Zitto Kabwe: Kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli ni kujipendekeza na unafiki

Zitto Kabwe: Kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli ni kujipendekeza na unafiki

Pascal Mayalla,
Kwani wasingelijitowa kwenye ule uchaguzi,ndo uhakika kuwa wangelipewa ushindi na CCM ,si ingelikuwa wameuhalalishia dhalimu kuonekana una haki!
Mbowe alicho fanya ni sawia kwa mustakbali wa Taifa lenye kiongozi Asieheshimu haki za wengine wala Demokrasia.
 
Mbinu anazotumia mbowe ni bora kuliko wanasiasa wote tz.na siasa za mbowe si za umwgaji damu. Na alichoongea hakuna neno lililomaanisha kujipendekeza Bali kuwakilisha mawazo ya maridhiano ambacho ni chakula muhimu ktk kudumisha amani ya taifa. MsemajiUkweli,
 
Mimi mwenyewe moyo wangu umesononeka na kuumia Sana wakati naona Magufuli hayuko tayari kuona upinzani nchini.
Magufuli ameua,amefunga wapinzani,amepoteza watu na kujeruhi wapinzani kwa Risasi Leo CDM kirahisi wanasema wanataka maridhiano na CCM hapo wameingizwa chaka,umehalilisha utawala unaokandamiza haki za watanzania.
Kwako wewe ungependekeza njia gani itumike ktk kuikomboa Tanz yetu?? Ungependa tutunishiane misuli hadi lini huku wenzetu wakizidi kuumia? Je endapo maridhiano yatafanyika si ndiyo mwanzo wakujua hatma ya Ndugu zetu waliopotea hadi hivi leo? Je wewe unaona ni bora Mh Lissu aendelee kuwa nje ya nyumbani kwake hadi lini? Hapo kwenye meza ya maridhiano si ndiyo mahali pake? Je wewe unafikiri kwenye meza ile watakao keti kutafuta maridhiano ni Wenye Viti wa Vyama pekee bila kuwa na Watu wa pembeni wenye Hekima, Busara na Uzalendo wa kweli ktk kujenga Demokrasia Nchini?
 
Kwenye kitabu cha ‘The Republic’ by Melissa Lane; Plato ana argue democracy is good lakini si ya Athenians at the time.

Madai yake ni kwamba aiwezekani watu wasio na uelewa ndio wawe waamuzi wa mambo muhimu ya nchi wakati hawana reasoning capacity na wengi ufuata mkumbo tu. Akatoa mfano wa mji ulioleta fujo; kwenye kikao iliamuliwa wanaume waadhibiwe kifo, watoto na wanawake wawe watumwa. Maajabu yake watu hao hao kesho yake tu wakafuta maamuzi yao.

Anauliza ni sababu zipi za logic ziliwafanya wananchi waamue na kufuta maamuzi yao. Jibu hakuna ni hisia tu za watu wachache wanaosimama wakipewa nafasi ndio wana influence asilimia kubwa ya wapiga kura na wote hawana qualification za kutoa argument sahihi kwanini kitu fulani kifanyike.

Hizi ndio siasa za upinzani Tanzania watu wanaotetea maamuzi ya Mbowe ya kipuuzi leo ndio hao hao pia watatea ya kipuuzi kesho.

Solution kwa Plato nchi lazima ziendeshwe na philosophers just for the sake of making the right decisions. Bado naamini Mbowe anastahili nafasi kubwa ndani ya CDM bali not decision making he just doesn’t have it.
 
Pascal Mayalla,
Ok, Labda wewe mkongwe utakuwa unafahamu vizuri, Em niambie wangetumia njia zipi kuidai hiyo haki ?!?! Maana naona wengi wenu mnasema njia hii ni ya kuomba poo, lakini hamsemi njia ipi ingetumika ..?! Ikumbukwe mambo mengi wameshafanya, Matamko, kususia, kutoshiriki mambo mbalimbali n.k !! Chama kilichoomba poo (Kwa mnavyodai nyie) ni kimoja tu CHADEMA, Kwanini hamtoi ushauri kwa vyama vingine kuidai hiyo haki kwa nguvu zote jino kwa jino ili mwisho wa siku huu wito wa CHADEMA utaonekana wa kiboya, na sisi wananchi tutachagua upande wa kuunga mkono..!! Nasubiri majibu yako🤔🤔🤔
 
Ni kweli kuwa Mbowe ame-surrender na ninavyomfahamu Magufuli ana ile mentality ya the winner takes all, atataka maridhiano na upinzani kwa masharti yake ikiwemo wapinzani waunge mkono juhudi.

Mbowe hapo wamefanya costly blunder kwani hii hali inamfanya Magufuli aamini kuwa mkakati wake wa kuiangamiza upinzani unazaa matunda.

Hata Magufuli akiridhia kufanya nao hayo maridhiano wanayohitaji wajue wao watakuwa wanaongea huku wakiwa wamesimama kwenye very weak ground and Magufuli is the one who will be calling the shots....!!!!

Kama Mbowe and co, are the ones people were expecting to pioneer the way to bring this government to heed their wishes then they are on the wrong side of bargain.

