Zitto Kabwe: Hayati Magufuli alikuwa ananichukia

Zitto Kabwe: Hayati Magufuli alikuwa ananichukia

ESCORT 1

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2015
Posts
1,412
Reaction score
3,043
Kiongozi wa ACT ndugu Zitto Kabwe akiwa katika kipindi cha Salama Na kinachorushwa Dstv, amekiri kuwa Hayati Magufuli alikuwa anamchukia sana.

Zitto ameongeza zaidi, Magufuli hakuwa na hekima, aliamini katika ubabe, hivyo nilianza kumpinga hapo ndipo chuki yake kwangu ilipoanza.

Zitto alifika mbali zaidi na kusema baada ya Lissu kupigwa risasi Dodoma mwaka 2017 ndipo alipoona kuwa Magufuli hana hekima hapendi kupingwa, hivyo Zitto akaongeza kumpinga hapo ndipo chuki ya Magufuli ilipozidi kwa Zitto.

Yaani hiki kipindi cha leo, Zitto kamsagia sana kunguni Mwendazake.

 
Zitto unasumbuliwa na udini tu.

Angejifunza kwa Shehe Ponda kusimamia ukweli

Kuliko kuwa mtu wa kuuma na kupuliza

Tunawaambia kila siku Achaneni na Mtu ambaye hawezi kujitetea tena.

Lakini kutwa kucha Magufuli Magufuli, Zitto ndio maana hata Kigoma hana ushawishi kabisa.

Nini kimebadilika ndani ya utawala huu zaidi ya upuuzi mtupu.
 
This man!

Halafu unamkuta naye huyu Mwanamaktaba wa huko karibu na Mwandiga yupo kwenye KAMATI Muhimu sana za Taifa, UMIMI mwingine unadumaza akili na kutofaa kuwa Mwanamapinduzi mwenye WAFUASI kabisa
 
Nimejiuliza hivi Salama na Zitto wote walijiamini nini? Kipindi cha leo Salama katoa airtime ya kutosha kwa Zitto kumsema Shujaa

Zitto anasema kama kuna Rais aliongoza kwa kujenga barabara basi ni Kikwete na sio Magufuli, hivyo watu waache kupotosha

Anasema Nyerere anakumbukwa kwa falsafa alizoziacha na sio miradi aliyojenga. Yaani leo Zitto kachafukwa mno
 
Zitto unasumbuliwa na udini tu.

Angejifunza kwa Shehe ponda kusimamia ukweli

Kuliko kuwa mtu wa kuuma na kupuliza

Tunawaambia kila siku Achaneni na marehemu kwani ni lazima tukiongea tumhusishe mtu aliyekufa tayari.

Jiwe hawezi kuachwa lazima uchafu wake usemwe ili vizazi na vizazi vimjue, ndio maana watu wake aliowaamini na kuwapa vyeo wanafungwa kama Sabaya
 
Nimejiuliza hivi Salama na Zitto wote walijiamini nini? Kipindi cha leo Salama katoa airtime ya kutosha kwa Zitto kumsema Shujaa

Zitto anasema kama kuna Rais aliongoza kwa kujenga barabara basi ni Kikwete na sio Magufuli, hivyo watu waache kupotosha

Anasema Nyerere anakumbukwa kwa falsafa alizoziacha na sio miradi aliyojenga. Yaani leo Zitto kachafukwa mno
Diallo ye alisema yule jamaa alikua na file lake kabisa Milembe.
 
Angemchukia asingemdekeza

Huyu jamaa alipewa first class care alipopata ajali

Kwa mdomo ule wenzake walinyoroshwa

Yeye alibaki anadunda na kuongeza wake tu
 
Muuaji mwendazake kafa
Zitto ni mwizi wa kisasa, nakumbuka enzi za akina Slaa Zitto alisumbua sana CHADEMA, mpaka akina Slaa wakawa wanamkaimisha ofisi Myika, Mpaka akina Kikwete wakamsaidia kumfungulia chama ili kuigawanya chadema. Bahati nzuri Magufuli alivyoingia tu madarakani alikuwa anajua mamluki wote, hivyo mamluki wote aliwasagia kunguni na ndio chanzo cha Zitto kuanza chuki na Magufuli. Zitto ni tapeli wa siasa tu, yeye kuuza mechi ili mkono uende kinywani haoni hasara
 
🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾👍🏽 Ayatollah Zitto kuna siku aliingia Maria Space akapewa nafasi ya kuzungumza alipomaliza alijua kutakuwa na maswali mengi basi akakimbia na hajarudi tena na sijui kama atarudi.

Wawe makini na Zitto ni ndumilakuwili na mnafiki wa kiwango cha SGR...

Zitto alimchukia Magufuli kwa kutoridhika na alichopata baada ya uchaguzi wa 2015!

Sio mtu wa kuaminika
 
Back
Top Bottom