaidii kama jamii ya watanzania!
 
Back
Top Bottom