Zitto Kabwe: Mahakama imetoa uamuzi kuwa Rais John Magufuli alivunja Katiba alipomuondoa Prof. Mussa Assad kama CAG

Zitto na genge lake Udini unawasumbua sana.

Acheni siasa za kupambana na Ukristo pimbi nyie
Hebu punguza jazba kwani hao majaji waliotoa hukumu wote ni waislamu?

Hapa unapiganiwa mfumo ambao utawafaidisha wote watakaoteuliwa katika cheo hicho na wala siyo huyo Assad kwani yeye ndiyo imeshatoka hiyo.

Hivi tuseme wakati Mtikila alipokuwa anapigania haki ya kuweka mgombea bila ya kuwa na chama alikuwa anapigania mfumo kristo?
 
Mkuu hao watu wana matatizo kwenye ubongo, unakuta mtu hana mbele wala nyuma huyo Magufuli hakuwa akimjua ila et nae anakwambia alikuwa anaishi kwa hofu ya kuogopa kutekwa na Magufuli.

Kwa taarifa yako kuna watu kibao wamefungwa, kuumizwa, kuharibiwa mali zao ambao hata Magufuli alikuwa hawajui. Kilichowaumiza ni huo mfumo wake wa utawala, na wala sio lazima iwe aliwahujumu yeye personal.

Mbona kuna watu wanasema walifaidika na miradi kadhaa ya utawala wa Magufuli, kwani hao wote alikuwa anawajua? Au hujui unaongea nini boss?
 
Basi hayo hata sasa yapo na huwa tunasema wanamuharibia Mama samia hatusemi mwenyewe Samia kafanya wala mfumo wake wa uongozi.

Polisi wanabambikia watu kesi za kuvunja na kuiba kwa kutumia silaha yani wanafanya kama mchezo tu, nina ndugu yangu yupo segerea anangaika na kesi hiyo ya kupewa na polisi.
 
Huyo jaji masoud ni kilaza wa kutupwa.
 
Kwann umwamini ndugu Zitto ?
Huwa ni kigeugeu anaangalia sana maslahi yake . Kitendo cha kusema kuwa Tume huru ya uchaguzi kwanza kabla ya katiba, ilinipa wasiwasi na dhamira ya Zitto katika kupigania demokrasia ya kweli. Kwa vile zanzibar wako serikalini, hivyo anataka uchaguzi ufanyike kwa kutumia tume huru , maana atapata wabunge na hivyo ruzuku, madaraka and the like.
 
Ndugu kila kitu sio udini, tukiwa hivyo mbona tujiharibia utu wetu.

Je, tunaweza sema Marehemu Magufuli alimuondoa Assad kwa sababu ya dini yake?

Hapana Magufuli alimuondoa Assad kwa sababu maono yao yalitafautiana sana.
Hakuna cha nini wala nini Assad na Zitto ni wadini tena walio kubuu.Kama unakumbuka Assad akiwa mkuu wa chuo kikuu Dodoma ndiye aliyeasisi kujengwa kwa msikiti maeneo ya chuo Magufuli alipokataa taasis za dini kuchangamana na taasisi za elimu za serikali ndo mgogoro ulipoanzia na Assad kawa anamtumia Zitto kama kuikomoa serikali ya Magufuli kama unakumbuka mpaka report ya CAG ikavuja kabla ya kusomwa bungeni.Kama Zitto sio mdini aende akamuunge mkono Mzee Mbatia kuhusu kesi ya kuondolea Spika Ndugai bila kufata katiba.
 
