Zitto Kabwe: Iundwe Tume kwa ajili ya ukiukwaji mkubwa wa Haki za Kibinadamu awamu ya 5

Zitto Kabwe: Iundwe Tume kwa ajili ya ukiukwaji mkubwa wa Haki za Kibinadamu awamu ya 5

Zitto alipopata fedha nyingi,akaziweka Dubai,alipewa na Serikali ipi,nimesahau?
Kwani wale walioua watu walikuwa hawajui kwamba wapo majaji katika nchi hii?
Sheria za nchi toka lini zikawahusu Watu wa Usalama wa Taifa?
Magufuli ameingia madarakani,amewaongeza walinzi wake mishahara,katika kuonyesha shukrani zao,wameua watu left and right? Sasa,utawafanys nini wauaji? Unataka Rais Samia awakamate walinzi wake? Awakamate na nini? Awakamate na walinzi wengine?
Swali hapa Ni utaratibu gani unatumika kuamua nani ni mhalifu na utaratibu gani unatumika kumuadhibu.
Kibaka akiiba,anapelekwa jela,basi. Mhaini akikamatwa,anapelekwa jela,anayesema. Siyo kufungws tu: anafungwa na kuteswa.
Hapa Kuna kuna fujo. Unsongea kuhusu mkuu wa Usalama wa mkoa,ambaye pia Ni mkuu wa mkoa. Hiyo ni fujo. Mossad wakitaka kumuua mtu,wanaongea na Waziri Mkuu tu.
Siku hizi,hainikubwa Ni mwanachama wa Upinzani.
 
Amekuwa kama wasanii wa bongo washajua wakitaka kiki nzuri imuhusishe diamond.

Ndio Zitto kumuongelea Magufuli kunampa kiki ya kuzungumziwa kwenye siasa za kitaifa.

Vinginevyo bila ya kumtaja Magufuli watu wenye interest nae ni Lissu na Lema (mainly due to personal grudges) maana ata hao CDM waliopo nchini kwa wingi wao hawana habari nae kesha doda kama mwanasiasa.
 
Kuna haja kubwa ya kuundwa kwa Tume ya Majaji kwa ajili ya kuwapa nafasi waathirika wa vitendo vya ukiukwaji mkubwa wa Haki za Binaadam vilivyofanyila wakati wa utawala wa Rais Magufuli kupata Haki zao. Watu ambao wamepoteza ndugu zao, waliotekwa, waliobambikiwa Kesi nk. MUHIMU

I repeat a call for a commission of inquiry, to headed by a retired Judge of Court of Appeal, on atrocities committed during the tenure of J P Magufuli administration. All Killings, abductions, disappearance of people, trumped up charges of money laundering MUST be investigated

Huyu jamaa amebakiza za unafiki na udini tupu.Ukiunda hiyo tume ,viongozi wote waliokuwepo katika serikali.Na Sasa wapo serikali.Wanatakiwa kukaa pembeni.Serikali si mtu mmoja ni viongozi wote.Kwa hiyo mama pia akae pembeni.Makamu wa Rais pia akae pembeni.Zitto mnafiki Sana,ndio maana cdm wakimtumia.
 
Halafu utadhani maisha yalianza 2015 wakati wakina Dr Ulimboka walitekwa na kung'olewa kucha awamu ya nne.Kuna watu walimwagiwa tindikali,kulishawahi kuwa tuhuma za wanasiasa kulawitiwa katika kampeni za chaguzi ndogo.Kuna watanzania waliofukiwa katika machimbo ya madini.

Hiyo tume ianze kufanya kazi kuanzia mwaka 1985.Wakina Pinocchet walitenda makosa miaka mingi sana iliyopita wakala mshahara wao.

Huyu Zitto Kabwe anatumika na baadhi ya watu ndani ya CCM.Hatutokubali pesa za walipa kodi zitumike kwa mizaa na malengo ya wapumbavu wachache wa nchi hii.

Unaogopa nini kama Magufuli alikuwa mtu mzuri, hapo si ndio sehemu usafi wake utaonekana? Yeye kaamua kuanzia 2015, ww unaweza kuamua kuanzia hiyo 2015 kurudi nyuma.
 
Amekuwa kama wasanii wa bongo washajua wakitaka kiki nzuri imuhusishe diamond.

Ndio Zitto kumuongelea Magufuli kunampa kiki ya kuzungumziwa kwenye siasa za kitaifa.

