Zitto Kabwe: Kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli ni kujipendekeza na unafiki

Zitto Kabwe: Kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli ni kujipendekeza na unafiki

Pascal Mayalla,
Umefuzu uzushi kiasi hujui maana ya kuomba poo. Maana ya poo unayojaribu kuipenyeza ni ile ya mtaani Unaunga mkono mikakati ya ZZK si bure ni kwa manufaa ya Magu.

CHADEMA ni chama huru cha siasa hakiamriwi wala kushinikizwa mikakati yake nje ya katiba yao inayotekelezwa na viongozi wake halali.

ZZK na timu yake wana haki ya maoni yao mikakati yao ambayo sijamsikia mtu wa CHADEMA amediriki kuishambulia kwa namna yo yote.

Kuheshimiana na kuvumiliana ndiyo matakwa ya demokrasia hata pamoja na kukubaliana na kutokubaliana kimawazo na kimikakati.

Endeleeni kumpotosha Magu namba tunaisoma pamoja tukishuhudia taifa linameguka vipande vipande.
 
Binafsi nampa credit Mh Mbowe, na ndio maana nadhani anastahili kuwa Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani. Kadiri Mbowe. Anavyozidi kuwa MTU mzima ndivyo hekima na busara zinavyoongezeka. Na kwa kauli yake hii ukweli imepoza moto uliokuwa unagukuta Tz, ukweli Mbowe anahitaji siasa na demokrasia ya wazungu na sio hii inayoendelea siasa ya waafrika. Kama kuna kitu kajifunza Mh Mbowe kutoka kwa mzee Lowasa ni kuondoa kinyongo rohoni. Na hii ni credit kubwa kwa wanasiasa wa Afrika.

Waache visasi. Wawe na roho za watoto.

Na kwa kauli hii ya Mh Zitto naamini bado ni kijana, asiye na busara na anastahili kupata semina kutoka kwa wanasaikolojia mfano Dr Elie Waminian, kwani Mh Zitto kile alichoshauri kupingana na Serikali hana uthubutu wa kusimmama mbele kutunishana msuli na serikali.

Waliweza miaka ile vijana wa ngangali, walivyokuwa ngangali. Hadi juma nature akatunga nyimbo kuomba vyama vya fisia na CUF viungane, ili kuepusha umwagaji wa damu. Na ni ushauri wangu kwa vijana wenzangu kama alivyowahi kusema Dr Ellie, huwezi kupigania hali zako kutoka kwa Serikali, Bali njia bora ni kusimamia hali zako
 
Hayo ni maoni ya Zitto Kabwe wa ACTwazalendo ambae ni rafiki yetu na mpinzani mwenzetu

Sisi tuko nyuma ya maridhiano project hata kama yatamkweza mhe Zitto Kabwe ambae maoni yake binafsi (kuwa Mwenyekiti wetu ni mnafiki)na sio ya chama cha ACT wazalendo

Ninaimani maridhiano yakienda vizuri naye atayaona matunda

Umoja ni nguvu
 
Zitto anaweza kuwa na point. Why CHADEMA wanaomba maridhiano sasa? Kwanini hawakuomba hicho wanachoita maridhiano kabla hata ya uporaji uliofanywa na CCM kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa?

Magufuli anaweza kuwapotezea kwanza na kuja kuwajibu December 2020 baada ya kuwa amewapora 98% ya majimbo yote
Watu hata polite language hatuijui, mara ngapi mtu unaenda hotelini unasema naomba unihudumia chakula furani, kama vile hicho chakula unapewa bure wakati unanunua kwa hela yako mwenyewe, au mara ngapi unamwambia mtu naomba unilipe deni langu, wakati hiyo ni hela yako na alikuja mwenywe kukukopa si kwamba ulimbeleza kumpa huo mkopo.
 
