Zitto Kabwe: Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa ambayo hamjawahi kuyaona, tusipoteze hii fursa jamani

Nadhani wewe ndio unachanganya mambo hapa, mimi naelewa vizuri. Hawa waliingia katika matatizo kwa ajili ya kukopa pesa nyingi China haikuwa uwekezaji wa kibiashara. Sisi issue ya Port ni uwekezaji wa makubaliano ya kibiashara. nikupe mfano miwili sisi na hao Srilanka. chukuwa wewe una kiwanja Kariakoo anakuja mfanya biashara anakwambia nipe kiwanja nijenge gorofa ikiisha nakupa maduka 4 mimi nachukuwa 10 baada ya miaka 20 nikiwa nimerudisha pesa zangu nitakupa wewe 10 na mimi 4 baadaya muda nyumba yote yako, huu uwekezaji wa kibishara na makubaliano ndio yetu Bagamoyo. Hao wengine ni kuwa walikuwa na kiwanja wakaenda Bank kukopa pesa nyingi biashara imekataa kurudisha hawawezi Bank inachukuwa nyumba. msichange mikopo na investment kama kukopa tumekopa kipande cha mwisho cha SGR toka Mwanza huo ni mkopo na lazima urudishwe, tulikopa Gas line toka Mtwara ndio mikopo. Ukisoma zote ulizonitumia ni kuwa walichukuwa mikopo
 
🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾 Ahsante sana hawa wahuni nchi imewashinda na wanajua hivyo sasa wamebaki kulazimisha kung’ang’ania madarakani kwa kutumia njia haramu. Zitto ni mnafiki na mroho wa madaraka watu wenye tabia hizi ni watu hatari sana kwa mustakabali wa Taifa. Sasa kaamua kujiegemeza kwa Mama akitegemea kupata ulaji.
 

Hayo maelezo yako umeyatoa wapi? Mbona ni tofauti na Hayati, Pia aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa TPA Kakoko.
 
Tatizo bandari mnayotaka kuijenga haipo Chatial... hapa ndipo tatizo lilipo msitafute mchawi.
 
Eti mameli makubwa ndiyo fahari yake kuona mameli makubwa bila faida yoyote
 
Nadhani kila mradi unatakiwa uwe kwenye mpango wa Maendeleo.Hatuwezi kuwa tunafuta miradi bila kufuata utaratibu wala kuirudisha miradi kwenye mpango kwa kutumia njia za Mkato.
 
ni kweli tatizo watatuendesha wao kwa mashati yao ukoloni mambo leo. bora tutafute vyakwetu tu tuwe huru.
 
Sasa hapo hapo kwenye mfano wako nani ana control cost za investment , pili nani ana control rent, na kwa ujumla revenue wakati wewe huhusishwi ktk hiyo biashara, halafu risk nyingine ikiwa biashara isiende vizuri hivyo wasirudishe hela yao ktk kipindi walicho sema inakuwaje.
Mwisho kuna kitu kinaitwa substance over form.
Kimsingi mtu anapoweka sharti la kurudisha pesa yake na faida ni mkopo. Usidanganyike na haya maneno mengine ya uwekezaji wa kibiashara.

Another example is the situation where a company short of cash sells its machinery to the bank and then leases the same property from the bank. ... Under the substance-over-form principle, the sale and subsequent leaseback are considered one transaction.
Hapa zimechukuliwa kwamba umekopa na sio umeuza hiyo machinery , na hela ya ku lease zimechukuliwa kama ni ya kulipa mkopo interest na principal

Ndio maana kwenye mambo kama haya tunatakiwa kuwatumia wataalamu na sio wanasiasa,
Hapa mwana siasa atakwambia huyu anatujengea sio anatukopesha na masharti yake ni nafuu kulinganisha na nini hakwambi,
Ndio tukaishia kujenga jengo la umoja wa vijana, uwt n.k n.k
 
KC wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema kitu ambacho wabunge wengi hawakijui ni kwamba Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa makubwa kutoka huko duniani ambazo hatujawahi kuziona hapa Tanzania
Halafu tuwape kwa miaka 99 sio ?

Ushenzi na umangimeza uliokubuhu. Kwa hili Zitto nakukatalia kwa herufi kubwa HAPANA
 
Halafu tuwape kwa miaka 99 sio ?

Uhsenzi na umangimeza uliokubuhu. Kwa hili Zitto nakukatalia kwa herufi kubwa HAPANA
Sasa wanjanja watu kuwekea miaka 33 wakati kuna kifungu kingine wanaficha kwamba mkataba utaendelea ikiwa hawajarudisha fedha zao huku fedha zingine wanachukua kwa ununuzi vipuri na mngt fees
 
Ngoja tukashangae mameli Bagamoyo.
Bwana eh tuandae makameraaa makubwa kabisa
Ila ipo siku watamkumbuka jpm kwenye hili
Maana naona nguvu kubwa ya kutuaminisha inatumika ili wafanikishe azma yao

Ova
 
Hatautatki hayo mameli yasiyo faida na wananmchi. Waambie wachina waende Kenya hatutaki Bandari Bagamoyo na mlogwe muipitishe patachimbika!
 
Sasa wanjanja watu kuwekea miaka 33 wakati kuna kifungu kingine wanaficha kwamba mkataba utaendelea ikiwa hawajarudisha fedha zao huku fedha zingine wanachukua kwa ununuzi vipuri na mngt fees
Khaa . . management fees ? Pumbavu kabisa
 
Bwana eh tuandae makameraaa makubwa kabisa
Ila ipo siku watamkumbuka jpm kwenye hili
Maana naona nguvu kubwa ya kutuaminisha inatumika ili wafanikishe azma yao

Ova
Hahahaaaa...... !

Mchina akitimba Bagamoyo wazaramo wote watasukumiziwa Msata na Pangani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…