Zitto Kabwe: Hayati Magufuli alikuwa ananichukia

Tunamweshimu Mbowe, ndo maana tunashindwa kusema ukweli...

Aliyeigawanya CHADEMA ni Mbowe na wala sio Zitto!!!

Zitto hata alipoondoka CHADEMA na kuunda chama chao na akina Mkumbo, wala hapakuwa na impact yoyote ya maana!! CHADEMA ilibaki kuwa ile ile!!

Mgawanyiko CHADEMA ulikuja baada ya kuja Lowassa... tuache unafiki!!

Kuja kwa Lowassa kukamfanya Dr. Slaa achafukwe!

Dr. Slaa alikuwa na wafuasi wengi sana CHADEMA, na alikuwa na ushawishi mkubwa maradufu... ni mjinga tu ndie atapinga hili!!!

Tukiacha unafiki, a moment Lowassa alipotangazwa kugombea urais, CHADEMA ikawa sio moja tena! Wengine waliingia kwenye uchaguzi mkuu 2015 huku wakiwa na vinyongo!!

Vinyongo vilikuwa vya namna mbili... mosi, ilibidi tu wakubaliane na ujaji wa Lowassa hivyo hivyo shingo upande, na pili, wengine walikuwa na kinyongo kwa sababu ya Dr. Slaa!!

Magufuli nae akaja kuendeleza tu kupiga kwenye kidonda kilichokuwa kimeachwa na ujio wa Lowassa ambapo akaanza kununua mpinzani mmoja baada ya mwingine ! Watu wakawa more demoralized hasa baada ya kuona hata huyo Lowassa mwenyewe akakaa mbali na chama mara baaada ya kupita uchaguzi mkuu!!

Huo ndo ukweli mchungu ambao watu mnakwepa kuuongea! Sio kwa sababu hamjui, bali ndo yale yale ya wana-CCM!! Hakuna kuwasema wakubwa!!
 
Dogo wacha kujichosha maana hivi sasa tupo kwenye awamu ya 6.

Hizo ndoto zako za kuabudu mambo ya awamu ya 5 zinakupotezea muda wako.
 
Hivi watu bado wanamsikiliza huyu dogo? Ukiwa mjinga na kumfuatilia Zitto basi umekwisha kiakili, huyu ni wa kuachana naye tu na ndiyo maana Salama alikuwa anacheka kama hataki vile. Kwa lugha nyepesi ni kwamba alimdharau tu dogo.
Tatizo la zzk hanaga aibu kabisa
 
Wewe ndio unaandika kiushabiki, Zitto ndio mwanzilishi wa migogoro pale chadema Kabla ya ujio wa lowassa,sema alizidiwa nguvu kwasababu kipindi kile chadema ilikuwa na nguvu,alianzisha Movement ya kugombea kuwa mwenyekiti wa Chadema akisaidiwa na Serikali ya Kikwete, chadema wakawa wanadukua mawasiliano yao na kundi lake,wakanzisha kundi yeye na akina Mwigamba na Kitila Mkumbo la MM1 kwa ajili ya kutukana viongozi wa chama, mpaka chadema wakaamua kumtimua, kwasababu akina Slaa walikuwa wamewachomeka akina Been Sanene wakawa wanaleta tarifa na miamala ilyokuwa ikitoka kwa Zitto kulipa kikosi chake,hata ukifukunyua humu unaweza pata uhalisia wenyewe.Zitto ni nyoka aaminiki.
 
Narudia, hakuna any negative impact ambayo ilisababishwa na Zitto! Yote hayo unayasema kwa sababu ile ile niliyoisema mwanzo kwamba hatutakiwi kumkosoa Mwenyekiti na ndo maana.kutaka kugombea uenyekiti unaona ni kuanzisha mgogoro!!!

Na wote ambao walijaribu kutaka kugombea uenyekiti... stori ni ile ile! Msaliti! Anatumwa! Analeta migawanyiko! Mambo ya aibu sana haya!!

Ukweli utabaki pale pale kwamba, harakati za Zitto hazikuleta athari yoyote CHADEMA! Ona hata hao unaowataja! Kitila Mkumbo alikuwa na nguvu ipi pale CHADEMA? Huyo Samson Mwigamba alikuwa ana nguvu ipi pale CHADEMA?!

Ajabu ni kwamba, waliowaaminisha hayo mambo, hivi sasa wengine wanakula pesa za serikali ile ile... huyu ni pamoja na Dr. Slaa! Wengine hivi sasa ni wabunge wa CCM au wanaohudumu ubunge kwa back-up ya CCM!!!
 
Weka takwimu kabisa ili ueleweke
 
Huwa nakuheshimu Sana, Technically, imagine this hypothetical scenario, angelikuwa amemuua mama, baba na mtu Yeyote aliyempendwa wako ungelisema tusimseme màrehemu, for that matter Magufuli?
Ni upumbavu ulippitiliza kimsema marehemu
 
Zitto ni kijana wa JK pamoja na akina J Makamba. Ni mpinzani wa kutengenezwa na hutumiwa kwa manufaa ya upande flani.

JamiiForums mobile app
 
Ujinga mtupu kusema mtu anakuchukia kwa sababu unamkosoa bila shaka ni kupinga maendeleo hatukatai kukosoa ila tunachukia watu wanaopinga maendeleo si enzi za jpm tu hata sasa tumechoshwa na siasa tunataka maendeleo tena yenye tija kwa taifa letu baadae sio upuuzi wa kutetea covid-19 ipo uhuni wa chanjo ndo tukupende ah wapi??
 
Hata kama kweli ndege ni mpya , the fact ni kuwa zoezi zima la ununuzi wa ndege liliendeshwa kwa usiri wa mtu mmoja , Watu wana uwezo wa kusema chichote kuhusu ndege hizo maana hakukuwa na uwazi .
Sasa amesha kufa tuambieni hela alizoiba Magufuli ziko wapi?
 
Samia anampenda
 
Mwenye kumuamini Zito ni mpuuzi, mtu alisha wahi kusema wanasiasa tusiwaamini bado utamuamini huyo zito wakati ni mwanasiasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…