Hana point huyo msaliti mkubwa watanzania sio wajinga tunakumbuka mwaka 2009 alivyoongoza genge la wasaliti na kupokea fedha na kugawa kwa hao wasaliti
Zitto anaweza kuwa na point. Why CHADEMA wanaomba maridhiano sasa? Kwanini hawakuomba hicho wanachoita maridhiano kabla hata ya uporaji uliofanywa na CCM kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa?

Magufuli anaweza kuwapotezea kwanza na kuja kuwajibu December 2020 baada ya kuwa amewapora 98% ya majimbo yote
 
Hayo ni maoni ya Zitto Kabwe wa ACTwazalendo ambae ni rafiki yetu na mpinzani mwenzetu

Sisi tuko nyuma ya maridhiano project hata kama yatamkweza mhe Zitto Kabwe ambae maoni yake binafsi (kuwa Mwenyekiti wetu ni mnafiki)na sio ya chama cha ACT wazalendo

Ninaimani maridhiano yakienda vizuri naye atayaona matunda

Umoja ni nguvu
Una MOYO
 
Nilichogundua wafuasi wa Chadema hawana tofauti na wa CCM. Wote walewale tu!
 
Zito Kabwe kama kweli una nia nzuri na Wananchi wa Tanzania tolea ufafanuzi kuhusu wewe kwenda kuchukua mabulungutu ya pesa Ikulu wakati wa JMK alipokuwa madarakani baada ya kuikosoa Serikali yake. Pili Tolea maelezo pesa zote ambazo ulipewa au kukopa kupitia NSSF. La mwisho tolea ufafanuzi kuhusu majungu ya kumzushia JPM kifo mara alipotoka kwenye ziara ya Luangwa na kusambaza video fake..
 
Zitto kapanic kwa lile walilofanya CHADEMA jana, kashtukizwa hakutegemea, anatamani ile nafasi ingekuwa yake kwa tabia zake za ki_opportunist, toka jana ni twitter, insta habanduki huko, eti leo Zitto anataka siasa za mapambano anawafundisha CHADEMA!, wonders shall never end, wakati ule anaenda kukutana na JK watu wanamuuliza kulikoni anasema JK ni sawa na babake, vipi leo Magufuli sio sawa na babake pia?!

wewe fuata upepo,

JK Mbowe aliomba maridhiano? why?

ukijibu swali hili unywe panadol

so mbowe kafanya kwa JPM kwa sababu zitto alifanya kwa JK

Yaani hasira za vionogiz wa juu wa chadema, na viongozi wa serikali za mitaa wote waliokatwa ni wajinga kuliko wewe unayeleta story za kuunga unga?
 
Zito Kabwe kama kweli una nia nzuri na Wananchi wa Tanzania tolea ufafanuzi kuhusu wewe kwenda kuchukua mabulungutu ya pesa Ikulu wakati wa JMK alipokuwa madarakani baada ya kuikosoa Serikali yake. Pili Tolea maelezo pesa zote ambazo ulipewa au kukopa kupitia NSSF. La mwisho tolea ufafanuzi kuhusu majungu ya kumzushia JPM kifo mara alipotoka kwenye ziara ya Luangwa na kusambaza video fake..

wewe ndio mswahili

aliyesema lichukua hela, ndio aweke uthibitisho

yaani ukinikuta na mama yako namuibia baba yako, najianika? si wewe uliyekuwa una record unaweka uthibitisho?

grow up
 
Nitakuwa wa mwisho kumwamini Zitto, huyu ni muongo kupitiliza, huyu hata CCM wanamjua hamaanishi lolote bali anawauza wenzake ilhsli yeye usiku anakula meza moja na ccm

UNA UTHIBITISHO wa unachosema? au ndio mwendelezo wa kuaminishwa na mbowe tangia enzi hizo zitto anataka uenyekiti??

with all these technology and flow of information, hauna hata PICHA? AUDIO?

Acheni hizo

MBOWE KAWAUZA TENA
 
Back
Top Bottom