Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani Unaamini unapoambiwa Ukifa unaenda kwa Mungu?Sijui kwa nini tu huyu jamaa huwa siamini ayasemayo....
Kwani Unaamini unapoambiwa Ukifa unaenda kwa Mungu?Sijui kwa nini tu huyu jamaa huwa siamini ayasemayo....
Siamini.Kwani Unaamini unapoambiwa Ukifa unaenda kwa Mungu?
Mbona kwenye ujenzi wa Chuo cha siasa cha CCM na vyama vya ukombozi hatukusikia hizi figisu. Tulichodikia ni kwamba Wachina na marafiki zetu.China sio mwekezaji tu ni mnyonyaji kama wanyonyaji rasilimali wengine.
Mwekezaji gani hajengi viwanda badala yake anachukua tu tenda za kujenga kila kitu hapa barani Africa na kuchota rasilimali zetu??
Gharama ni dola bil 10,ambazo wao wanatakiwa wazipate pamoja na faida katika hicho kipindi cha muda wa concession ambayo ni miaka 50 au chini ya hiyo kulingana na umahiri wetu kwenye negotiation.Unaelewa mtu akikuuliza maana ya kwa gharama ipi?
Mfano wewe ukitaka kujenga nyumba mfano ya 80m na kulipa na riba ikafika 40m jumla 120m
Na mwingine aje akwambie nitakujengea nyumba lakini nitaka nayo hadi nipate 200m.
Utachukua uamuzi upi
Ngoja wauweke tuone kama ni mzuri au mbaya kama ni mbaya kwa vipengele vinaweza kujadiliwa ili win win situation ipatikane ,miradi kama ile ndio inakuza uchumi.
Details zinadai kwamba Wachina wangeleta management team yote kwa miaka 100 ijayo na pia mapato yote ya hiyo bandari kwa miaka 100 ni yao ili kurudisha mkopo wao, Tanzania haipati hata senti.
Ni mambo ya kushangaza kabisa!Mbona kwenye ujenzi wa Chuo cha siasa cha CCM na vyama vya ukombozi hatukusikia hizi figisu. Tulichodikia ni kwamba Wachina na marafiki zetu.
Kitu ambacho sielewi ni wapi Mchina anakuwa rafiki na ni wapi ambapo anakuwa siyo rafiki.... In short. Je China ni rafiki au siyo rafiki!!?
Usichanganye mada hapa, Magufuli alijichafua mwenyewe. Alikuwa na nafasi ya kuwa Rais bora kabisa lakini akachagua kuwa Dikteta. Mimi simkubali na sitamkubali kwa namna yake ya kuendesha nchi kama familia yake, lakini bado sikubaliani na mradi wowote ulioasisiwa na Kikwete baada ya Ridhiwan kukamatwa China.Hawa wametumwa! Hii campaign itakuwa chini ya uratibu wa timu ile ile inayomchafua JPM.
Bandari ya Bagamoyo itajengwa stay tuned! Hivi daraja la wakwe pale Busisi na Bandari ya Bagamoyo kipi cha muhimu. Wasukuma mjiandae kisaikolojia!So...?
Stupid statement! Hayo mameli makubwa yataleta nini? Ni statement inayostahili kutolewa na vijana wa kivukoni wakisubili kuzamia meli. Yaani meli kubwa zinaweza kuja bila sababu.KC wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema kitu ambacho wabunge wengi hawakijui ni kwamba Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa makubwa kutoka huko duniani ambazo hatujawahi kuziona hapa Tanzania..
Shida mnaochangia hamkumsikiliza. Kasema waliona plan ya huo mradi lakini mkataba haukueahi kupelekwa bungeni wala hawakuwahi uona uko ikulu tu, kaomba badala yake uwekwe wazi watu wajue kilichokuwemo kuliko tu mtu kusema tu kwanini usiwekwe wazi.Kwa gharama ipi , ya kuuza hiyo Bandari kwa wawekezaji.