Zitto Kabwe: Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa ambayo hamjawahi kuyaona, tusipoteze hii fursa jamani

Zitto Kabwe: Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa ambayo hamjawahi kuyaona, tusipoteze hii fursa jamani

Kwani waliutekeleza? Kama hawakuutekeleza na siyo rafiki kwanini usiwekwe wazi? Maana siyo mkataba wamambo jeshi waweke wazi tuone kaa kweli nchi ilitaka kuuzwa maana aliyeuoana akatwambia ndiyr pia alitwambia ATCL inatengeneza faida na gawio likaletwa, ni afadhali uwekwe wazi tuache kusikia sikia tu tuwe na hakika na yaliyomo.
Yeye Zitto kasema kwakuwa hajui yaliyomo yeye aliona tu presentation, kama wale walikuwa na terms mbaya tunaweza tafuta washirika wengine au serikali ikajenga yenyewe ila anachelea kwa ukubwa wa bandari ile serikali haiwezi kuijenga bila usadizi.
Mimi ningependa wasifanye move bila kuweka mkataba wazi kama alivyosema zitto.
Umewaza na kunena vyema!
 
KC wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema kitu ambacho wabunge wengi hawakijui ni kwamba Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa makubwa kutoka huko duniani ambazo hatujawahi kuziona hapa Tanzania

Kisha hizi meli tunazoziona zikileta mizigo Dar port ndio zitakuwa zinabeba miizigo kutoka Bagamoyo na kusambaza sehemu mbalimbali duniani amesisitiza Zitto

Tusiiache fursa hii jamani na siyo kweli kwamba kila mradi ulioanzishwa awamu ya Kikwete ulikuwa mbaya kwani hata reli ya SGR mradi uliasisiwa vizuri na serikali ya JK lakini serikali ya awamu ya tano imekuja kuutekeleza kwa namna tofauti, amemalizia Zitto.

Chanzo: Clouds 360
Nisizungumze Sana,maana wenda Kuna watu wanajua na wanaupeo mkubwa kuhusu bandali hii,lakini wenda wengine atuhujui vizuri ila tumebatika kua na karama ya fikra,
Mfano hivi tukiamua kwamba mradi huo na pesa yake kuongezwa kwenye bandari ya Dar ikapanuka zaidi mameli makubwa na makubwa hayawezi fika ,au vipi mladi huo ukipelekwa kwenye majiji makubwa ya mwambao nje ya dar ikiwemo TANGA n.k lazima tuwekeze kitu kikubwa sehem moja,alihali bado ukanda huo una badandari nzuri japo wenda haiwezi fikia michoro mipya ya bandari bandari ya Bagamoyo,
Taifa ili kwenda kasi lazima kupanua wigo why Kama vipi isipelekwe MTWARA, kunanani Bagamoyo ????
Wakuu sipingi kujengwa bandari ya Bagamoyo but lazima kuwa na fikra pana katika kuitanua tz ,Tz ni kubwa Sana na kila mwananchi anaitaji tulsa sawa bila kujali yuko wapi,chamsingi kodi kuingia ,
MWISHO
HILI SWALA WASAIDIZI WA MH RAIS MAMA SSH, MSIMUINGIZE CHAKA KWA MASLAHI BINAFSI MPENI MDA ,ATAFAKARI,
 
KC wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema kitu ambacho wabunge wengi hawakijui ni kwamba Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa makubwa kutoka huko duniani ambazo hatujawahi kuziona hapa Tanzania

Kisha hizi meli tunazoziona zikileta mizigo Dar port ndio zitakuwa zinabeba miizigo kutoka Bagamoyo na kusambaza sehemu mbalimbali duniani amesisitiza Zitto

Tusiiache fursa hii jamani na siyo kweli kwamba kila mradi ulioanzishwa awamu ya Kikwete ulikuwa mbaya kwani hata reli ya SGR mradi uliasisiwa vizuri na serikali ya JK lakini serikali ya awamu ya tano imekuja kuutekeleza kwa namna tofauti, amemalizia Zitto.

Chanzo: Clouds 360

Huyu ni wale ambao Mwalimu alisema wanatabia ya kimalaya malaya; ananunulika, kwa bei fulani!

Hakuna mtu aliyepinga bandari kama bandari. Kilichopingwa ni terms and conditions za ujenzi wa hiyo bandari. Maelezo aliyoyatoa yeye ni useless katika debate ya utekelezaji wa huo mradi.
 