Vinginevyo bila ya kumtaja Magufuli watu wenye interest nae ni Lissu na Lema; ata hao CDM waliopo nchini hawana habari kesha doda kama mwanasiasa.

Mbona cdm tupo na tunakubali hizi jitihada zake tuone unyama aliofanya yule kiongozi muovu.
 
Mbona cdm tupo na tunakubali hizi jitihada zake tuone unyama aliofanya yule kiongozi muovu.
Common denominator hapo inayokufanya utoe support ni Magufuli sio Zitto.

Ndio maana nikasema ili apate kiki za kitaifa inabidi amuingize Magufuli.

Je CDM wewe kama una fuatilia siasa za Zitto juzi kazindua baraza lake la mawaziri sijui wasemaji; unamjua msemaji wa ACT wa maswala ya afya? Nakupa muda you can google too.

Sasa nikikwambia nitajie wasemaji watano wa ACT wa wizara tofauti si nakuwa nimekupa mtihani.

Zitto amesha chacha sasa hivi anatumia mbinu za wasanii wenyewe wanakwambia hakuna kiki mbaya wala nzuri; Magufuli anampa kiki ya kuzungumziwa kitaifa.

Mtu keshaondoka bado tu khaah.
 
Zitto mjinga mjinga kweli ,wewe unasikia mtwara huko sijui polisi kauwa raia na kuchuwa pesa yeye anahaika na kiumbe kimeshajifia huko na kujipumzikia,hapa tunataka upinzani wa kweli na siyo huu uchwara nyambafu....!uje hapa utumbie madudu kwenye ripoti ya CAG Nini tukifanye kama wananchi unatuletea ujingaa hapa.

Acha kupanick, taarifa za dhalimu ni lazima ziwekwe wazi.
 
Common denominator hapo inayokufanya utoe support ni Magufuli sio Zitto.

Ndio maana nikasema ili apate kiki za kitaifa inabidi amuingize Magufuli.

Je CDM wewe kama una fuatilia siasa za Zitto juzi kazindua baraza lake la mawaziri sijui wasemaji; unamjua msemaji wa ACT wa maswala ya afya? Nakupa muda you can google too.

Sasa nikikwambia nitajie wasemaji watano wa ACT wa wizara tofauti si nakuwa nimekupa mtihani.

Zitto amesha chacha sasa hivi anatumia mbinu za wasanii wenyewe wanakwambia hakuna kiki mbaya wala nzuri; Magufuli anampa kiki ya kuzungumziwa kitaifa.

Mtu keshaondoka bado tu khaah.

Ni hivi, Zito yuko sahihi kwa haya madai yake. Hao wasemaje wake mimi siwajui wala sitaki kuwajua. Hao mawaziri tu wa hii serikali ya mijizi ya kura siwajui wengi, ndio itakuwa wasemaji wa chama cha Zito?
 
Huyu jamaa ni bwege sana tena mpenda sifa kupindukia. Siku moja nilikuwa zanzibar hoteli moja ya Mazrui , Maalimu seif na viongozi wengine wa upinzani walikuwa na kikao hapo hotelini na zito alikuwepo. Baadae alitoka nje ya kikao akanikuta nimesimama naangalia vitabu vya Prof Shivji alikuwa amevitandaza anauza. Basi Zito alinifuata na kuniuliza Kamanda unasemaje? Vipi Zanzibar, Vipi Mambo mimi nikabaki namshangaa wala sikumuitikia kwanza yeye hanifahamu mimi kabisa kwa nini aniite mimi kamanda. Huyu anajifanya ni msomi lakini ni hopeless
 
Ni hivi, Zito yuko sahihi kwa haya madai yake. Hao wasemaje wake mimi siwajui wala sitaki kuwajua. Hao mawaziri tu wa hii serikali ya mijizi ya kura siwajui wengi, ndio itakuwa wasemaji wa chama cha Zito?
Sishangai unaposema huwajui, yet Mbowe katoka juzi akikutana na ma padre kila mtu anajua, sasa hivi yupo sijui na campaign gani watu wanajua.

Zitto anafanya nini, no ones knows nje ya matukio ya kitaifa. Jina linakuja kutokana na mambo ya kitaifa lakini sio mikiki-mikiki ya chama chake.

Ajabu ni kwamba na bado unaikataa point yangu niliyosema; hata CDM hawana interests na movements za Zitto na wala huwa hawajui anafanya nini for the most part.

Kilichobaki kwake ni kutumia kiki ili asikike na kwa sasa hakuna mtu mwenye kuitoa hiyo kiki kama unapomzungumzia Magufuli.
 