Magufuli alikuwa ni mvunja katiba mkubwa. Ila hizo mahakama kama angekuwa hai bado zingetoa hukumu ya kumfurahisha. Bila katiba mpya tena kwa njia ya machafuko, tusitegemee hatua zozote kuchukuliwa kwa hawa walevi wa madaraka.
Cc: UHURU JR
Machafuko unayaweza?
Umejipanga?
Unauwezo wa kukaa ughaibuni mpka yaishe?
Usiombe gari usiloweza endesha litakuua bure.
Hapo tu hamna machafuko unahaha kutafutia vingedere vyako chakula je kukichafuka si vitakufa ukiviona[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] muda mwingine sio lazima kuropoka wakati hujui athari za machafuko na yakitokea kuyazima ni kazi sana libya mpka leo miaka 11 imepita hakuna nafuu yoyote kuna miundo mbinu mpka leo haijatengamaa ww unaomba machafuko dah mtu wa hovyo sana
 
Huyo jaji masoud ni kilaza wa kutupwa.
Hakuna kitu ni Udini tu.Kama sio udini huyo Zitto akafungue kesi kuhusu kuondolewa Spika Ndugai bila kufata katiba au amuunge mkono Mbatia kwenye kesi aliyoifungua Mbatia kuhusu kutofatwa katiba katika kuondolewa kwa spika.
 

Mimi tayari siishi kwa raha, watakaoteseka ni hawa wanaokula kwa ulaini. Ngoja yatokee uone nani watakaoteseka. Na mwisho wa hayo machafuko heshima itarudi.
 
Zitto na genge lake Udini unawasumbua sana.

Acheni siasa za kupambana na Ukristo pimbi nyie
Kabisa huyu ZZK ni mfia dini anapenda kusimamia ishu za wavaaa dontachi, hafai kuwa kiongozi wa chama...naona awamu yao sasa.
 
Yaani nikuteue mimi halafu nishindwe kukupiga chini ! Nitakuwa mkuu wa nchi au mkuu wa wilaya !
 
Hakuna kitu ni Udini tu.Kama sio udini huyo Zitto akafungue kesi kuhusu kuondolewa Spika Ndugai bila kufata katiba au amuunge mkono Mbatia kwenye kesi aliyoifungua Mbatia kuhusu kutofatwa katiba katika kuondolewa kwa spika.
Uko sahihi
 
Hapa ni swala la semantics tu. Kesi hiyo ilikuwa ni ya kikatiba na ilihusu uhalali wa sheria iliyotumika kumwondoa CAG madarakani, haikuwa inahusu mamlaka ya rais kumwondoa CAG madarakani kwa kutumia sheria hiyo iliyopingwa. Kwa hiyo kumwinganisha Magufuli kwenye hukumu hiyo ni makosa kwani yeye hakuwa mshitakiwa.

Hukumu inasema kuwa kifungu cha 6(1) cha sheria iliyotumika kumvua madaraka kinakinzanana na kifungu cha 144(1) cha Katiba, haisemi kuwa mtu aliyemvua madaraka kwa kutumia kifungu hicho alivunja katiba. Ndipo swala la kuwa na Katiba iliyonyooka linakuja tena. Katiba hiyo hiyo inalipa bunge mamlaka ya kutunga sheria zinazotawala utumishi wa CAG ambapo kifungu hicho kilitungwa na Bunge kwa mujibu wa Katiba hiyo hiyo hiyo.
 
Wadau NAWASALIMU.
Naamini Mtakumbuka ile KAULI ya Aliyekuwa CAG Prof.ASSAD aliyoitoa baada ya Kuondolewa kwenye Nafasi ya kuwa CAG na pia Pale Alipoitwa BUNGENI na SPIKA aliyelazimishwa KUJIUZULU kutokana na KUROPOKA kwake Bw.NDUGAI
Prof ASSAD alisema
ASILIMIA 60% ya VIONGOZI HAWANA UWEZO
Jana IMETHIBITIKA MSHAKAMA KUU baada ya RAIS MAGUFULI kuthibitika kuwa ALIVUNJA KATIBA huku MWANASHERIA MKUU wa SERIKALI akishuhudia kwa KUMWONDOA ktk NAFASI yake Prof ASSAD ya CAG.
Ukweli ni AIBU KUBWA.
 
Hapo ndio utajua kuna hataree kwa nchi yetu inapotokea mtu anakuwa na nguvu kuliko maslahi ya Taifa, lakini pia ndio utajua kuwa hatuna Taasisi imara zenye uwezo wa kulinda maslahi ya Taifa!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…