Zitto Kabwe: Mahindi ya Tanzania ni salama

Zitto Kabwe: Mahindi ya Tanzania ni salama

Mlivyochoma vifaranga vyao 6000 nakutaifisha ng'ombe zao mliwaeleza kindugu? Mkuki kwa nguruwe ...
 
Akuna muda wa kubembeleza nyang'au ni kuwapa salamu tu,dawa ya moto ni moto.
 
Serikali ipi Kaka zitto? kwani tuna serikali? si mlituambia hakukwa na uchaguzi bali uchafuzi sasa serikali imetoka wapi?
 
Ukiwaangalia siasa zinazoendelea nchini Kenya kuhusu bei ya Gunia (90 kg) ...wakulima wanataka walipwe sh 3,640 kwa gunia na wanalalamika kwamba kwa sasa wana mahindi mengi sana plus kwamba 2022 wana uchaguzi basi wakulima wamewakamata wana siasa

Sasa upo uwezekano wa serikali yao kutumia njia hii ya kusema kwamba mahindi yetu yana sumu ili kuwazuia wafanya biashara watanzania wasipeleke mahindi kenya ili kuwalinda wakulima wao ...lakini haya nayaandika ila sijathibisha ...

Kenya ilipata wakati mgumu kipindi kile tumezuia ghafla kuwauzia mahindi, wao walijipanga vizuri mahindi wanatoa mexico na kule wananunua kilo moja shilingi 180 hadi 200 kwa pesa ya Tanzania, wakaingia makubaliano na zambia ili wawe wanawapelekea mahindi yao na ukumbuke zambia kwa sasa hizalisha mahindi mengi na bora na masafi kwani 90% ya settlers wote wa zimbabwe walikimbilia zambia na walipewa maeneo bure kabisa, sasa kwenye mahindi walitusoma mapema na wakaamua ndio maana unaona wanajiamini kusema hivo. Zaidi tukiwabembeleza watakuja kununua kwa bei wanayoitaka wao na kibiashara watakua wameshinda.
 
Hivi ni lazima muuze mahindi yenu Kenya

Biashara iliisha zamani, karanga nyekundu inachukuliwa malawi kwenda kenya na wamalawi hurudi na bidhaa za viwandani ikiwamo mafuta ya kula, mahindi yanatoka zambia ambapo wazungu waliokua zimbabwe wako pale mahindi yao bora na masafi sasa Tanzania hatuna soko la mahindi zaidi ya kenya kwa sababu mzambia anauza pia Congo, Burundi market volume ni ndogo unategemea nini? Kwenye hili Chadema wasihusishwe hapa tuangalie uhalisia na sio siasa zetu za ndani
 
Wako wapi wale wapumbavu walikuwa wakipiga makelele eti wakenya sisi ndio tunawalisha, haya mnaemlisha kasema hataki chakula chenu, mnapagawa nini tena? Kaangeni bisi mle, hapo ndio mtajua umuhimu wa masoko na kuyaheshimu
Mkuu ni suala la mda tu, mahindi tutauza vizuri tu.
Unadhani Wakenya zsidi ya milioni 50 wasubili mahindi kutoka Mexico?
Na yale yanazalisha pumba za kutosha balaa, hasara kwa wanaosaga na kukoboa
 
Majibu yatoke wizara ya kilimo kuliko kwa huyo Zitto kabwe.

Kama walivofanya wakenya.

Zitto aache tabia za wanasiasa '"mediocre" kuzungumzia kila kitu. Yes, ni diplomacy, ola angehimiza wizara ya kilimo kupitia wakala wa utafiti wajibu barua ya Kenya kwa facts. Sio kuzungumzia diplomacy kwenye research za wengine.
Barua ya wakenya ni ya ndani haijaandikiwa serikari yetu huwezi ijibu ,mimi nazani taasisi zinazohusika na ubora wa chakula za kenya na tanzania zikutane na wachukue sampuli wapime waje na majibu ya kutoka maabala
 
Kuna mambo watu wanafanya kwa kujifunza. Unafanya Jambo la Kwanza, unajikuta umekosea Mara ya pili bado umekosea na unaendelea Tena kukosea basi Hilo halitakuwa Tena Jambo la kujifunza Bali utakuwa unafanya makusudi au kichwa Cha panzi.

Iweje Jambo likosewe kwenye mahindi,korosho na mbaazi bado tuite mtu alifanya makosa. Ingekuwa Ni mtu anasimamia biashara yako anafanya yote haya nadhani isingekuwa rahisi kudhani Ni makosa badala yeke makusudi ndo ingechukua nafasi.

Biashara za watu zimeharibika kutokana na matamko ya kwenye majukwaa bila kuatafakari athari za kibiashara za watu.
 
Mbona unatuchanganya Mkuu?
Ningetegemea baada ya kukiri kuwa mahindi yanayolimwa Manyara na Dodoma kweli yana sumu, ungetaka kujua kwa nini bado yanaingia kwenye soko. Kama kuna sehemu ambayo inajulikana kuwa mazao yao yanakuwa na sumu basi ni busara kwa Kenya kuzuia mahindi yote maana uwezekano wa kuingizwa yenye sumu kinyemela ni mkubwa. Kama ulivyosema kuwa wajibu wa serikali yetu ni kwa watanzania, vile vile wajibu wa serikali ya Kenya ni kwa wakenya. Ni wajibu wetu sisi kuwahakikishia kuwa tumedhibiti uuzwaji wa mahindi yenye sumu nchini mwetu na sio wa kwao wa kuanza kuulizia haya mahindi yametoka mkoa gani. Tujifunze kwa wenzetu ambao wakigundua tatizo kwenye ndege moja tu basi ndege zote za aina hiyo zinazuiwa kuruka.

Badala ya kuwalalamikia wakenya inabidi tuwaulize wanaohusika kwa nini mahindi yenye sumu kutoka Dodoma na Manyara yanaingia kwenye soko letu? Kwa nini afya na uhai wa mtanzania usithaminiwe kama wenzetu wanavyothamini uhai wa raia wao.
Hayo ya mahindi ya Mexico hayana tija maana Kenya wana uhuru wa kuagiza mahindi kokote wanakotaka. Hata kama yana pumba sana. Tija itakuwepo kama utaweza kuthibitisha kuwa ama mahindi yetu hayajawahi kuwa na sumu au mahindi ya kutoka Mexico yana sumu lakini wanayafungia macho.

Mimi nadhani tunastahili kuwashukuru wakenya kwenye hili badala ya kuwabeza.

Amandla....
 
Back
Top Bottom