Zitto Kabwe: Katika ndege 12 alizonunua Hayati Magufuli, ndege 6 hazifanyi kazi, ziko grounded, zina kutu, ingawa tuliambiwa ni mpya

Zitto Kabwe: Katika ndege 12 alizonunua Hayati Magufuli, ndege 6 hazifanyi kazi, ziko grounded, zina kutu, ingawa tuliambiwa ni mpya

Sasa ndege inarushwa bila kufanyiwa service na hata bajeti ya service watu wanapiga unategemea hiyo ndege hata kama ilikuwa mpya itakuwa imara tena?

Unajua muda mwingine huwa natazama umashuhuri wa huyu jamaa zitto kabwe kwasasa ndipo nagundua jamaa hana jipya la kuoffer kwenye political platform ya Tanzania zaidi ya kuongea vitu ambavyo havina ukweli.

Sasa wewe watu wanaiba mabilion ya pesa sasa hivi huwezi sikia akikazania. Ila kila anapokwenda yeye ni magufuri hiki magufuri kile yaani utadhani yule mzee alimgongea mkewe sasa anakisirani naye. [emoji23][emoji23][emoji23]

Jamaa ni mpumbavu sana huyu miaka hii sijui ndio wenge la umri kwenda.

..jibu hoja bila kumtukana Magufuli na Zitto.
 
Zile ndege zote kwa jumla hazifiki hata trilioni mbili. Hii ni hela ambayo kwa kutazama ile miamala aliyokuwa anaikusanya kwenye malipo ya kodi mbalimbali huku chini ukichanganya na vyanzo vingine kama malipo ya tanesco, na makampuni mengine yaani hiyo ni hela ndogo sana.

Tatizo letu watanzania huwa kutumia akili sijajua tunafeli wapi. Ni kwann kipindi cha magufuri waliokuwa wakilalamika sana kupita maelezo hadi michozi walikuwa ni viongozi, watoto wao, hawa viongozi wa upinzani, wamiliki wa NGO's, baadhi ya wafanyabiashara wakubwa etc na wananchi wa kawaida walikuwa poa tu na wengi wao hawakuwa wakipitia hali kama ya sasa.

Haujiulizi kwann sasa hivi hawa viongozi wakubwa, wadau wao, washirika, viongozi wa upinzani etc, wanashindwa kumtamka magufuri hata kwa zuri hata moja, ingawa mambo aliyofanya mengine yanawafaidisha kwa sasa?

Kimsingi kuna siri nzito sana inafichwa na hili kundi la mchwa ambalo wanataka wao pekee yao ndio wafaidike na rasilimali za hili taifa. Kwakifupi hawa watu wameshakuwa compromised inapokuja swala la masilahi ya taifa.

Zile ndege ni chache sana kwa idadi ya mikoa tuliyo nayo. Lengo kuu ni kila mkoa at least uwe na ndege mbili au tatu ambazo zinapiga safari ili kuboost Biashara na mawasiliano. Hizi ndege aina ya bombardier ni ndege nafuu sana kumaintain na hazina usumbufu kama watu wanakuwa serious na biashara.

Zile story za sio lazima kununua ndege unaweza kukodi ni story za kibiashara tu. Unaweza kununua ndege zako hata mia ukiwa na watendaji wazuri faida utaiona na utakuwa na afadhali kuliko yule anayekodi. Sema watanzania tuna kasumba moja, yaani jambo akisema mzungu basi linakuwa kama ibada yaani mwafrika hawezi waza nje ya akili ya maneno ya mzungu.

Mzungu alisema ukitembea kwenye jua kali la mchana utapata kansa ya ngozi. Ofcourse ni kweli ila kwa mtu mwenye albinism na wazungu wenyewe hili jua lina madhara. Ila waafrika unakuta nao wanacopy hii habari wanapakaa sunscreen kwenye ngozi ili watembee juani sasa wewe jua likikupiga una melanin ambayo inafanya ulinzi wa ngozi yako bila hata wewe kuwaza chochote unahangaika na sunscreen ya kazi gani? Machinga wote na wakulima wanaoshinda juani si wangejaa pale Ocean road kutibu kansa ya ngozi.

Juzi kati wakati wa korona, Magufuri akawakataza lock down mkasema vibaya mzee wa watu kuwa hajielewi sijui nini na nini, mzee alikomaa kweli kweli, mwisho wa siku aibu ikawarudia wanaharakati wa mchongo. Corona mbona haikusambaa na kuua inchi nzima?!

Wazungu wameshika sana vichwa vyetu kiasi kwamba tunaamini wapo accurate kwa 100% kumbe sio kweli na always hiyo haiwezi tokea. Tuwe tunatumia akili zetu.

Hawa viongozi uchwara akina Zitto wanalipwa kufanya uhaini ninyi mnawaona icon.

..Magufuli alikuwa anatumia kifaa cha kusaidia mapigo ya moyo kilichotengenezwa na wazungu, halafu anakuja mtaani anasema yuko vitani na wazungu mabeberu.
 
Mimi hayanihisu hayo
Wewe umekuwa mnajimu au mganga kujua kuwa mimi ni mmoja wenu huko?

