Tatizo lenu hamtaki kusikiliza!
Mngekuwa mnasikiliza hoja na kizipima badala ya kupinga tu kwa kuwa mtoa hoja humpendi.
Mradi wa Bandari ya Bagamoyo,ulikuwa ujengwe kwa makubaliano ya uwekezaji wa pande tatu,Tanzania,Oman na China. Wawekezaji wangejenga miundo mbinu ya bandari na industrial parks kwa ajili ya viwanda zaidi ya 800 na kuchukua port charges kwa kipindi cha miaka 50. Serikali haikuyakiwa kutoa hata sumuni! Katika kipindi hicho serikali itachukua kodi zingine mbalimbali kama ushauri wa forodha kama kawaida. Baada ya miaka hiyo, bandari inakuwa mali ya serikali 100%
Utaratibu huu ndio unaotumika hata sasa kwenye bandari ya Dar. Wapo TICTS wanaendesha bandari hiyo.
Mradi wa Bandari ya Bagamoyo unamanufaa makubwa katika uchumi wa Tanzania. Pamoja na kuifanya Tanzania kuwa lango juu la bidhaa kwa zaidi ya nchi 8 za Afrika,unaifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda vya kisasa ambavyo vitahudumia soko la ndani na nchi nyingine za Afrika.
Mradi huu utazalisha ajira nyingi mno katika sekta mbalimbali kama mahoteli, usafirishaji nk.