Chadema mnajiona wanyonge mbele ya kila mtu!
Sisi tulifikiri ni kwa wazungu tu kumbe hata kwa wakenya? Au kwa vile wanaongea sana Kingereza?
Ngoja niongezee mambo machache
1. Ni kweli Kenya imekua tegemezi kwa mazao ya nafaka kutoka Tanzania tangu uhuru. Kuna watu wanadhani utegemezi huo hauwezi kuisha. Si kweli. Bei wanayonunua Mexico ni ndogo mara 3 ya bei waliyokua wakinunua hapa nchini. Kwahiyo kibiashara si rahisi kurudi.
The Standard wameripoti kuwa mwezi huu Kenya imeingiza tani 2M, na mwezi December waliingiza tani 2M zingine. Lakini mahitaji yao kwa mwaka ni tani 3.6M kwahiyo wana ziada ya tani laki 6. Hivi hapa wanarudije kwetu?
2. Hoja kwamba tutauza nchi zingine nayo ni kujipa matumaini tu. Mbona 2017 tulihangaika kutafuta soko hadi mahindi yakaharibika? Hizo nchi zingine hazikuwepo? Tusitoe majibu mepesi kwa maswali magumu. Manji alipoacha kununua Mbaazi tulisema serikali itanunua na kupeleka huko anakopelekaga Manji. Lakini nini kilitokea? Bei imeporomoka kutoka 3,000/= hadi TZS 200/= kwa kilo. Korosho mnakumbuka pia kilichotokea? Kwahiyo tusijipe matumaini. Hali itakua mbaya. Ni kilio kwa wakulima wa mahindi.
3. Kitengo chetu cha ujasusi wa kiuchumi (Economic intelligence) kimepwaya. Wakenya wametumia hii loophole kutupiga za uso. Kwanza wametafuta mahindi ya bei rahisi huko duniani, sisi wala hatuna habari. Wamenunua stock kubwa makachero wetu wala hawakushtuka. Walikua busy kuangalia account ya Mbowe ina kiasi gani na anaishije baada ya ubunge. Tunafeli sana kwenye ujasusi wa kiuchumi.
4. Hatuwezi kupata soko jingine nje ya nchi kwa sababu Kenya wametuchafua. Kwenye taarifa yao wamesema mahindi kutoka Tanzania yana sumu kuvu (aflatoxin) inayosababisha kansa. Sasa ni nchi gani itakubali kununua mahindi yetu watu wake wakaugue kansa?
5. Hii ni vita ya kibiashara. Kama kweli Wakenya ni ndugu zetu na tumewalisha kwa miaka 60 walitakiwa watueleze kindugu. Kama wameona tatizo kwenye mahindi watuambie, sio kuitangazia dunia. Juzi kulikua na kikao cha wakuu wa nchi za EAC, je walishindwa kutuambia kuwa mahindi yetu ni substandard? Kwanini hawakusema kwenye kikao wamekuja kuongea hadharani ili dunia nzima ijue? Lengo lao ni nini?
6. Mkataba wa ushirikiano wa EAC unaeleza bidhaa ikishathibitishwa na shirika moja la viwango inaweza kutumika nchi yoyote ya EAC bila kuthibitishwa tena. Mahindi yetu yakifika mpakani yanakagukiwa na TBS. Yale yenye viwango tu ndio huruhusiwa kuvuka. Sasa kwanini yakifika Kenya yanakaguliwa tena? Je wakenya hawatuamini? Mbona wao bidhaa zao zikija hapa na mhuri wa KEBS hatukagui tena?
7. Kama kweli mahindi yetu yangekua na sumu kuvu (aflatoxin) TBS walipaswa wawe wa kwanza kugundua. Sio yanapita mpakani halafu sumu inagunduliwa Kenya. Hii inaashiria mambo matatu. Either madai ya Kenya ni uongo, au uwezo wa TBS ni mdogo, au Maafisa wa TBS mpakani wanapiga hela kupitisha mazao yaliyo chini ya kiwango. Uchunguzi ufanyike hatua zichukuliwe.
8. Ukiachana na mahindi, Kenya bado ni tegemezi kwetu kwa mazao mengine ya chakula. Ukienda Mang'ola utakuta malori ya Wakenya yanabeba vitunguu, kule West Kilimanjaro malori yamebeba karoti, hoho na viazi. Kwahiyo kama wamejipanga kwenye mahindi, wanatakiwa kujipanga kwenye mazao mengine pia. Tukiamua kuzuia mazao mengine watakula ugali bila mboga. 2017 walipata Sembe crisis sasa hivi watapata matembele crisis.
9. Kenya ni nchi ya pili inayofanya biashara na sisi yenye value kubwa baada ya Uingereza. Pita kwenye supermarkets utaona bidhaa nyingi ni kutoka Kenya. Kwahiyo tukiamua kupiga counter attack tukazuia bidhaa zao kuja kwetu watapoteza market share kubwa sana na watanyoosha mikono.
10. Chokochoko hizi zinaweza kuvuruga tena Jumuiya ya Afrika mashariki. Kumbuka chokochoko kama hizi ndio ziliivunja Jumuiya mwaka 1977. Ni muhimu viongozi wakae na kuchukua hatua. Uchunguzi ufanyike kuhusu madai ya Kenya. Kama kweli mahindi yetu yana sumu kuvu (aflatoxin) TBS waulizwe yalipitaje mpakani? Kama si kweli basi Kenya watuombe radhi maana wametuharibia soko hata kwa nchi zingine.
Pia kwa kipindi hiki cha mpito serikali iwanusuru wakulima kwa kununua mahindi yao kwa bei ileile waliyokua wakinunua Wakenya. Mahindi hayo yahifadhiwe kwenye ghala la taifa, yatatufaa baadae. Vinginevyo itatokea deflation kubwa sana. Gunia moja moja la mahindi litauzwa bei ya chips kavu.
Mwenye masikio na asikie.!!