Ukiwa mtu wa dhana ni moja ya unafiki
Jifunze kutokudhania mtu badala yake andika kwa wahusika tu

Mimi niko nje ya nchi tangu 1989 hizo siasa zenu mmalizane wenyewe

Kwa kukusaidia humu wamo mpaka wabangaladeshi na mpaka walioko Mexico wanachangia humu
Jifunze kujadili kwenye mitandao huru
Nimechangia hoja tu mengine mtapambana wenyewe

Wizi wa hizo ndege tunajua sasa nini kifanyike ndio suala Zima hapa
Na sio mapambio

Huna utakaoifanya maana uko nje ya nchi. Rudi uje uonyeshe nini kifanyike. Kwa sasa endelea kubeba box huko.
 
Ulitegemea ziwe grounded lini ? Kama service hamna unataka ziruke vip , hata kama ni mpya unajua service schedule yake , ndege sio Gari , hlo shirika wamedhamiria kuliua , na watu wanashangilia , ogopa sana kundi la wajinga
Serikali ndio yenye jukumu ya kufanya hizi service maana ndio mmiliki na sio shirika.

Amandla...
 
Kama ndege sita zipo grounded, hilo haliwezi kuwa kosa la Magufuli, tatizo la Zitto amekariri kila siku kutupa lawama kwa mtu mmoja ambaye kwa sasa hayupo, na kumlinda yule aliyepo, akidhani wote hatuna akili.

Hizo ndege kama zimekosa matunzo, na sasa Magufuli amefariki karibia miaka miwili iliyopita, Zitto anatakiwa ajue wakuwalaumu ni hawa waliopo kwa matunzo mabovu ya hizo ndege, na sio yule aliyezinunua, bila kujali kama ni mpya au mitumba, kwani waswahili husema kitunze kidumu, sio unashindwa kukitunza, halafu unamlaumu aliyenunua!.

Anachofanya ni kama ujinga wa watoto kumlaumu baba yao kwa ubovu wa nyumba aliyowajengea baba yao aliyefariki, wakati wao ndio waangalizi wa nyumba hiyo, ujinga wake ni kutumia kigezo cha wingi wa ndege kama sababu ya hizo ndege sita kuwa grounded, hoja ya kijinga kabisa.
Kama hakuwa ruhusu waongee wakati zinanunuliwa kuna kosa gani wakiongea leo. After all Zitto smezungumxia mchakato mbovu wa manunuzi na Ndege 6 kuwa grounded. Huko siyo kusema Magufuli bali ni kuibua uozo kipindi kile. Hata Maza majuzi katuibulia Mamilioni kupelekwa China... Huko nako ni kusema Magufuli..!? Mwbieni CAG aache kutoa report za Awamu ile kwa kuwa mwenyewe hayupo.
 
Serikali ndio yenye jukumu ya kufanya hizi service maana ndio mmiliki na sio shirika.

Amandla...
Wakati zinakuja kwa mbwembwe na kupiga push up Airport waliona sawa. Leo wanaona tatizo kukosolewa. Hivi toka lini ndege mpya ikawa grounded in less than 5 years. Ndege zinadunda zaidi ya miaka 30. Hata MaV Eighty yao 5 years bado yanaonekana mapya.
 
Tatizo siyo kupanda au kutopenda ndege, na wala siyo kununua ndege zilizotumika. Lakini inatakiwa ifahamike:

1) Ni kweli ndege zilizonunuliwa zilikuwa zimetumika?

2) Kama.zilinunuliwa zimetumika, kwa nini tulidanganywa kuwa ni mpya?

3) Kama zilikuwa mitumba, pesa tuliyoambiwa imetumika kununua ndege mpya, yote ilipelekwa kwa muuzaji au kuna watu waliipiga?

4) Waliohusika na huo ununuzi na malipo, kwa nini wasihojiwe ili watoe ufafanuzi juu ya hayo yote?

Kuharibika kwa kitu chochote si jambo la ajabu, lakini kuharibika kwa ndege 6 kwa kipindi kifupi namna hii, ndege zilizokuwa mpya, si jambo la kawaida. Hii sasa ni zaidi hata ya magari ya kichina.
Kwani we unamuamini nani kati ya zito na serikali.
Tuanzie hapo,
Angesema treni ningemuelewa sababu wote tuliambiwa tutaamza na mitumba kwanza.
 
Kama zina kutu mbona sa mia kanunua mabehewa ya treni ya mitumba na zito asemi kitu tena kanunua kinyume na sheria za nchi kuhusu serikali kununua vitu used ...pia kwanini asinge mlaumu Samia kwa hizo ndehe kupata kutu na kuto kuruka wakati wa jpm zote zilikuwa zinafanya kazi au ana dhani watanzania ni wapumbavu wenzake..... blodi shiti .
Jamaa anachuki za kipumbavu alafu halinaga aibu.
 
Huyu mpumbavu hana kitu ingine ya kuongea?
Magufuli hayupo sasa tufanyeje tena sisi wananchi.
Badala ya kusema sera zao za chama yanarudi kulekule Magufuli blaah blaah ssi inatusaidia nini?
Ndio hawa wasomi mnawategemea wapiga ramli
 
Okay kweli jamaa alifanya jambo baya sana ila ameondoka sasa...

Vipi hawa waliopo sasa wanaotafuta Crane ya Kumaliza Bwawa kama sindano kwenye haystack ?, Vipi wanaopanga kufumua Shirika la Tanesco na kulijenga upya kwa matrillioni hao tutawazungumza lini ? Au tunangoja baada ya miaka kumi wakishaondoka ?!!!!
 
Back
Top Bottom