Issue ya Bagamoyo Port imekua kama hadithi ya kuku na yai kipi kilianza.

jambo ninalojiuliza, kama hawa wawekezaji wenye wanatoa hela zao 100% kufinance mradi, huku host country anatoa ardhi tu bila senti moja, iweje Rais akatae? Napata shida sana kuelewa hili jambo!
 
We ndiyo wawaza hivyo lakini kumbua China ndiye exporter mkubwa duniani nani kwanini meli iende mpaka China kama inaweza chukua mzigo huo huo bagamoyo ikarudi ilipotoka.
Tatizo la watanzania wanajifanya wajuaji wa kila kitu!

Malayman tu wanajadili mambo ambayo hawana hata basic knowledge! Nonsense kabisa.

Umejaribu kuwaelewesha kwa kina kuhusu mradi huu na maelezo ya Zito lakini watu wanapinga tu kwa kuwa wameamua hivyo! Hawataki kusikiliza hoja!
 
Zitto huwaga mpiga debe wa mabeberu tu hata sinshangai, hii meli kubwa kiasi gani istue dar? Muongo sana huyo. Na yeye kaiona wapi?
Mabeberu nawapenda sana.
 
Tatizo la watanzania wanajifanya wajuaji wa kila kitu!

Malayman tu wanajadili mambo ambayo hawana hata basic knowledge! Nonsense kabisa.

Umejaribu kuwaelewesha kwa kina kuhusu mradi huu na maelezo ya Zito lakini watu wanapinga tu kwa kuwa wameamua hivyo! Hawataki kusikiliza hoja!
Wachangiaji wengi hawajamsikiliza. Wanamshambulia tu na hii ni hulka ya wengi. Kuna muda uwa nakwepa kuchangia baadhi ya threads kwakuwa mtu anaweza bisha jambo ambalo hata hakulifuatilia kabisa.
 
Kwa huu ukanda wety, hatuna mizigo ya kuleta mameli makubwa...

Ni sawasawa unapeleka Yu tong kijijini huko ukapaye abiria wkt ukijua hakuna abiria wa kujaza hilo gari....

Ukanda umekaa kushoto, hata nchi zilizotuzunguka hazina mahitaji ya mameli makubwa....

Zitto ana % zake kwenye hili
 
Huyu ni wale ambao Mwalimu alisema wanatabia ya kimalaya malaya; ananunulika, kwa bei fulani!

Hakuna mtu aliyepinga bandari kama bandari. Kilichopingwa ni terms and conditions za ujenzi wa hiyo bandari. Maelezo aliyoyatoa yeye ni useless katika debate ya utekelezaji wa huo mradi.
Hizo terms ziko wapi na je, kama zipo kwano majadiliano yamefika mwisho ???

Tatizo la hiki kizazi, majadiliano yanaongozwa na CHUKI, UMSUKULE, UNYUMBU na UPUMBAVU.

Hakuna nchi makini duniani inaweza kukataa FDI.

Mambo ya mikataba ni majadiliano na makubaliano.
 
Huyu ni wale ambao Mwalimu alisema wanatabia ya kimalaya malaya; ananunulika, kwa bei fulani!

Hakuna mtu aliyepinga bandari kama bandari. Kilichopingwa ni terms and conditions za ujenzi wa hiyo bandari. Maelezo aliyoyatoa yeye ni useless katika debate ya utekelezaji wa huo mradi.
Hivi mkuu umesikiliza interview yake kweli? Hata yeye anataka kujua terms and condition anataka mkataba huo uwekwe wazi kwa umma maana zaidi ya kuwa ikulu hata wabunge hawajawahi uona hizo terms mlimegewa na jpm ambaye ndiye pia aliwamegea kuwa ATCL inapata faida na gawio akapokea.
Kukata mzizi wa fitina mkataba uwekwe wazi.
Zitto yeye alichoona ni presentation ya mradi mkataba naye anatamani uona ajue nini kilichomo kitu ambacho serikali haijawah fanya
 
Kwa huu ukanda wety, hatuna mizigo ya kuleta mameli makubwa...

Ni sawasawa unapeleka Yu tong kijijini huko ukapaye abiria wkt ukijua hakuna abiria wa kujaza hilo gari....

Ukanda umekaa kushoto, hata nchi zilizotuzunguka hazina mahitaji ya mameli makubwa....

Zitto ana % zake kwenye hili
Mameli makubwa huwa yanabeba nn ambavyo ukanda huu hauhitaji? Mkataba uwekwe wazi tuone hayo masharti kama ni ya kipuuzi tuachane kinyume na hapo ni nafasi nzuri kwa nchi kuwa na bandari ya kiwango kikubwa.
 