Kwanini tusianzie awamu ya nne tuchunguze uhalali wa kesi ya Babu Sea,Kuvamiwa na kupoteza jicho kwa Kibanda, kuteswa na kutupwa msituni kwa Dr Ulimboka na kifo cha utata cha Chacha Wangwe alafu baadaye tuamie awamu ya tano.
 
Na iundwe tume huru ya kuchunguza mazingira ya kifo cha hayati John Pombe Magufuli.binafsi sijaridhishwa na maelezo juu ya kifo chake.
Mkuu Magufuli amefariki bila mkono wa Mtu.
 
Kuna haja kubwa ya kuundwa kwa Tume ya Majaji kwa ajili ya kuwapa nafasi waathirika wa vitendo vya ukiukwaji mkubwa wa Haki za Binaadam vilivyofanyila wakati wa utawala wa Rais Magufuli kupata Haki zao. Watu ambao wamepoteza ndugu zao, waliotekwa, waliobambikiwa Kesi nk. MUHIMU

I repeat a call for a commission of inquiry, to headed by a retired Judge of Court of Appeal, on atrocities committed during the tenure of J P Magufuli administration. All Killings, abductions, disappearance of people, trumped up charges of money laundering MUST be investigated

Ama kweli, ukipenda chongo, huita kengeza, hivi Mbowe alibambikiwa kesi awamu ya tano? Mfanyabiashara wa madini kule Mtwara aliyeuawa na Askari Polisi naye ni awamu ya tano? Huyu Wakili sijui Madeleka naye ametekwa awamu ya tano? Au yaliyotokea awamu ya tano inahusika Serikali lakini ya awamu ya sita Serikali haihusiki, huyu ZZK ni mchumia tumbo, hizi double standard ni manufaa binafsi au ya Watu?
 
Awamu ile ilikuwa ni ya kishetani naona hata nchi kutoka gizani itachukua muda sana.
 
Kwanini tusianzie awamu ya nne tuchunguze uhalali wa kesi ya Babu Sea,Kuvamiwa na kupoteza jicho kwa Kibanda, kuteswa na kutupwa msituni kwa Dr Ulimboka na kifo cha utata cha Chacha Wangwe alafu baadaye tuamie awamu ya tano.
Huyu jamaa ni mpuuzi, yaani yeye chuki zake na awamu ya tano anataka kuaminisha watu upuuzi wake kwamba ndiyo ilikuwa ya hovyo kuliko zote? Kwamba yaliyotokea awamu nyingine Serikali haihusiki ila yaliyotokea awamu ya tano Serikali inahusika, anatumika vibaya huyu.
 
Mabomu ya kivita kwenye mkutano wa Chadema? Au wale hawana haki? Dr Mvungi? Alphonce Mawazo? Unajua sometimes hawa wanasiasa wanatuona punguani sana.
Kuna watu wanawaamini hao wanasiasa yani haumwambii kitu, kuna watu unakuta ukimsema Lissu au Mbowe basi anaweza hata kukutukania mzazi wako.
 
Kuna haja kubwa ya kuundwa kwa Tume ya Majaji kwa ajili ya kuwapa nafasi waathirika wa vitendo vya ukiukwaji mkubwa wa Haki za Binaadam vilivyofanyila wakati wa utawala wa Rais Magufuli kupata Haki zao. Watu ambao wamepoteza ndugu zao, waliotekwa, waliobambikiwa Kesi nk. MUHIMU

I repeat a call for a commission of inquiry, to headed by a retired Judge of Court of Appeal, on atrocities committed during the tenure of J P Magufuli administration. All Killings, abductions, disappearance of people, trumped up charges of money laundering MUST be investigated

Mimi naunga mkono kabisa hiyo tume iundwe haijalishi nani kashauri hilo jambo hakuna asiyejuwa chini ya utawala wa dikteta magufuli watu wengi wegi walipotea, kuuwawa, kuteswa, kupotea wengine mpaka leo hawajulikani walipotea ndio maana tunataka tume huru Ili tujuwe nani walihusika na uharamia huu katika nchi huru kabisa ili mambo haya Yasije kutokea tena .
 
Kuna watu wanawaamini hao wanasiasa yani haumwambii kitu, kuna watu unakuta ukimsema Lissu au Mbowe basi anaweza hata kukutukania mzazi wako.
Sasa wewe kama wanasiasa hawakuhusu unawasema wa nini?? Nenda kamseme Diamond? Alikiba na Konde boy huko ndio level yako.
 
Back
Top Bottom