Zitto Kabwe: Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa ambayo hamjawahi kuyaona, tusipoteze hii fursa jamani

Zitto Kabwe: Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa ambayo hamjawahi kuyaona, tusipoteze hii fursa jamani

Hivi mkuu umesikiliza interview yake kweli? Hata yeye anataka kujua terms and condition anataka mkataba huo uwekwe wazi kwa umma maana zaidi ya kuwa ikulu hata wabunge hawajawahi uona hizo terms mlimegewa na jpm ambaye ndiye pia aliwamegea kuwa ATCL inapata faida na gawio akapokea.
Kukata mzizi wa fitina mkataba uwekwe wazi.
Zitto yeye alichoona ni presentation ya mradi mkataba naye anatamani uona ajue nini kilichomo kitu ambacho serikali haijawah fanya

Ukikuta mtu anatetea kitu bila ya kuwa na all relevant information, unamweka kundi gani?
 
We ndiyo wawaza hivyo lakini kumbua China ndiye exporter mkubwa duniani nani kwanini meli iende mpaka China kama inaweza chukua mzigo huo huo bagamoyo ikarudi ilipotoka.
Kaka mizigo unatoka China kuja huku kwetu ni Mitambo,Magari,Steel Product,Nguo,Viatu na madawa. Meli nyingi kutoka China ni General Cargoes.

Mbolea inatoka Morocco,Norway,Russia. Magari yanatoka Ulaya na Japan, material ya Cement yanatoka Ukraine na Uarabuni, Mafuta ya kupikia( Edible oil) Sri lanka na Malyasia na Mafuta ya Petrol/Diesel tunaagiza Uarabuni.Madawa ya binadamu na bidhaa kibao tunatoa Ulaya, Ngano inatoka Canada.

Hilo Suala la meli na Bandari ya Bagamoyo kutegemewa na Afrika haliwezikani sisi tupo upande wa Mashariki tunapambana na Bandari kuanzia Egypt, Djibouti,Somalia,Kenya, Mozambique,South Africa.

Egypt kamwe haiwezi kusubiri mzigo uje Bagamoyo ndio upelekwe kule wakati Wana bandari kubwa na wapo karibu na Dubai ambapo kuna Transhipment. Somalia ni Tia maji wanasubiri bidhaa toka Dubai na Ulaya kwa kiwango Cha kawaida. South Africa hawawezi kuja sababu ya Cost na lazima hiyo meli iende kule sababu kuna mizigo mingi ya ku export ambayo ni mining products na agriculture products.

Sisi itakuwa ni sehemu ambayo meli inashusha mizigo mingi Kisha inaondoka na empty container au tupu kwakuwa hatuna bidhaa nyingi za ku export kadri ya ukubwa wa hizo meli.
 
Hizo terms ziko wapi na je, kama zipo kwano majadiliano yamefika mwisho ???

Tatizo la hiki kizazi, majadiliano yanaongozwa na CHUKI, UMSUKULE, UNYUMBU na UPUMBAVU.

Hakuna nchi makini duniani inaweza kukataa FDI.

Mambo ya mikataba ni majadiliano na makubaliano.

Hiyo dunia unayoisema ni hii hii ambayo sote tunaijua au dunia nyingine? Yaani nchi ikubali predatory and exploitative FDI just because hiyo ni FDI?
 
Foreigner manina kweli wanajua viongozi wetu nani wampe mlungula ili awe mpigadebe wao.
 
Hiyo dunia unayoisema ni hii hii ambayo sote tunaijua au dunia nyingine? Yaani nchi ikubali predatory and exploitative FDI just because hiyo ni FDI?
Hiyo predatory and exploitative FDI iko wapi ??

Na je,makubaliano yalifafikiwa au wahusika hawakutaka makubaliano yoyote ??
 
Kama Zitto Mchumi Mbobezi amesema hivyo mimi ni nani ngumbaru wa MATEJOO nikatae? JIWE alidanganywa.
Zitto amekuwa Mbunge kwa miaka kadhaa, je, amefanikisha japo kuendeleza ufuko wa Ziwa Tanganyika? Ni Zitto huyo huyo aliyedandia zao la korosho wakati la mchikichi jimboni kwake lisiendelezwe.

Bandari ya Kigoma imeboreshwa na usafiri wa Ziwa Tanganyika kuimarishwa. Zao la korosho pia limepata msukumo mpya. Yote hayo yametekelezwa kwa maono, maamuzi magumu na usimamizi imara wa Mwendazake.
 
Tatizo lenu hamtaki kusikiliza!

Mngekuwa mnasikiliza hoja na kizipima badala ya kupinga tu kwa kuwa mtoa hoja humpendi...
Umeuona na kuusoma huo mkataba? Tanga na Mtwara kwenye kina cha asili sio Tanzania ambapo viwanda hivyo vingeweza kujengwa?

Kwamba, yule aliyeusoma, akachukua hatua ya kufanya maridhiano na China, ni punguani?

Wasomi wanazidi kutustaajabisha, mara wasaini mikataba mibovu, mara waibe pesa, mara watengezeane syndicates, mara wauze rasilimali za taifa na kwenda kuficha pesa nje, na sasa tunasikia wanasema Gas fuelled power plant ni nafuu kuliko Hydro.

Sitajutia kutosoma kama usomi utaendelea kupambanuliwa hivi.
 
Ukikuta mtu anatetea kitu bila ya kuwa na all relevant information, unamweka kundi gani?
Presentation yake ilikuwa nzuri sasa anachotaka ni kuona mkataba, hakuna.mahali aliposema bandari ijengwe kwa huo mkataba maana hajauona ndiyo maana anataka uwekwe wazi kila mtu auone kama ni mbaya basi itafutwe plan B ama renegotiation.

Pia kasema Oman imeingia mkataba na zanzibar kujenga bandari hivyo kujenga tena hiyo bandari bagamoyo itakuwa haimake sense unless waje na mpango ya jinsi hizo bandari mbili zinavyoweza kufanya kazi kwa pamoja.
 
Zito naye ni mtu wa madili. Meli kubwa kubwa za nini kama Kodi anakusanya mchina!!!
 
KC wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema kitu ambacho wabunge wengi hawakijui ni kwamba Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa makubwa kutoka huko duniani ambazo hatujawahi kuziona hapa Tanzania...
Hatutaki mameli makubwa tunataka maslahi makubwa kwa nchi hawa makuwadi wa uchumi wanataka kutufikisha pambaya.

Zitto ni ntu wa dili
 
Kama Zitto Mchumi Mbobezi amesema hivyo mimi ni nani ngumbaru wa MATEJOO nikatae? JIWE alidanganywa.
Mchumi ama mchumia tumbo mbobezi , hivi tangu uanze kufuatilia siasa umeshawahi kusikia zitto anampiga mawe J.K?

Hivi unamfahamu mmilili wa ACT?

Kwanini membe aliichagua act na si vyama vyengine?

Siku ukipata majibu utaijua rangi halisi ya zitto
 
Mchumi ama mchumia tumbo mbobezi , hivi uanze kufuatilia siasa umeshawahi kusikia zitto anampiga mawe J.K?
Acha Bla bla kama una ushahidi weka na sio kuokoteza story zenu kwa wanaCUF wa vijiweni na kuleta JF.
 
Back
Top Bottom