We ndiyo wawaza hivyo lakini kumbua China ndiye exporter mkubwa duniani nani kwanini meli iende mpaka China kama inaweza chukua mzigo huo huo bagamoyo ikarudi ilipotoka.
Kaka mizigo unatoka China kuja huku kwetu ni Mitambo,Magari,Steel Product,Nguo,Viatu na madawa. Meli nyingi kutoka China ni General Cargoes.
Mbolea inatoka Morocco,Norway,Russia. Magari yanatoka Ulaya na Japan, material ya Cement yanatoka Ukraine na Uarabuni, Mafuta ya kupikia( Edible oil) Sri lanka na Malyasia na Mafuta ya Petrol/Diesel tunaagiza Uarabuni.Madawa ya binadamu na bidhaa kibao tunatoa Ulaya, Ngano inatoka Canada.
Hilo Suala la meli na Bandari ya Bagamoyo kutegemewa na Afrika haliwezikani sisi tupo upande wa Mashariki tunapambana na Bandari kuanzia Egypt, Djibouti,Somalia,Kenya, Mozambique,South Africa.
Egypt kamwe haiwezi kusubiri mzigo uje Bagamoyo ndio upelekwe kule wakati Wana bandari kubwa na wapo karibu na Dubai ambapo kuna Transhipment. Somalia ni Tia maji wanasubiri bidhaa toka Dubai na Ulaya kwa kiwango Cha kawaida. South Africa hawawezi kuja sababu ya Cost na lazima hiyo meli iende kule sababu kuna mizigo mingi ya ku export ambayo ni mining products na agriculture products.
Sisi itakuwa ni sehemu ambayo meli inashusha mizigo mingi Kisha inaondoka na empty container au tupu kwakuwa hatuna bidhaa nyingi za ku export kadri ya ukubwa wa hizo meli.