Africa is always the victim, nothing is ever our fault. Yaani kila muwekezaji ni mbaya na anataka kutuibia.
Alafu yaambie yawekeze yenyewe hayawekezi.Alafu yanaiba yanapeleka huko huko kwa wazungu.ndiyo maana yanapowaita wazungu mabeberu nayaona ni mambuzi jike tu ambayo ni mapumbavu fulani hivi
 
Gharama ni dola bil 10,ambazo wao wanatakiwa wazipate pamoja na faida katika hicho kipindi cha muda wa concession ambayo ni miaka 50 au chini ya hiyo kulingana na umahiri wetu kwenye negotiation.

Ni kama wawekezaji kwenye mradi wa Mlimani City wanavyofanya. Baada ya muda wa mkataba,majengo yote ya Mlimani City yatakuwa mali ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
ulishasoma ripoti ya CAG juu ya uwekezaji wa Mlimani city kwa chuo kikuu kama bado kaitafute halafu uone hata wanajiita wasomi wanavyoingia mikataba ya hovyo
 
Watalaam wanasema bandari ya dsm inaweza kupokea meli kubwa (21 century vessels) kwa sababu kina kime ongezwa kutoka mita 9 mpaka 16

Bw.Julius Nghula anasema mahitaji yetu ndio yataleta izo meli kubwa. (Dwmand and supply concept hapa naona inatumika) mtalaam huyu katolea mfano
Bandari ya mtwara ina kina kirefu kuliko lkn meli kubwa za mafuta zinatua dsm kwa sababu mahitaj ya mafuta dsm.ni mengi

Mtalaam huyu anasema ziwepo sababu zingine za ujenzi wa bandari ya bagamoyo lkn sababu isiwe kupwa na kujaa kwa maji wala kina

Huyu mtalaam alikuwa live tbc habari
Patamuuu hapo
 
KC wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema kitu ambacho wabunge wengi hawakijui ni kwamba Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa makubwa kutoka huko duniani ambazo hatujawahi kuziona hapa Tanzania

Kisha hizi meli tunazoziona zikileta mizigo Dar port ndio zitakuwa zinabeba miizigo kutoka Bagamoyo na kusambaza sehemu mbalimbali duniani amesisitiza Zitto

Tusiiache fursa hii jamani na siyo kweli kwamba kila mradi ulioanzishwa awamu ya Kikwete ulikuwa mbaya kwani hata reli ya SGR mradi uliasisiwa vizuri na serikali ya JK lakini serikali ya awamu ya tano imekuja kuutekeleza kwa namna tofauti, amemalizia Zitto.

Chanzo: Clouds 360
Nasema sitaruhusu huyo upuuzi ufanyike nchi,sipo tayari kuweka rehani nchi yangu kwa bepari jinping,srilanka wanalia,Zambia wanalia,Kenya wanalia lkn mimi sipo tayari kulia.
 
Kwakuwa aliyekuwepo hakutaka mawazo tofauti akikusikia kitakachokupata wanakijua kilichowapata. Hivi shida iko wapi kuweka mkataba wazi maana hata yeye hajasema utekelezwe bila huo mkataba kuwekwa wazi.
Ni now kwasababu ndiyi watu wanajisikia huru walau kuzungumza mawazo yao. Mbona wakati wa JK watu walikuwa wanazungumza tu akitaka atayachukua akigoma basi sasa hiyo chance waliikosa sasa wameipata.
Umenena vyema!

Wote tumeshuhudia ukatili na ubabe wa Magufuli. Nani angethubutu kuchallenge uamuzi wake? Nani angethubutu kusema alitudanganya?

Walikuwa sahihi kunyamaza. Kama walivyonyamaza kwenye kila suala alilolitolea maamuzi kama suala la kukataa watoto wa kike wanaopata mimba wasirudi shule kuendelea na masomo!

Kwa kuwa sasa Mungu ameturudishia uhuru wa nchi yetu tena,ni jambo la heri tuwe na mjadala wa wazi kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo kama huu mradi. Tuujue ukweli. Tuliyoambiwa na upande mmoja tu wa Magufuli hatuwezi kuyaamini! Alitudanganya ATCL inapata faida kumbe ni hasara tupu. Alikuwa haiaminiki! Hata kwenye hili,anaweza kuwa alitudanganya kwa sababu ambazo alizijua mwenyewe.
 
Back
Top Bottom