Kwa kauli hizo za upinzani ni wazi sasa serikali hii itapata pa kupumulia kwa kuwa wamehalalisha ionekane kuwa ni kwa ridhaa ya rais tu ndio muafaka wowote wenye kuathiri maslahi ya taifa unaweza kupatikana.

It's short of what the reasonable people can expect, Mbowe and co are very very wrong to give Magufuli and his henchmen a spurious victory, the undeservedly victory they appear to be getting without even kicking a ball. Very saddening indeed.
 
RUSTEM PASHA, Mkuu Mh Mbowe hakumtizama Magufuli kama Yeye au M/K wa ccm bali kama Kiongozi Mkuu wa Nchi mwenye Mamlaka Kikatiba kwa mujibu wa Sheria za Nchi yetu. Hivyo Mh Mbowe hakumuomba Magufuli maridhiano bali Kiti alichokikalia Mh Magufuli kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanz.
 
Pascal Mayalla,
Wewe upo tayari kudai? Au unaandika kishabiki maandazi tu.Tunakupuuza tu kwani huna jipya zaidi ya kujipendekeza tu. CHADEMA ni zaidi ya akili yako hivyo nakushauri uendelee kutibu tumbo lako tu.
Eti mwandishi huru huku umejaa unafiki na kujipendekeza tu.
 
Jicho la mbali,
Kinachowasumbua Chadema ni kesi ,
Wakijifanya wanapambana na jiwe jino kwa jino
Watakwenda kweli segedensa
Kuna mtu mkubwa kawashauri wajitafakari na kisha waungane na jiwe, katika kujenga nchi
Na jiwe atawaonea huruma na
kesi yao itafutwa kimya kimya..
Mtoto wa mjini ukiona maji mazito unatafuta chocholo..
Kwenye kesi umechemka Mkuu kwni hawaogopi kufungwa. Kwni kufungwa kwao itakuwa ni kielelezo tosha kwa Dunia kuwa Tanz inaongozwa na mtu wa namna gani. Mh Mbowe alishasota rumande kwa miezi zaidi ya mitatu na nado ni yule yule wa jana na leo.

Wao kama Wapinzani wako mlangoni wanabisha hodi ili aliye ndani aamue kufungua mlango wangie ndani wazungumze au awafungulie mbwa awashambulie.
 
Na wewe hutaki maridhiano yawepo ili watu waendelee kuuliwa?? Looser
Mimi mwenyewe moyo wangu umesononeka na kuumia Sana wakati naona Magufuli hayuko tayari kuona upinzani nchini.
Magufuli ameua,amefunga wapinzani,amepoteza watu na kujeruhi wapinzani kwa Risasi Leo CDM kirahisi wanasema wanataka maridhiano na CCM hapo wameingizwa chaka,umehalilisha utawala unaokandamiza haki za watanzania.
 
Nimesoma tweets za Zito Kabwe kuhusu kitendo cha Chadema kwenda kushiriki sherehe za uhuru Mwanza. Amewashutumu wapinzani wenzake kuwa wamejipendekeza kwa maoni yao ya kuwa na maridhiano ya kitaifa. Kwa maoni yangu Zito hakutakiwa kushambulia namna ile kama kweli anaamini katika upinzani halisi. Namuona kama mvurugaji tu wa upinzani na mtu anayependa kuonekana wa kipekee katika mambo mengi. Wewe unaonaje? Karibu kwa mjadala.
 
Egnecious, Siku ya ufunguzi wa bunge wakati wapinzani wakitoka ukumbini yeye aliamua kujipendekeza kwa kubaki ndani alitegemea kupata moja ya teuzi
 
kajamaa unafiki kameuanza zamani sana, kuwa nacho makini sana!
Siyo unafiki tu bali kakiwa pale Chuo Kikuu Mlimani kalikuwa ni ka kiongozi ka DARUSO, kalishiriki sana kuwauzia vyumba vya kulala Wanachuo wakati ilikuwa ni haki yao kupewa vyumba bure. Hapo utaona ni kwa namna gani haka ka Zitto ni kajizi na kanafiki. Mbowe kamsaidia sana Zitto kimaisha akiwa pale UDSM,kamjenga kisiasa, kwa kifupi Mbowe ni kama mzazi wa Zitto alipaswa kumhehimu japo kidogo lakini kutoa hiyo lugha ya kwamba anajipendekeza ni utovu wa nidhamu. Na haya ndo tumekuwa tukiwakosoa Wapinzani mara kwa mara kwa kumuita Rais JPM ni mshamba,Dikteta halafu wanajinasibu kwamba ni lugha ya kawaida ya kukosoa,sasa na hili la Zitto la kumwambia Mbowe anajipendekeza, je ni lugha ya kawaida ya kukosoa?
 
Kukataa malidhiano na mtu ambaye ameshasema kuwa ukinilazimisha ndio unapoteza kabisa, mtu mwenye vyombo vya dola vilivyosheheni silaha kadhaa wa kadhaa wakati wewe huna hata nguvu ya kumbonda jiwe hata moja ni kujitakia kifo.
 
Back
Top Bottom