Zitto Kabwe: Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa ambayo hamjawahi kuyaona, tusipoteze hii fursa jamani

Zitto Kabwe: Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa ambayo hamjawahi kuyaona, tusipoteze hii fursa jamani

Kwa gharama ipi , ya kuuza hiyo Bandari kwa wawekezaji.
Tatizo lenu hamtaki kusikiliza!

Mngekuwa mnasikiliza hoja na kizipima badala ya kupinga tu kwa kuwa mtoa hoja humpendi.

Mradi wa Bandari ya Bagamoyo,ulikuwa ujengwe kwa makubaliano ya uwekezaji wa pande tatu,Tanzania,Oman na China. Wawekezaji wangejenga miundo mbinu ya bandari na industrial parks kwa ajili ya viwanda zaidi ya 800 na kuchukua port charges kwa kipindi cha miaka 50. Serikali haikuyakiwa kutoa hata sumuni! Katika kipindi hicho serikali itachukua kodi zingine mbalimbali kama ushauri wa forodha kama kawaida. Baada ya miaka hiyo, bandari inakuwa mali ya serikali 100%

Utaratibu huu ndio unaotumika hata sasa kwenye bandari ya Dar. Wapo TICTS wanaendesha bandari hiyo.

Mradi wa Bandari ya Bagamoyo unamanufaa makubwa katika uchumi wa Tanzania. Pamoja na kuifanya Tanzania kuwa lango juu la bidhaa kwa zaidi ya nchi 8 za Afrika,unaifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda vya kisasa ambavyo vitahudumia soko la ndani na nchi nyingine za Afrika.

Mradi huu utazalisha ajira nyingi mno katika sekta mbalimbali kama mahoteli, usafirishaji nk.
 
Watu washakula hela, propaganda zinaendelea.
 
Lobbyist Kazini......kashachukua chake mapema. Ndungai na Kamati yake nao wakapiga chapuo.
Hii kitu ina madhara kwa nchi zetu maana Wachina siyo jukumu lao kutufundisha namna ya kuingia mikataba, ukiingia kichwa kichwa umepigwa na kinachofuata utulie dawa ikuingie hadi mkataba itakapoisha....mfano mibaya ya mikataba ya China ktk nchi za Africa ni Djibouti, Angola, DRC na Zambia na zinginezo. hii inaitwa Belt and Road Initiative ya China ...

The Belt and Road Initiative, known in Chinese and formerly in English as One Belt One Road or OBOR for short, is a global infrastructure development strategy adopted by the Chinese government in 2013 to invest in nearly 70 countries and international organizations.
 
Hii habari imekaa design kama gazeti la udaku. Tupatie habari kwa ukamili sio kuibia na kutoa mambo out of context.
 
Mkuu achana na Zitto kwa mda.

Trend yake ya Sasa amejigeuza zwazwa.

Mwache kwanza hadi kichwa kikitulia Ndio uanze kumpost. Hasa akiendelea kukosa teuzi maana hapo alipo anatakani ateuliwe.
Anaenda kugombea ubunge kule kwa Dr Mpango!
 
China sio mwekezaji tu ni mnyonyaji kama wanyonyaji rasilimali wengine.
Mwekezaji gani hajengi viwanda badala yake anachukua tu tenda za kujenga kila kitu hapa barani Africa na kuchota rasilimali zetu??
Huna taarifa za kutosha kuhusu wachina.

China ndio wawekezaji wakubwa sasa hivi duniani kwa sababu ya ukwasi wao. China wana mapesa mengi mno ya kuwekeza!

Hata mradi wa bomba uliosainiwa juzi kule Uganda,wachina wanamiliki hisa nyingi tu kukaribia zile za wafaransa.
 
Tatizo lenu hamtaki kusikiliza!

Mngekuwa mnasikiliza hoja na kizipima badala ya kupinga tu kwa kuwa mtoa hoja humpendi...
Unaelewa mtu akikuuliza maana ya kwa gharama ipi?

Mfano wewe ukitaka kujenga nyumba mfano ya 80m na kulipa na riba ikafika 40m jumla 120m.

Na mwingine aje akwambie nitakujengea nyumba lakini nitaka nayo hadi nipate 200m.

Utachukua uamuzi upi
 
Mkuu jamaa ni mnafiki na mchumia tumbo mkubwa. Details za mkataba huo na Wachina zikiwekwa hadharani Watanzania tutaukataa.

Ngoja wauweke tuone kama ni mzuri au mbaya kama ni mbaya kwa vipengele vinaweza kujadiliwa ili win win situation ipatikane ,miradi kama ile ndio inakuza uchumi.
 
Naunga mkono hoja na ifunguliwe tu bagamoyo ku shine kama chuttle....
 
Back
Top Bottom