Zitto Kabwe: Kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli ni kujipendekeza na unafiki

Zitto Kabwe: Kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli ni kujipendekeza na unafiki

Pascal Mayalla,
"Mimi namuunga mkono Zitto, haki haiombwi wala hailetwi kwenye kisahani cha chai, inadaiwa".

Mwambie Zitto na chama chake wapambane kudai haki KWA NJIA HIYO UNAYOONA INAFAA balada ya kuijadili CHADEMA.Aache siasa za kujibanza ubavuni mwa CHADEMA.Wakati wote CDM inapambana kudai haki,yeye(Zitto) alikuwa upande wa watawala lakini hatukusikia CDM ikiilalamikia ACT-Wazalendo yake.Wenzake kila siku wanashinda mahakani,yeye anashinda twitter, halafu anajifanya anapambana kudai haki.Akisikia fununu ya kukamatwa na polisi,anatimua mbio kujificha au mara watakuta bwawa.Uoga Uoga tu.
 
Chadema wamefanya jambo jema kinachomsumbua zitto ni wivu na unafiki wote tunajua tangia zitto aingie upinzani hajawahi kushiriki maandamano wenzake wamefikiria mbali wanautazama uchaguzi ujao kwa jicho la tatu sanasana zitto ategemee kubebwa na kina seif huko zanzibar ila huku bara hatapata kitu
 
Egnecious, Nani kakueleza kiwa serikali hii ina lengo la kukuondolea lindi la umaskini na ufukara???

Huyo jirani yako kama ni mcongo+mburundi tunaaminije kama wewe jirani yake pia si mburundi au mcongo? Unafikiri hao uhamiaji wao ni wajinga kuliko wewe hata wabaini jirani yako si raia halafu wamuache? Umeharibu kuongea tuhuma usizokuwa na uthibitisho wake.
 
Nyie mikutano mnazuia, sasa chadema mnataka wafanyaje, akili kubwa wamewasubiri mukusanye watu wenyewe tena mbele ya jiwe, halafu wakaitumia hiyo fursa vizuri,

regardless hiyo siku ilikuwa ni muungano au uhuru wao kwao cha muhimu ni kupata jukwaa la kusema hicho walichokisema tena mbele ya muhusika mkuu,

hivi mnafikiri hicho walichokisema walishindwa kuitisha waashishi pale kinondoni na kusema? Tena pale wamepata live coverage karibia media zote, wafikiri hiyo nafasi wangeipata wapi.
 
Nashangaa kwanini CHADEMA hawajioni kama wamekosea. Yani Mbowe kawa Mungu mtu. Mnampigiaje magoti mtu aliyewafanyia kila aina ya unyama????
Hili jambo linashangaza sana. Sikutegemea Chadema wangefanya vile, wanampa legitimacy mtu anayetufanyia (sisi na wao) vituko vya ajabu kabisa. Eti wanamuomba demokrasia, sijui maridhiano, blah blah..
 
Huyu ndio Zitto.
IMG_20191209_165135.jpeg
IMG_20191209_165119.jpeg
IMG_20191209_164943.jpeg
 
Egnecious,
Nimesoma makala yako hii fikirishi na kurudi nyuma miaka takribani 47. Naamini kabisa kuwa hili siyo jambo la siri na wewe, kama mtu unayeifahamu vema familia ya Zitto Zuberi Kabwe unaweza kuondoa utata!, Ningekuomba unisaidie kuhusu hili kwa nia njema ya kujiridhisha tu.

Nilimaliza elimu yangu ya msingi mwaka (1972) na nilisoma na mtu mmoja mfupi anaeitwa Zuberi Kabwe pale shule ya msingi Muungano iliyoko Mwanga, Kigoma. Alikuwa anafahamika kama "Mbembe" na alikuwa akihudhuria masomo akitokea Mwandiga kila asubuhi na kurejea huko alasiri baada ya masomo. Naomba kujua kama unajua iwapo ana uhusiano wowote na huyu ZZK mwanasiasa. 🙏🙏

Niliishawahi kumuuliza ZZK mwenyewe zamani kidogo, hajanijibu hadi siku ya leo. Nadhani kwa mada hii naweza kujifunza kitu zaidi na pengine wengine kujifunza kile wasichokijua.🤔🤔
 
Pascal Mayalla,
Mbowe ametumia ile option ya kujitundika mwenyewe. Maridhiano kwanza ikishindikana twende ulingoni HAKI itadaiwa kwa nguvu na mbinu zote.

Kwa mtawala asiyeielewa demokrasia kama JPM ni muhimu akapata wasaa wa kuelimishwa kwa njia mazungumzo yaliyo ndani ya maridhiano. Akishaelewa then ndiyo hatua muafaka za kudai haki kwa mbinu zote zikiwepo za Zito za "naming and shaming".
 
Hatulazimishwi kuwa na mitazamo sawa humu. Niseme tu, Chadema na wapinzani wengine wasitegemee kupata haki katika zama hizi za uporaji wa chaguzi,mauaji,utesaji,utekaji na kesi za kubambikiana. Watu wanaofanya dhuluma deliberately hupaswi kusimama nao majukwaani.
Kwenye uzi huu Zitto anashambuliwa na ataendelea kushambuliwa, lakini mimi tangu nishuhudie yale ya jana nimejikuta na mtazamo kama wake.
Nchi hii kwa sasa wapinzani hawawezi kupata haki on a silver platter. Watu wawe realistic.
 
Zitto anabadilika sana,huwezi jua ana simamia nini, yaani hata Maridhiano hayataki? mwambieni yeye na familia yake waandamane kuitafuta haki sio kudanganya watu wengine, njia waliotumia upinzani jana ni sahihi na bora , kukaa mezani na kujadiliana ni sahihi kabisa.
 
Egnecious,

Hekaya hii ndefu haiondoi ukweli kuwa Magufuli ndio anavuruga nchi yetu na yeye ndio hasa atapeleka nchi hii kwenye machafuko. Kitendo cha viongozi wa cdm kwenda kwenye hizo sherehe huku uchaguzi ukiwa umenajisiwa waziwazi ni kufuta madai yao ya msingi. Tunamuunga mkono Zito kwa msimamo huu hata kama tunajua ni mnafiki.
 
Pascal Mayalla,

Nakuunga mkono kwa asilimia mia moja. Mbowe kachemka na hilo halina mjadala, sijawahi kuona popote ufanyiwe uhuni ww, kisha unaenda kuomba maridhiano na mtu anayekufanyia uhuni. Bado naendelea kuamini muda wa Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm umeshapita, hana mbinu mpya zaidi ya kujisalimisha kwa Magufuli.
 
Back
Top Bottom