Zitto Kabwe: Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa ambayo hamjawahi kuyaona, tusipoteze hii fursa jamani

Wekeni hadharani vipegele vya mkataba. Hatubishanii umuhimu wa bandari. Mkataba. Mwendake alituambia mkataba ule ni mbovu. Uleteni bungeni, wabunge wauone na waujadili. Hatutaki kina Chifu Mangungo wafufuke! Karl Peters wa leo (Wachina) ni wajanja mno.
 
Kwa nini iwe Bagamoyo na isiwe Kilwa au Mafia? Tuache uzuzu hii ni project ya JK ila anatumia wapambe wake na mmojawapo ni Zitto. Huyu ni suhuba wa JK mkubwa sana.
 
Sasa mimi nitautoa wapi huo mkataba? hiyo ni kazi ya bunge. sidhani kama kuna mkataba labda majadiliano maana mkataba unakuwa umeshawa kuwa sign na unakuwa kisheria mimi sijui kama kuna mkataba wa lisign. Ni kazi ya watunga sheria kutaka kuona hayo majadiliano na kuweka wazi kwa wananchi wote. mashaka yangu tu aina ya wabunge waliopo wana upeo wa kujadilia mambo labda wachache. lazima zipimwe hasara na faida zake mwisho wa siku uzito una beba maamuzi. Mimi sina mkataba na wala sijui kilichopo hata aliyeongea hakuweka ushahidi kama karatasi wenye masharti hayo yalikuwa maneno tu kama sisi hapa tunavyoongea.
 
Nimekupata. Tunajadili kwa muktadha wa Muheshimiwa sana Ndugai anayetetea sana kila anachosema mwendazake alishauriwa vibaya. Alete proof hiyo bungeni wabunge waone nani kamdanganya nani.
 
kwanini wasitoe mkataba tukauona? wanabaki tu tujenge wengine wanasema tusijenge. bora hoja za JPM zilijikita kwenye mkataba
 
Nimekupata. Tunajadili kwa muktadha wa Muheshimiwa sana Ndugai anayetetea sana kila anachosema mwendazake alishauriwa vibaya. Alete proof hiyo bungeni wabunge waone nani kamdanganya nani.
Mimi nilichosikia kwa Ndungai ni kuwa port Bagamoyo inahitajika sasa kama wa China hamuwezi kuafikiana nao tafuteni wawekezaji wengine yoyote aje ajenge yeye kasema mradi unahitajika. Hayati yeye kasema wanataka kutuibia basi yakaishia hapohapo, ndio maana yanaitwa majadiliano na PSA inataka watu wenye kujuwa kujadiliana wale ni wafanya biashara hawaji kutoa misaada lazima watuvuta upande wao. Mimi na uhakika port itajengwa sasa itajengwa na nani hilo sijui. Bunge wako busy kujadili Legacy ya marehemu badala ya maendeleo.
 
Kwa asimia ngapi Bandari zetu za Tanga na Mtwara zinatumika? Kuna tofauti gani za gharama kati ya kuzipanua na kuziimarisha Bandari za Tanga na Mtwara na ujenzi wa Bandari mpya ya Bagamoyo. Ni faida zipi zitakazoletwa na Bandari ya Bagamoyo ambazo hatuzipati katika Bandari za Tanga na Mtwara? Majibu ya Maswali haya ndio yatakayo halalisha au kutohalalisha ujenzi wa Bandari Mpya ya Bagamoyo. Lakini pia uwezekano wa upanuzi wa Bandari ya Dar Es Salaam.
 
Alafu muda wao ukiisha wanakuachia magofu na ardhi yako isiyo na faida tena maana imekua turned into desert
 

kwenye hili nafikiri mchina anataka njia ya uhakika ya kuchukua malighafi kutoka DRC , Zambia na hata Tanzania. Kufanikisha hili wanataka bandari watakayo iendesha wao na reli. Bandari ndio hiyo ya Bwagamoyo na reli wanaitaka TAZARA. Nafikiria pia wanataka njia hiyohiyo itumike kuleta bidhaa kutoka kwao kwa mauzo huku wanakokuita bara jeusi.
 
Sawa mameli makubwa makubwa tunayataka lakini kwanini hawataki TRA yetu ikusanye kodi kwa miaka zaidi ya 30? Tupe sababu
 
Reactions: Ame
Alafu muda wao ukiisha wanakuachia magofu na ardhi yako isiyo na faida tena maana imekua turned into desert
Udsm wataachiwa magofu pale mlimani city km sio majengo yaliyopoteza mvuto baada ya hio miaka 50...wasomi ila hamna kitu, watu wanaingia mikataba kwa maslai binafsi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…